G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 12,486
- 39,965
Ninajaribu kuangalia kama nitaona ubunifu na mawazo huru toka kwa vijana wa ccm. Kwa bahati mbaya ninachokiona ni ile tabia ya tokea kwa Nyerere kuwalisha watu kauli mbiu bila kujenga hoja za ushawishi. Nimemsikiliza huyu katibu nadhani wa vijana toka moshi akisoma tu hasara za serekali3 kama zilivyoainishwa na tume ma kisha akasoma faida za serekali 2 tu kama zilivyoainishwa na tume. Najiuliza kama sio maigizo mbona hakusoma hasara za serekali 2 na faida za serekali 3!?
Labda sio lazima asome nipendavyo mimi, lakini kipindi nadhani kinaongozwa na wasomi na taswira ya taifa letu kwa wasomi. Hivi kwa,kuwasomea watu faida za muundo unaoutaka bila kuwaambia pia mapungufu yake ni usomi huo? Haya labda wataenda kwa wananchi kuipigia debe hiyo katiba pendekezwa, wakikutana na watu wanaotaka ulinganifu wa faida na hasara za miundo yote miwili tutegemee wasomi wetu kushawishi kwa hoja? Ama itabidi waende na jeshi la polisi kuzuia maswali wasiyoyataka?
Watanzania hapa inabidi tujifunze kitu kikubwa sana, tumekuwa na tabia ya kuchagua viongozi kwa kusikiliza kauli mbiu bila kuhoji maswali ya msingi, wakati wa kampeni unakuta vikundi vya burudani vinatumia masaa 3. Salamu za timu ya kampeni lisaa limoja, anayetaka kuchaguliwa anaongea dakika chini ya 15!! Kichekesho kiko kwenye maswali kwa mgombea. Anaulizwa maswali matatu tena ya watu waliopangwa wanamuuliza tukikuchagua utatufanyia nini. Yeye anajibu nitawaletea maji, umeme, barabara na amani. Watu wote mayowe bila kumuuliza utawezaje na lini na nini kilikushinda muda wote uliokaa madarakani? Baada ya hapo ni nderemo vifijo, chakula, kugaiwa tshirt, kofia nk. Hapo anasubiri kura yake na ikishindikana siku ya kura jeshi la polisi linatumika kumpitisha chini ya tume isiyo huru. Hiyo ndio hali halisi na tatizo hili tunaliona hata kwa hawa wanaojiita wasomi, eti wanakauli mbiu katiba pendekezwa tumeipokea, tumeielewa (kumbuka hawasemi tumeisoma) na tumeikubali!!
Mkuu, huyu jamaa niliishi naye mabibo hostel mwaka 2011 ila alifukuzwa chuo kutokana na tabia za kuchukulia mambo juujuu kama alivyofanya leo! Wakati wa vurugu za Arusha ambazo watu walipigwa risasi kuna jambo aliongea kwa kweli nilimchapa sana kutokana na ujinga wake! Huyu ni usalama wa taifa na ni ndugu na Beno Malisa..Hovyo sana.Hajui kuwa wakati Warioba akiainisha alitoa hasara za kila upande na ikabainika serikali mbili ndiyo hasara
zaidi? Hovyo kabisa hawa watu na haya maneno ndo wanaenda kuwalisha watu wenye uelewa mdogo huko vijijini! Achilia mbali maadili na tunu za taifa.Katiba haina meno kabisa kisheria na muundo wa serikali wa hovyohovyo! Nitakata mtu walahi! Tukutane majukwaani tuelezane ukweli!!!