Kongamano kuuubwa kesho tar 30 mjini tabora. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kongamano kuuubwa kesho tar 30 mjini tabora.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kivia, Jan 29, 2011.

 1. K

  Kivia JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kesho kutakuwa na kongamano kubwa hapa Tabora la kutafakari kauli za maaskofu na siasa ya tz kwa ujumla. Viongozi wa dini na wageni mbali* watakuwepo. Pia kongamano litakuwa LIVE KUPITIA RADIO IMAAN. Kuanzia saa tatu asubuhi. Usikose.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  yale yale.sbadala ya kujadili umaskini wa tanzania na kushuka kwa elimu nyie mwajadili kauli za maaskofu na siasa zitawanufaisha nini watoto wenu???
   
 3. I

  Ipole JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 296
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana nawe hilo kongamano ni vema likafanyika ili kujibu hoja za hao maaskofu suala la kujadili maendeleo ya wanafunzi litajadilwa baada ya kuwajibu maaskofu.
   
 4. Ngalikivembu

  Ngalikivembu JF-Expert Member

  #4
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,908
  Likes Received: 355
  Trophy Points: 180
  Lina umaana.mlio karibu jaribuni kuhudhuria.
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 29, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  kwa hiyo ni kongamano la waislam tu?
   
 6. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #6
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Fikra mbofumbofu, kauli ya maaskofu na siasa tatizo lenu ni akili na fikra finyu ktk kupambanua mambo ya maendeleo na dini, havitengani kamwe.
  mbona wakati maaskofu walikuwa wanasema kuisifia serikali na wakati mwingine kama askofu Kilaini anasema Kikwete ni safi, 'chaguo la Mungu' mbona hamkuona kama kajichanganya ktk siasa? maana vyama vingine havikuafiki na havikukimbilia ktk hisia za kuchanganya dini na siasa. ila nyie ndo mnaona kwa sababu tu maaskofu hao hao wameikosoa serikali hiyo hiyo waloisifia awali, ila nyie kwa kuwa hamtaki kuongozwa kwa ukweli mmebaki ktk fikra dhoofu za kidini.
  kongamano halina maana na ni muflis lisilo na ufanisi.
   
 7. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh wakati wengine tunalilia ufisadi na uwajibikaji wa serikali, wengine wanaleta mifarakano kwa kuingiza udini. tuna safari ndefu kufikia uhuru wa kweli.
  Uzuri ugumu maisha unatupiga vibaya bila kuangalia udini.
   
 8. M

  MMASSY JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Upuuzi,huwezi kaa na kujadili kauli huku kuna mambo nyeti ya kujadili.nendeni arusha mkafanyie huko muisome namna
   
 9. M

  Mtu Mmoja JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2011
  Joined: Mar 18, 2010
  Messages: 596
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  hebu kuweni serious kidogo jamani, shida zote hizi, bei a umeme, katiba mpya, dowans/richmond, matokeo ya form IV, mauaji ya raia, ujambazi nk nk, kweli kauli ya maaskofu ndo mmeona dili la kupotezea watu muda wao? but ni uhuru wa maoni unaoindwa na katiba, nendeni tu mkajadili ial sidhani kama wenye akili watahudhuria. tegemeeni waliwao watupu.
   
 10. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hapo penye nyekundu ndio patakapowatia adabu... ref: matokeo ya form IV
   
 11. Mpui Lyazumbi

  Mpui Lyazumbi JF-Expert Member

  #11
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 1,853
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Jadilini matokeo ya kidato cha nne kwa shule za kiislam au zinazomilikiwa na waislam. Fanyeni hima maana ni aibu jamani.
   
 12. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #12
  Jan 30, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :msela:chapa mguu twende km kawaida yao kongamano la ma**********:bump:
   
 13. m

  maguga Member

  #13
  Jan 30, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii radio Imani na wanao ituma hawatutakii mema kabisaa!!!tuwatafute tuwajue..watueleze nia yao waziwazi!!!!!
   
 14. N

  Ndevu mbili JF-Expert Member

  #14
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 382
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hivi waliopo huko hawawezi kutuwekea picha kwenye Utube?
  Jamaa yangu nimempigia simu akanisikilizisha muhtasari.
  Allah blessing you!
   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hao ndiyo Wanyamwezi jamani. Tena usishangae, Mzee wa Acudo aka Pekecapekecha aka Prof. Kapuya, ndiye kawadhamini hizo hela za mkutano. Yaani Tabora bado tupo karne ya .............teteteeee naogopa kusema.

