Korea Kaskazini yarusha ndegevita zaidi ya 200 jirani na mpaka wa Korea Kusini

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Vikosi vya kijeshi vya Seoul vilisema karibu ndege 200 za jeshi la Korea Kaskazini ziligunduliwa kwenye rada zikiwa angani siku ya Ijumaa

E0DDF4C1-FFF7-491D-93DA-CE23553F1E78.jpeg

Jeshi la Korea Kusini limesema kuwa Korea Kusini ilirusha makumi ya ndege za kivita baada ya kuona idadi kubwa ya ndege za kivita za Korea Kaskazini kwenye rada, jeshi la nchi hiyo lilisema. Tukio hilo lilitokea wakati wa mazoezi ya anga ya Seoul na Washington, ambayo yamesababisha maonyesho kadhaa ya nguvu toka Pyongyang katika siku za hivi karibuni.

Wakuu wa Pamoja wa Jeshi la Korea Kusini (JCS) walisema ndege 80 zilikusanywa siku ya Ijumaa kujibu zaidi ya safari 180 za kijeshi za Korea Kaskazini, na kubainisha kuwa ndege hizo za Pyongyang hazikukaribia mpaka kati wa Korea Kaskazini-Kusini

JCS iliongeza kuwa F-35A zilizotengenezwa na Marekani ni miongoni mwa ndege za Korea Kusini zilizorushwa, na kwamba jeshi lilikuwa katika "mkao kamili wa kujibu."

Wakati Seoul ikitoa maelezo machache kuhusu safari za ndege za Korea Kaskazini, maafisa walisema vurugu hizo za Pyongyang zilibakia kaskazini mwa Mstari wa mpaka wa Kijeshi unaotenganisha Korea hizo mbili.

Ndege hizo za Kusini zilirushwa pia mwezi uliopita kwa jibu kama hilo baada ya ndege 10 za Korea Kaskazini kuonekana kwenye rada, ingawa tukio hilo pia lilimalizika bila kuongezeka kwa mgogoro zaidi.

Mvutano umeongezeka kwenye Rasi ya Korea katika miezi ya hivi karibuni, huku Kaskazini ikitekeleza rekodi ya majaribio ya silaha mwaka huu - ikiwa ni pamoja na kombora la masafa marefu (ICBM) lililorushwa baharini mapema wiki hii. Wakati huo huo, Seoul, imefanya duru kadhaa za mazoezi ya kijeshi ya moto na Marekani, ikiwa ni pamoja na zoezi linaloendelea la 'Vigilant Storm', zoezi kubwa zaidi la anga kuwahi kufanywa kati ya washirika hao wawili. Pyongyang mara kwa mara imelaani mazoezi hayo kama maandalizi ya shambulio kwa Pyongyang, huku Washington na Kusini zikisema Korea Kaskazini imejihusisha na "chokozi" hatari za majaribio yake ya kulipiza kisasi kwa kurusha Makombora kinyume na utaratibu.

Aisee ndege 200?

Air denfense lazima izidiwe tu
Tunaaminishwa Korea kaskazini ni masikini wa kutupwa. Sasa sijui anawezaje kurusha modern military aircraft 200 kwa mpigo, achilia mbali ICBM missiles anazotengeneza kila siku!

Na hapo kama zimerushwa 200, basi lazima zipo zaidi ya hizo. Maana hakuna mwehu anaeweza kurusha ndege zake zote kwa pamoja.
 
Putini alikuwa na ndaro zaidi ya hizo za korea kaskazini lakini sasa miezi 8 tu ata mwaka haukufika ya vita anaazima silaha kutoka Iran taaban nafsi yake

Kila mara nawahojiMerika hapa - ebu tupatie ufafanuzi wa kilidhisha: hivi jeshi la Merikani iliwachukua miaka mingapi kupigana vita huko VietNam,je,walifanikiwa kuwashinda wa VietCong au Wamerikani walisepa huku tails zao zikiwa between their legs - hayo hamuyakumbuki, badala yake masaa yote kazi ni kumunanga Putin pamoja na jeshi la Urusi kwamba si lolote si chochote, kisa? Kwa nini anawachukua muda mrefu kupigana huko Ukraine - yaani miezi minane ya mapigano mnaona ni muda mrefu, lakini Merikani kutumia miaka kumi ikipigana huko VietNam na wakashindwa na kudhalilishwa na wapiganaji wa VietCong hilo hamlisemi au mnajifanya kulisahau!!!

By the way historia inaonyesha kwamba US ilianza kujiingiza kwenye suala la VietNam ikishirikiana na Wafaransa tangu 1955, wafaransa walipo bwaga manyanga Uncle SAM ndio kajiingiza kichwa kichwa zaidi kwenye suala zima la VietNam in 1965, matokeo yake mbona yanajulikana Dunia nzima hata kwa watoto wadogo hisipo kuwa kwa baadhi ya Watanzania wachache ambao ni wabishi by default.
 
Malengo ni tofauti sana US na Vietnam miaka hiyo na Russia na Ukraine
 
Tunaaminishwa Korea kaskazini ni masikini wa kutupwa. Sasa sijui anawezaje kurusha modern military aircraft 200 kwa mpigo, achilia mbali ICBM missiles anazotengeneza kila siku!

Na hapo kama zimerushwa 200, basi lazima zipo zaidi ya hizo. Maana hakuna mwehu anaeweza kurusha ndege zake zote kwa pamoja.
Unapoambiwa ni masikini haimaanishi anaringana na sisi huku.
 
Uwanja wa vita ndio umedhihirisha ukweli huo ata ukiwa na unazi pia
Wewe Upo uwanja wa vita?

Kwa hiyo Urussi imeishiwa Ndege na Silaha?

Kwani silaha za US zote zinatengenezwa na Serikali ya US.

Toa unazi wako bhana. Hata kama mnazi basi ongea sense ueleweke siyo kuropoka kama kijijiweni.

HUU UZI UNAMHUSU MRUSSI AMA?
 
Back
Top Bottom