Hao ndiyo Wanyamwezi jamani. Tena usishangae, Mzee wa Acudo aka Pekecapekecha aka Prof. Kapuya, ndiye kawadhamini hizo hela za mkutano. Yaani Tabora bado tupo karne ya .............teteteeee naogopa kusema.
Naombeni msituhukumu wote maana hilo litakuwa genge la watu wachache sana na sidhani hata mji mzima utasikia juu ya hilo. Tabora ni moja ya miji ambayo imechoka sana na ukiwapa hela kidogo, watakuja. Ukiwapa kishughuli kidogo, watakuja ili muradi wakirudi makwao, wakatambe kwa wake zao na nyumba ndogo kuwa "leo wamechoka sana maana walikuwa KAZINI.................." Kesho akiamka, hana kazi na anaanza kupga tu miayo.
Kwao wao, ni heri kwenye Kongamano ataambulia walau chai na maandazi. Inasikitisha ila ndiyo ukweli wenyewe.
Muwapuuze tu hao wajinga wachache kwani hawawakilishi TABORA NZIMA.
Msitegemee MSOMI yeyote aliyemaliza form 6 kwenda juu aende hapo. Labda kama kwenye hilo Kongamano, kuna ULAJI wa nguvu atapata. Hapo kweli ataenda kuchukua hela za bure za akina CCM.
CCM wanazidi kupoteza hela chache walizonazo kuzima moto wa PIPO PAWAA badala ya kuzitumia kwa mambo ya maana. Mkoa wa Tabora si ndiyo walimkimbia Jukwaani Kikwete? Sema kuwa Tabora ni moja ya mikoa rahisi sana kuchakachua kutokana na umasikini na woga wa Wanyamwezi. Kumbukeni maneno ya Prof. Baregu kuwa "Mtaji wa CCM ni Umasikini wa Watanzania/Wanyamwezi/Tabora/Sikonge....."
Mfano mzuri ni mie hapa ambaye huwa NAPINGANA na ufisadi waziwazi bila kujali unafanywa na chama gani. Tutabanana nao hadi kieleweke. Nategemea CHADEMA wataanza kampeni zao kwenye mikoa masikini sana kama Tabora, Singida, Mtwara, Lindi na Tanga maana ndiyo mikoa pekee ambayo CCM wana nguvu sana. Na huko, Watanzania wamelala kwa kweli, lohhh.
Kwa Sikonge wanasema kabisa, hata awekwe NYANI kama mgombea wa CCM, basi atashinda.