Kompyuta za IGP, Mkemia Mkuu zaibwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kompyuta za IGP, Mkemia Mkuu zaibwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Selous, May 10, 2009.

 1. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2009
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Jamani hebu nisaidie hili suala kama lilivyo mana nashindwa kuelewa content kama lina mahusiano na ufisadi na if we real serious.


  WAKATI kesi ya watuhumiwa 11, walioiba kompyuta katika ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), ikiendelea imebainika Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Said Mwema, naye ameibiwa kompyuta ndogo (Laptop).

  Wiki mbili baada ya tukio la wizi wa kompyuta za IGP Mwema, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, nayo iliibiwa kompyuta ya mezani ambayo inasadikika ilikuwa na kumbukumbu nyingi ambazo hazijabainishwa zinahusiana na mambo gani.

  Uchunguzi uliofanywa na Tanzania Daima Jumapili, kwa wiki kadhaa sasa umebaini kuwa kumekuwapo kwa wasiwasi mkubwa wa kuibwa kwa nyaraka na vifaa mbalimbali katika ofisi za viongozi wakubwa wa serikali akiwemo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG).

  Chanzo kimoja kimelidokeza Tanzania Daima Jumapili, uchunguzi wa wizi wa kompyuta hizo mpaka sasa unaendelea ili kuwabaini wahalifu waliotenda tukio hilo na kujua walikuwa na lengo gani.

  Chanzo hicho kimebainisha kuwa kikosi maalum kimeundwa kufuatilia wizi huo ambao umeonekana kuanza kushamiri katika ofisi nyeti za serikali hasa katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na tuhuma nyingi za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka yanayofanywa na viongozi.

  Taarifa za ndani zinadai kuwa kompyuta ya IGP iliibwa mezani kwake majira ya mchana siku ya Ijumaa wakati mkuu huyo akiwa amekwenda msikitini kuswali.

  Katika meza hiyo kulikuwapo na simu za mkononi na kiasi cha fedha kinachodaiwa kuwa sh milioni saba, lakini ni kompyuta pekee ndiyo iliyoibwa.

  Habari zaidi zinabainisha kuwa IGP aliporudi alishangaa kutoikuta kompyuta hiyo ilhali simu na fedha vilikuwapo kama alivyoviacha, baada ya kubaini wizi huo zilichukuliwa alama maalumu za vidole zikaonekana ni za mlinzi wake wa karibu (Board guard), ambaye inadaiwa huwa na kawaida ya kuingia mara kwa mara katika ofisi pasi na kutiliwa shaka.

  Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa uchunguzi ulipofanyika ndani ya jeshi la polisi ilibainika kuwa kuna afisa wa jeshi hilo, mwenye cheo cha mkaguzi, ndiye aliyeichukua kompyuta hiyo, ambaye hadi sasa anahojiwa ili kulisaidia jeshi hilo liweze kupata chanzo cha uhalifu huo.

  Aidha, taarifa zinasema kuwa aliyeichukua kompyuta hiyo, inadaiwa, amelipwa sh mil. 10 kama ujira wake kwa kazi hiyo.

  Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI), Robert Manumba, alipoulizwa juu ya hatua ambazo jeshi hilo linazichukua dhidi ya wizi huo ambao unaonekana wazi kulenga kuiba nyaraka muhimu za serikali, alisema huo ni wizi kama mwingine kwani wezi hao hawakulenga kuiba kompyuta hizo kwa lengo maalumu.

  “ Siyo kwamba wizi haufanyiki, unafanyika sana; mara hii umetokea katika ofisi nyeti inayomhusisha mkuu wa jeshi la polisi, wizi huo umefanyika tu kama unavyoweza kufanyika nyumbani kwako, haukulenga ofisi hizi tu,” alisema DCI Manumba.

  Pamoja na kusema hivyo, alilithibitishia Tanzania Daima Jumapili kuwa hatua za uchunguzi zinaendelea ili kuwabaini wahalifu hao ambao wamefikia hatua mbaya.

