Konda wa daladala na dereva

Zumbukuku

Member
Joined
May 17, 2011
Messages
70
Points
0

Zumbukuku

Member
Joined May 17, 2011
70 0
Konda wa daladala na dereva wake walikuwa wanakula vichwa hadi wanachanyikiwa kiasi wakaapizana kuwa kama huko kwa Mungu kutakuwa na kula vichwa kama wanavyokula sasa basi itakuwa peponi. Basi wakakubaliana kuwa yeyote mmoja wao akifa aende kuona hali ya kula vichwa huko kwa Mungu halafu afanye kila njia arudi amtaharifu mwenzake aliyebaki.

Basi ghafla dereva akafa. Sasa baada ya mazishi kupita siku moja wakati Konda amelala akaona mtu anamshika kidole cha mguuni..kuangalia kumbe dereva.

Akamuuliza, vipi hali ya vichwa na madaladala huko mbinguni,dereva akamwambia anazo habari mbili yaani moja nzuri na nyingine mbaya. Basi akamwambia konda habari nzuri ni kuwa huko mbinguni kuna kula vichwa si mchezo kwani yeye ameenda ahera na hakuna madaladala mengi,yaani wanapanga bei wenyewe. Habari mbaya ni kuwa amemchagua yeye kuwa konda wake!
 

Forum statistics

Threads 1,390,637
Members 528,220
Posts 34,057,222
Top