Prof. Shivji: Ukweli unapatikana kwenye mijadala. Kugusia ya kaduma- Je ilingewezekana kwa mtu mwenye kiwanda kujiunga na tanu kwakuwa anaamini ktk ujamaa? Wangapi tunawafundisha watoto wetu wasiwe mabepari. Kuhusiana na mbita: Tulisema wazi kwamba hatuwezi kununulika,je kweli leo hatuwezi kununulika? Kujiunga na chama kwa ahadi ya cheo sio kununulika? Kuwa na msimamo ni muhimu sana.
Vijana someni historia ya nchi yetu na chambueni AA. Historia ya nchi yetu kisiasa haijaandikwa vzuri. Hatujafanya uchambuzi kutathmini athari za kuachana na azimio la arusha. Vijana tu-question everything, hata nyerere hatukuwa tunamkubalia kila kitu. Hata wakulima wanataka tufanye utafiti ili waweze kujua mazingira yao. AA haikubadilishwa kwa ajili ya watu wadogo (azimio la ZNZ), bali lilihalalishwa kwa kutumia watu wadogo. Wewekezaji hawaji kuwapa ajira watu wadogo.