  “Tanzania hatuna wizi wa kulenga ofisi maalumu za serikali, ndiyo maana unapotokea unawashangaza watu wengi lakini tumejipanga vilivyo katika uchunguzi kuhakikisha tunawakamata wale wote waliohusika,” alisema Manumba na kuongeza:

  “Nakwambia ukweli, wewe umekuja kuniuliza kwa sababu wizi umetokea katika ofisi hii, lakini matukio kama haya yanatokea pia katika nyumba za watu binafsi, hata siwezi kukuhesabia idadi ya kesi hizo, tusiwashtue watu waamini kuwa ulilengwa kwa kazi hiyo.”

  Manumba alizidi kusisitiza kuwa wizi upo dunia nzima na wanaweza kuiba mahali popote kama wataona kuna kitu, lakini hakuna wizi uliopangwa kulenga katika ofisi hizo za IGP, DPP , au kwa Mkemia Mkuu wa Serikali.
  Taarifa zimeeleza kuwa kompyuta iliyoibwa katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilikuwa kubwa ya mezani (PC), ambayo ilichukuliwa kupitia dirishani katika mazingira ya kutatanisha wakati milango ikiwa imefungwa.

  Chanzo chetu kutoka ndani ya ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, kimeeleza kuwa kompyuta hiyo ilikuwa ikitumika ndani ya ofisi ya Mkemia Mkuu, ambapo bado haijajulikana na nyaraka gani muhimu zilikuwa zimehifadhiwa humo.

  “Ni kweli kompyuta iliibwa hapa, milango imefungwa tumefika tukaelezwa kuwa kompyuta ya msaidizi wa bosi wetu haionekani wakati milango ilikuwa imefungwa,” alisema mmoja wa watumishi wa ofisi hiyo ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

  Aidha kuhusu tukio hilo lililotokea katika ofisi hizo zilizoko karibu na Taasisi ya Saratani, Ocean Road, imeelezwa kuwa bado uchunguzi unaendelea ili kubaini mtu aliyehusika kuiba kompyuta hiyo kama ni mmoja wa wafanyakazi au la.

  Kutokea kwa wizi huo kunawafanya baadhi ya watu kuwa na wasiwasi kuwa kuna njama zimepangwa na baadhi ya watu kupoteza vielelezo au ushahidi wa tuhuma au kesi mbalimbali zinazowakabili.

  Wasiwasi huo umechangiwa zaidi na matukio ya hivi karibuni ya kupandishwa mahakamani kwa baadhi ya vigogo wa serikali, wafanyabiashara na watu binafsi kwa wizi au matumizi mabaya ya madaraka. Mpaka sasa watu 11 wameshapandishwa katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kujibu tuhuma za kuiba kompyuta katika ofisi ya Mkurugeni wa Mashtaka Nchini (DPP).


  Source: Tanzania Daima
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  May 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  Miye hata kuwaambia mambo mengine sina hamu.. kuna sehemu ya stori hiyo haijaandikwa. Kwa sababu tunataka kuangalia kwa vipande vipande.. .. we have to look for patterns.. nje ya hapo tutashangaa tu..
   
 3. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  1. Hata hivyo napongeza kama huko jeshi la polisi na mkemia mkuu angalau wanatumia laptop.

  2. Inasikitisha kwamba kama taasisi kama ya polisi hawezi kulinda usalama wa data zao... technologia zipo ambapo data haziwezi kuwa na faida kwa yeyote anapoiba... isipokuwa itabidi tu a format na kutumia hiyo computer kwa matumizi mengi.
   
 4. G

  Giroy Member

  #4
  May 10, 2009
  Joined: Dec 17, 2008
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda wanataka kuharibu ushahidi fulani,lakini pia ni kasha kwa jeshi la polisi,kama siyo dili kuna watu lazima wapoteze kazi.tuache longo longo jamani.
   
