Kumkopesha mtu shida sana,
Mimi wiki kama 2 kuna jamaa alinifata home usiku akaniomba nimsaidoe kiasi kidogo cha fedha alikuwa mpole sana na mnyenyekevu nikamwambia sina.
Akanifata tena siku iliyofata akiwa na mtoto wake anatia huruma kwamba mtoto anaumwa akanisisitiza nimkopeshe atanirudishia baada ya wiki moja.
Imefika wiki simuoni nikaanza kumtafuta nikikutana naye ananiambia hana hela hajapata. Ananiahidi kesho ,ikifika hiyo kesho aliyosema haji naanza kumtafuta nikimpata ananijibu hajapata ananipa ahadi ambazo hatekelezi.
Yaani ikawa mimi ndio namtafuta namdai .
Jinsi ambavyo sipendi kufatilia watu nimeamua kumchunia kila akiniona anajistukia saa nyingine anajificha wakati mimi nishamuona na mimi nampotezea.
Kukopesha watu imekuwa jau sana .
Unapata kazi ya kuanza kumfatilia akulipe wakati alipokuwa anashida yeye ndiye alikutafuta