kongamano la katiba UDSM Lahujumiwa

Kiranja

JF-Expert Member
May 19, 2007
751
336
katika hali ya kushitua na kushangaza,kesho wakati UDSM wakiwa wameamua kuwa na kongamano kubwa la kujadili uwepo wa katiba mpya,lipo kundi la watu ambao wanadai kuwa ni waislamu na wao wameamua kuitisha kongamano lao kesho ktk ukumbi wa karimjee na wanategemea kutoa matamko mbalimbali lengo ni kuhakikisha kuwa media itaondoa attention kwenye katiba. pia watatoa matamko controversial sana juu ya utawala kuwa JK na serikali yake inahujumiwa na wakristo. pindi tamko likikamilika litawekwa hapa jamvini kwani ndio draft ya kwanza imekuwa tayari. ukumbi wa karimjee umelipiwa na mnene mmoja serikalini. leo mahubiri kwenye misikiti kadhaa DSM yamekuwa yakionyesha kuwa kila mara anapokuwa rais muislam basi anawekewa vikwazo na hata kudhalilishwa na wametoa mifano mingi ya Mwinyi na sasa JK.More 2 come later
 
Hatutaki siasa za maji taka , kama ni kweli sasa hao ndiyo wanaochochea udini ili kulinda maslahi ya watawala wa namna yao, ni upuuzi inngawa najua kwa maslahi ya kisiasa ya kundi fulani mipango kama hiyo ya kuhujumu kongamano la katiba haitafanikiwa , na washindwe na walegee.
 
Stupit this udinism, yani kla mara wanafikiri watanzania ni wapumbavu kiasi cha kuamini fulani anahujimiwa kisa ni wa dini fulani. Huu ni ujinga ambao watanzania lazima tuuepuku.

mbona kipindi cha mkapa mambo mengi ya kutisha yalikuwepo kama kuzama kwa MV Bukoba. Nahakika nao wangesema wamehujumiwa. wakati mambo mengine ni uongozi mbovu.

Enyi waislam wenzangu msikubali kununulika na kuanza propoganda chafu na mkashindwa kumkosoa mtu eti kisa ni dini yako. Kwenye serikali hatuangalii dini tunaangalia mtu safi asifiwe na mchafu akemewe.

Wakristo kwa waislam. Kemeeni uovu mkiuona hata kama mtu ni wa dini yako, na msifieni mtu pale anapostahili sio kutumiwa na wanasiasa kuleta pumba huku familia zenu zikibaki masikini.
 
Hawa wana lao jambo. Pengine wanataka Tanganyika igawanywe kuwa na Jamhuri mbili kama ambavyo inavyotokea Sudani hivi sasa.
 
uDINI UPO KWA WANASIASA BUT SISI MTAANI TUNAKULA BATA TUU!
 
Hawa wana lao jambo. Pengine wanataka Tanganyika igawanywe kuwa na Jamhuri mbili kama ambavyo inavyotokea Sudani hivi sasa.
hatuwez gawanya tanganyika kwa watu walio wachache-sudan znagawanywa mana north din moja ni weng,south dini nyingine ni wengi-sisi dini moja ndo wengi-so wao ndo watafute pa kwenda-ngoja tuone ni kitu gani au tamko gani watakuja nalo hio kesho
 
Asante kwa kunifanya nifungue akili zangu. Mchana pale Mwenge walikuwa na mahubiri marefu sana, sikuweka umakini wowote ila yalikuwa na mwelekeo wa siasa. Kumbe ni hivyo! TUNAANGAMIA NDUGU ZANGU! Kwa nini wanataka kuwapambanisha ndugu! Ndugu zangu ni waislamu sasa ni nini hii!!!!!! SITAKATA TAMAA, MAPAMBANO YANAENDELEA HATA WALETE UDINI WA SIASA KALI KULIKO ZA IRAN!
 
