Kongamano vijana wa Mkoa wa vyuo Vikuu TBC1

Kongamano vijana wa Mkoa wa vyuo Vikuu TBC1

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
241
TBC..Televisheni ya Taifa inaonesha kongamano la vijana wa vyuo vikuu wa CCM.

Ni aibu na fedheha kwa chombo cha Umma kutumika kisiasa au kutumiwa na wanasiasa.

Ni chombo cha Umma, inafaa kitumiwe kueneza maslahi ya Umma si maslahi ya Chama tawala. Chama tawala au Chama chochote si umma bali sehemu ya umma.

TBC igeni mfano wa VOA, BBC, Press Tv etc na huo ushabiki, waachieni Radio Uhuru
 
Nape anasema Tanzania hakuna upinzani wa kweli bali kuna waganga njaa tu.

Anasema vyama vya upinzani ni vyama vya matukio tu na tukio likipita ndio basi.

Anasema kwakuwa wameungana basi kazi inakuwa rahisi kwani unapiga risasi moja tu unaua watatu kwa mpigo.Anawaita wahuni.

Anasema kuna wazee wanapiga kelele kudai Tanganyika wakati wamefaida muundo huo wa serikali 2.Kaongeza vijana wanaodai serikali ya Tanganyika ni washamba tu na ni vijana wa juzi tena wananuka maziwa na akatoa mfano wa BAVICHA.
 
Tbc inatumika na wanaccm watakavyo! Tbc ni mali ya ccm na sio watanzania wote!
 
Watanzania tuna kila sababu ya kuiombea UKAWA ili umoja wao ufanikishe azma ya kuiondoa CCM madarakani,tuanze maisha yenye utu na mipangilio bora ya Maendeleo.TBC wataihama CCM baada ya kuondoka Madarakani kwa hiyo isikupe tabu.
 
Mbona kila kitu mnaangalia kwa jicho la kisiasa zaidi?
 
Karibu kwenye live update,nimeamua kujitoa fahamu iliweze kuhudhuria huu mkutano!!!Baada ya salaam na utambulisho,ndugu Nape nnauye aanza kuchamba wa pinzani awafananisha na Yona wa biblia,asema wako wazee wanapiga kelele wakati wamefaidi matunda ya serekali 2 baada hotuba isiyofanana na usemi wa mwalimu "Argue,don't shout".**********Zinafuata salaamu kutoka viongozi wa CCm vyuo,ni dhahiri hawa vijana uwezo kufikiri ni mdogo hata uwezo wa kuwasilisha hoja unatia shaka uwezo uhai wa chama hapo baadae!!!
 
Sema KONGAMANO LA WACHUMIA TUMBO NA WATOTO WA MAFISADI, Kijana anayejitambua mzalendo kwa taifa lake hawezi kukusanyika hapo.
 
Hawa vijana wanaosema ni wasomi nina uhakika ni wajinga asilimia mia moja!!!
 
Vijana wanaoiunga mkono mkono ccm wako very strong mentally and phisically. Duh!! huwezi kuwalinganisha na waleee wavuta bangi
 
Wanacheza taarabu tu! Kuna haja ya kuendesha operesheni maalum kupima ufahamu wa hawa wanalumumba...Zero brain imetamalaki sana Lumumba!
 
Nawacheki! jamaa akisema CCM OYEEEEEEEE! wanaitikia wachache tu!
 
Katiba ya wahuni haitapita..Zaidi itachomwa hadharani!!
 
nimepewe 10,000 ili mihudhurie
ila nimekula kona mbaya
 
Vijana wamefatwa vyuoni kwao wamepakiwa na magari mpaka mlimani city wamepewa tshirt,chakula na nauli wakiambiwa katiba mpya wao wanaitikia TUMEIPOKEA,TUMEIELEWA NA TUNAIUNGA MKONO,huo ndo ujumbe waliotumiwa hawa wanaojiita wasomi wa chama cha mapindu
 
Nawacheki! jamaa akisema CCM OYEEEEEEEE! wanaitikia wachache tu!

Tatizo wamepewa!! chochote kwenda pale lakn ukweli wanaujua moyoni ndiyo maana hawataki.

ccm na tbc1 wanaihujumu nchi
 
Back
Top Bottom