Kongamano la Azimio la Arusha

Fideli rafael toka DUCE:anauliza ikitokea wote walioko ukumbini wanaambiwa wataajiriwa kwa mshahara mmoja watakubali?....hoja yake ni kuwa tofauti ya vipato baina ya watu haiwezi leta umoja
 
MY Take: bado vijana wanahitaji kuwekwa vizuri kwenye eneo la kuchambua mada, naona wanatoka nje ya maswali muhimu ya mtoa mada Shivji, naona wazee wameweza kutoa hoja nzuri sana na uwezo mkubwa bado wa kujenga hoja kuliko vijana wa sasa
 
JOSEPH BUTIKU:chuo kikuu kifanya etafiti wa tulikotoka, tulipo na tunakokwenda...ni muhimu kufanya hivyo sbb tunayo historia.
 
Mzee BUTIKU: mambo 2. Kwanza kumshukuru Prof. Shivji, kwa utafiti na ufasaha katika kupambanua mambo mengi. anashauri chuo kikuu kama mzee wajitahidi kufanya utafiti wa tulikotoka na tunako taka kwenda. Chombo cha kusaidia kazi hiyo ni chuo kikuu cha Dsm na vyuo vingine, ni muhimu kufanya hivyo kwasbb tunayo historia kwasbab hatuwezi kuwa na miaka 50 ya uhuru mkawa mpoa na hampo
2. Katika AA yapo mambo ya msingi, msingi mmoja ameusema prof napenda kuusisitiza. Msingi wa kwanza, AA linahusu SISI, humu na wengine nje ya Taifa, maana yale tunayofanya humu ndani ndio yanakuwa msingi wa mahusuiano yetu na watu wengine nje ya Taifa.
 
MY Take: bado vijana wanahitaji kuwekwa vizuri kwenye eneo la kuchambua mada, naona wanatoka nje ya maswali muhimu ya mtoa mada Shivji, naona wazee wameweza kutoa hoja nzuri sana na uwezo mkubwa bado wa kujenga hoja kuliko vijana wa sasa


Mkuu utu uzima dawa, hawa wazee wanashusha nondo za uhakika
 
BUTIKU: Utu nido msingi w akila kitu, na lazima tulikubali hilo, maana tusipokubali hilo hatuwezi kuzungumzia usawa: values zetu kama watu, wapare, wahindi, na wapare na wagogo tunashiriki nini katika taifa letu, value zetu zinazotuunganisha ni zipi? Mwisho, Hakuna Azimio la Zanzibar, kulikuwa na kikao cha kawaida cha Halamshauri kuu ya chama ya Taifa.
 
Wazee walio kuwa ndani ya chama wakaanza kuwa omba omba kutoka kwa vijana waliokuwa na pesa. wakaona haifai wakasema tutaendeleaje kuwa viongozi huku tunaomba omba, wakasema tulegeze masharti wapangishe tujumba. Sasa viongozi wa leo wameongeza zaidi ni pamoja kuomba pesa za mafisadi,
 
BUTIKU: hakuna Azimio la zanzibar, kulikuwa na kikao cha NEC ya CCM bila kumwambia Mwalimu...viongozi walianza kuwa omba omba ndio maana wakaruhusu kulegeza masharti ili waruhusiwe kupangisha nyumba zao wapate hela..baada ya kubadili kanuni ndipo sasa wenye tamaa walipo badili kweli kweli
 
huwezi kuondoa umimi, lakini unaweza kuusupress, AA lilikuwa lisaidie kusupress Umimi.
 
Mzee Butiku anaeleza kuwa hakuna Azimio la Zanzibar kwani Azimio hilo halikuwa na MIIKO
 
Butiku: dunia ya leo huwezi kufanya mabo wewe mwenyewe lazima utahitaji external aid...je wasomi wamejiandaaje kukubali hiyo misaada na wakatti huo huo kuweka msimamo kwenye masharti yake?
 
Nnape Moses Nauye: watu waliozungumza ktk mjadala wa karimjee walitaka AA liwe reference ya kuandika katiba Mpya. AA ni jambo la msingi sana kwa utaifa na historia yetu. Fursa ya kutengeneza katiba mpya ni fursa ya kurudisha AA, na fursa ya kulijenga taifa letu kutoka hapa na kwenda kule tunataka kwenda.
 
NAPE MNAUYE: azimio la Arusha ni moja kati ya mambo muhimu kwenye historia ya nchi yetu...tukiitumia vizuri fursa hii ya kuandaa katiba mpya tutapata nafasi ya kurejesha misingi ya nchi yetu...tufunge mikanda tupambane turudishe misingi
 
Nauye: Kurudisha AA ni mapambano vijana wafunge mikanda waingia katika mapambano.
 
MY Take: bado vijana wanahitaji kuwekwa vizuri kwenye eneo la kuchambua mada, naona wanatoka nje ya maswali muhimu ya mtoa mada Shivji, naona wazee wameweza kutoa hoja nzuri sana na uwezo mkubwa bado wa kujenga hoja kuliko vijana wa sasa

Ni kweli ndugu uzoefu na historia vinasema hata wasipokuwa viongozi,wazee toka enzi walitumika kama washauri.
 
NAPE: tukirudi kwenye misingi taifa letu litaenda kule linakopaswa kuelekea
 
Back
Top Bottom