Hapa issue sio kuhujumu kongamano la UDASA bali ni kipimo kizuri cha kuonesha utofauti kati ya waislamu wenzangu ambao wamekua nyuma kudai katiba mpya na wasomi (malecturer wetu) kuhusu Future ya nchi yetu. Kesho ndo tutajua ni watu gani huwa wanakwamisha maendeleo ya nchi yetu. Hivyo ngoja tupate matokeo yake hiyo kesho.
 
katika hali ya kushitua na kushangaza,kesho wakati UDSM wakiwa wameamua kuwa na kongamano kubwa la kujadili uwepo wa katiba mpya,lipo kundi la watu ambao wanadai kuwa ni waislamu na wao wameamua kuitisha kongamano lao kesho ktk ukumbi wa karimjee na wanategemea kutoa matamko mbalimbali lengo ni kuhakikisha kuwa media itaondoa attention kwenye katiba. pia watatoa matamko controversial sana juu ya utawala kuwa JK na serikali yake inahujumiwa na wakristo. pindi tamko likikamilika litawekwa hapa jamvini kwani ndio draft ya kwanza imekuwa tayari. ukumbi wa karimjee umelipiwa na mnene mmoja serikalini. leo mahubiri kwenye misikiti kadhaa DSM yamekuwa yakionyesha kuwa kila mara anapokuwa rais muislam basi anawekewa vikwazo na hata kudhalilishwa na wametoa mifano mingi ya Mwinyi na sasa JK.More 2 come later

Watu wa Pwani bana, fitna! fitna! fitna! fitna!
 
Naomba waislamu msinielewe vibaya kwa maneno nitakayoandika hapa kwani ndivyo ninavyoamini mimi binafsi.
1. Binafsi naamini Waislamu kama watanzania wengine wana uchungu na uzalendo na nchi yao
2. Naamini waislamu kwa misingi na maamrisho ya dini yao, hawana nia ya kuvuruga amani wala kubagua watanzania wenzao kwa misingi ya dini
3. Naamini waisalmu wanapata haki kwa mgao sawa na wanavyopata wananchi wa dini zingine

Tatizo ninaloliona ndugu zangu ni kuwa kwa siku za karibuni (baada ya mchakato wa uchaguzi kuanza), waislamu wameanza kuchafuliwa kwa maksudi na watu wenye malengo ya kisiasa, kwa maslahi binafsi ya watu hao. Kwa bahati mbaya nahisi kuna udhaifu fulani katika system ya uislamu, inayosababisha wawe vulnerable na kurubuniwa kirahisi
1. Nahisi kuna ukosefu wa hirachy katika uongozi wa dini ya kiislamu. hapa namaanisha kuwa ni rahisi sana akajitokeza anayejiita shehe, Bakwata, au sijui nani akasema au kutenda kitu fulani kwa 'niaba' ya waislamu leo, na kesho akatokea mwangine, akawa kinyume nae, pia kwa niaba ya waislamu. Unaweza kuona mfano wa maandamano na mauji ya Arusha
2. Nina wasiwasi na nia ya BAADHI ya viongozi wa dini ya waislamu kuwa za kibinafsi zaidi
3. Nina wasiwasi na uaminifu wa BAADHI ya viongozi wa waislamu, kuwa na dalili ya kurubuniwa kirahisi na wanasiasa
4. Nina wasiwasi na elimu ya BAADHI ya viongozi wa waislamu, kwani pamoja na busara na uwezo wa asili juu ya masuala ya uongozi, lakini hatuwezi ku-underestimate umuhimu wa elimu katika uongozi

Kutokana na hayo, naona sasa kwa kuona kuwa wamezidiwa kila idara, CCM (au kikundi fulani ndani ya CCM), kimefanikiwa kuwarubuni baadhi ya viongozi wadhaifu wa waislamu, katika matukio tofauti, lakini katika mpango endelevu, na kuutumia uislamu kama ngao yao dhidi ya harakati za wanachi za kujikomboa kutoka katika udhalimu wa CCM

Nawaasa waislamu wote wenye nia njema kupinga na kulaani mpango huu wa kishetani wa CCM, wa kuwatumia kama ngao. Mtu yeyote ajue kuwa katika nchi ambayo hakuna dini yenye majority katika population representation, then hakuna chance kuwa move za udini na kidini zitakazowesha kundi lolote kupata maslahi yake, kinyume na matakwa ya walio wengi.