  Naombeni msituhukumu wote maana hilo litakuwa genge la watu wachache sana na sidhani hata mji mzima utasikia juu ya hilo. Tabora ni moja ya miji ambayo imechoka sana na ukiwapa hela kidogo, watakuja. Ukiwapa kishughuli kidogo, watakuja ili muradi wakirudi makwao, wakatambe kwa wake zao na nyumba ndogo kuwa "leo wamechoka sana maana walikuwa KAZINI.................." Kesho akiamka, hana kazi na anaanza kupga tu miayo.

  Kwao wao, ni heri kwenye Kongamano ataambulia walau chai na maandazi. Inasikitisha ila ndiyo ukweli wenyewe.

  Muwapuuze tu hao wajinga wachache kwani hawawakilishi TABORA NZIMA.

  Msitegemee MSOMI yeyote aliyemaliza form 6 kwenda juu aende hapo. Labda kama kwenye hilo Kongamano, kuna ULAJI wa nguvu atapata. Hapo kweli ataenda kuchukua hela za bure za akina CCM.

  CCM wanazidi kupoteza hela chache walizonazo kuzima moto wa PIPO PAWAA badala ya kuzitumia kwa mambo ya maana. Mkoa wa Tabora si ndiyo walimkimbia Jukwaani Kikwete? Sema kuwa Tabora ni moja ya mikoa rahisi sana kuchakachua kutokana na umasikini na woga wa Wanyamwezi. Kumbukeni maneno ya Prof. Baregu kuwa "Mtaji wa CCM ni Umasikini wa Watanzania/Wanyamwezi/Tabora/Sikonge....."

  Mfano mzuri ni mie hapa ambaye huwa NAPINGANA na ufisadi waziwazi bila kujali unafanywa na chama gani. Tutabanana nao hadi kieleweke. Nategemea CHADEMA wataanza kampeni zao kwenye mikoa masikini sana kama Tabora, Singida, Mtwara, Lindi na Tanga maana ndiyo mikoa pekee ambayo CCM wana nguvu sana. Na huko, Watanzania wamelala kwa kweli, lohhh.

  Kwa Sikonge wanasema kabisa, hata awekwe NYANI kama mgombea wa CCM, basi atashinda.
   
 16. Keren_Happuch

  Keren_Happuch JF-Expert Member

  #16
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 1,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Jamani mimi naomba kueleweshwa tu kidogo, kwani maaskofu walisema nini? Labda itanisaidia kujua kwanini ndugu zetu kimewauma sana???
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jan 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Siyo MUHIMU walisema nini......... Cha muhimu ni kuwa CCM wanaona waendelee kutumia Waislaam katika kushikilia kuendelea kutawala Tanzania. Jana nimeongea na ndugu yangu anayeishi Tabata na akasema WANA SIKU 5 HAKUNA UMEME. Sasa unategemea watu watajali DINI badala ya matatizo waliyo nayo?

  Kwa wanaofikiri kwa mkoa kama Tabora ni SHIDA itawafanya wabadilike, basi mnakosea. Mkoa wa Tabora unaishi kwa formula zake. Tabora mjini ni kama KIJIJINI ila sema watu wanaishi mjini. Watu wengi pale ni WAKULIMA. Kama kuna wafanyakazi ni wachache sana sana na wengi watakuwa Waalimu, Polisi, Jeshi. Wanaobaki ni Wanafunzi, wafanya biashara na kundi kubwa sana wakiishi kwa kutegemea kilimo. Hata wafanyakazi, wengi wanakuwa na mashamba yao nje ya mji ingawa wizi ni mkubwa sana.

  Sasa hawa watu, kuwe na mshahara, kusiwe na mshahara, wamejiweka katika hali kuwa "wasiitegemee sana serikali......." Kwa wale wazee au wanajifanya wamekuwa wazee kwa sababu ni WAVIVU wa kutupwa, hushinda kutwa wakitafuta kisababu chochote cha kusema NINI KAFANYA SIKU HIYO........

  Ndiyo maana sishangai kuwa MAKONGAMANO kama haya yapelekwe Tabora maana Dar es salaam wangelitolewa Baru. Wee mtu hajaoga, hajala na unamletea eti kongamano? Nenda Arusha huko kama hawajakutoa ngeu.

  MTAJI WA CCM NI UMASIKINI WA WATANZANIA .....Prof. Baregu.
   
 18. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #18
  Jan 30, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @sikonge nakubaliana na weye kua shida haiwafanyi watu wa tabora kubadilika. Lkn ujue tu kua hayo si kwa tabora tu bali ni karibu tanganyika nzima hayo ndio maisha yao. Kwani mtwana ajua shida?
   
Loading...