Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 9,824
- 13,194
Kuanzia sare zao za kazi yaani, shati na suruali. kwanza ni vichafu, lakini pia ni vichakavu na sielewagi vinachakaaga kwa kazi gani au kuvaliwa wapi zaidi ya humo humo kwenye daladala 🐒
Sawa, kazi ni kazi ilia angalau wawe wanaoga, wawe wanasafisha midomo, walau kunyoa ndevu na kua nadhifu kiasi...
Mfano unakuta konda kavaa sare juu ya t-shirt yake, anavuja jasho, mdomoni ameng'ata kalamu, mdomo unatema harufu nzito, halafu anakusanya nauli, abiria mmebanana nae anataka kupenya humohumo mlipobanana dah, na wewe umeulamba kweli, umechomekea zako shati jeupe unaelekea town 🐒
Huu mtindo au fashion yao inakera, inaudhi na kwakweli inatia kichefuchefu na ni aibu inayotia doa unadhifu wa waTanzania
Hivi hali ile ya makondakta na madereva wa daladala inachochewa na nini hasa?🐒