Waislamu wakumbuke kwamba, hata kama raisi atawapendelea katika nafasi za uteuzi, au mambo fulani madogo, hiyo naina maana ikilinganishwa na wanyanyaso wanayopata kama wananchi wengine katika nynja za kuichumi, afya, elimu n.k

Waislamu wakumbuke kuwa, kama wataamua kuisapoti serikali kwa kila kitu, eti kwa sababu raisi ni muislamu, ipo siku raisi huyom ataondoka madarakani, afafu wataona aibu kupinga mambo ambayo, ama leo wanayatetea, au yameanzishwa na raisi wa sasa.

Waislamu wakumbuke kuwa hakuna mtu yeyote mwenye akili timamu anayempinga Kikwete kwa eti ni muislamu, bali anapingwa kwa kuwa ni dhaifu kiuongozi na kiutawala.

CCM wakumbuke kuwa wanapandikiza mbegu ambayo muda sio mrefu itawaangamiza hata wao

Hali kadhalika CCM wajue pia kuwa hata kama wana taarifa zozote zi 'kiintelijensia' kuwa pengine wapo wakristo wanaompinga JK kwa udini au wenye hila za maslahi ya kidini, njia muafaka ya kukabiliana nao sio kuzidi kupandikiza udini, bali ni kuukemea

Naamini wanaokuza udini ndani ya CCM ni wale wanaohitaji maslahi ya muda mfupi bila kujali mustakabali wa ama CCM au Tanzania katika siku zijazo.
 
katika hali ya kushitua na kushangaza,kesho wakati UDSM wakiwa wameamua kuwa na kongamano kubwa la kujadili uwepo wa katiba mpya,lipo kundi la watu ambao wanadai kuwa ni waislamu na wao wameamua kuitisha kongamano lao kesho ktk ukumbi wa karimjee na wanategemea kutoa matamko mbalimbali lengo ni kuhakikisha kuwa media itaondoa attention kwenye katiba. pia watatoa matamko controversial sana juu ya utawala kuwa JK na serikali yake inahujumiwa na wakristo. pindi tamko likikamilika litawekwa hapa jamvini kwani ndio draft ya kwanza imekuwa tayari. ukumbi wa karimjee umelipiwa na mnene mmoja serikalini. leo mahubiri kwenye misikiti kadhaa DSM yamekuwa yakionyesha kuwa kila mara anapokuwa rais muislam basi anawekewa vikwazo na hata kudhalilishwa na wametoa mifano mingi ya Mwinyi na sasa JK.More 2 come later

ITV Wameahidi kurusha live toka saa nnne asubuhi. Wananchi wengi tutafuatilia kupitia ITV
 
katika hali ya kushitua na kushangaza,kesho wakati udsm wakiwa wameamua kuwa na kongamano kubwa la kujadili uwepo wa katiba mpya,lipo kundi la watu ambao wanadai kuwa ni waislamu na wao wameamua kuitisha kongamano lao kesho ktk ukumbi wa karimjee na wanategemea kutoa matamko mbalimbali lengo ni kuhakikisha kuwa media itaondoa attention kwenye katiba. Pia watatoa matamko controversial sana juu ya utawala kuwa jk na serikali yake inahujumiwa na wakristo. Pindi tamko likikamilika litawekwa hapa jamvini kwani ndio draft ya kwanza imekuwa tayari. Ukumbi wa karimjee umelipiwa na mnene mmoja serikalini. Leo mahubiri kwenye misikiti kadhaa dsm yamekuwa yakionyesha kuwa kila mara anapokuwa rais muislam basi anawekewa vikwazo na hata kudhalilishwa na wametoa mifano mingi ya mwinyi na sasa jk.more 2 come later

hata mlete udini ,ukabila na urangi wa ngozi sisi wapiganaji hatujali!!!. Tutapigania nchi yetu mpaka mwisho wa nyakati.
 
Waislam hawana uongozi,kila msikiti na maamuzi yake!ni jamii isiyokua na muelekeo ktk tanzania.Rais atakayevunja bakwata na kuunda chombo chenye tija kwa waislam wote ndiye atakaye kuwa na manufaa kwa waislam
 
Back
Top Bottom