 5. M

  Mulugwanza Member

  #5
  May 10, 2009
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Mbona majibu ya Manumba ni ya jumla jumla sana, hivi DCI ni cheo cha kisiasa au ni profesional job? naona umefika sasa wakati wa watu kutumia akili kidogo! Manumba anadhani kuwa watanzania ni wajinga kiasi hiki? Majibu yake hayaendani na kilichotokea, hata kijana wangu mwenye umri ya miaka 5 asingeweza kujibu upuuzi kama huu!
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  May 10, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,394
  Trophy Points: 280
  grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
   
 7. F

  Future-Tanzania JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2009
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mkuu tupe data tuchambue, kuna kitu akisound right! kweli kibaka aache hela na simu aibe computer!!!!!!!!!!! mhhhhhh!!!!!!
   
 8. Sura-ya-Kwanza

  Sura-ya-Kwanza JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2009
  Joined: Nov 17, 2007
  Messages: 561
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Afadhali hivyo ni vitendea kazi...Rasilimali je?
   
 9. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,625
  Likes Received: 2,003
  Trophy Points: 280
  Mwema alidai kuwa licha ya ushahidi alio nao,hawezi kuwakamata mafisadi kwasababu wanaweza kuiyumbisha nchi...Sasa kama kuna mtu ameamua kuyumba na hao mafisadi,ni wazi kuna fukuto humo serikalini na kwenye institutions zote zenye siri za mafisadi hao...kama vile mkemia mkuu,IGP na takukuru.
  Amenimaliza jamaa aliyekwiba computer kwa malipo ya milioni 10 na wakati huo huo akiacha milioni 7 kwene deski...Upungunguwani utatumaliza kwani sijui ni njaa ama ukosefu wa akili.
  Mafisadi wameshagundua kuwa mwavuli wanaojikinga nao ushatoboka matundu kibao na hivyo hakuna mantiki kuendelea kujikinga na mvua,sana sana wanachotakiwa ni kuizuia mvua hivyo kama wana uwezo huo....Mfisadi wamegunduwa kuwa hakuna mshikamano tena baina yao kwa kuitumia serikali,tayari kuna matundu na kwasababu serikali nayo inaonekana kutaka kujivua lawama,then ni wazi kuwa extreme measures kama vile kuiba ushahidi zinaweza kuwa applied na mafisadi hao kwasababu nasikia kuwa hata siri za kashfa za baadhi ya watu zinatafutwa,nadhani ni trend hiyo hiyo....Masikini wabongo,tunatumiwa na kuyumbishwa kama wendawazimu,inasikitisha.
  Cha muhimu kuna joto,joto ambalo limeleta pressure kubwa na kupuuzia tena si rahisi,nadhani ni either mwisho wa mafisadi umekaribia,ama anguko la wazalendo,inategemeana na karata za wazalendo,maana cha muhimu wazalendo waelewe ni kuwa there is NO EASY TASK.
   
 10. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  haya majibu kama hayafai kutoka kwa mtu mwenye dhamana kama DCI......

  alafu hao wakuu hawana backup data zao?
   
 11. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Duh hii noma, nakumbuka hata mwaka jana tuliambiwa hapa kuwa muungwana nae aliibiwa laptop...........!
   
 12. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2009
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Hapa kuna Mchezo mchafu unaendelea......tutakuja kuambiwa Vielelezo na ushahidi muhimu wa kesi vimepotea kwenye zile Komputa zilizoibiwa............SISI SI WADANGANYIKA?
   
 13. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,844
  Likes Received: 1,110
  Trophy Points: 280
  Huyu DCI si mzima huyu, yaani zimeibwa laptops za Rais, DPP, IGP na Desk top ya Mkemia Mkuu, halafu yeye anadai ni wizi wa kawaida? Kweli Taifa limetekwa na Mafia group wala hayupo wa kuliponya. very sad. TISS wako wapi?
   
 14. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0


  Tena aziache Mil. 7 achukue Laptop ya 1.5 Mil !!!!!!!!??? logically No, kwa kutumia akili kidogo sana, yaani huhitaji hata kusoma ngumbalo , Kuna mchezo mchafu wa mafisadi
   
 15. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hapa kuna jambo linataka kufichwa, haiwezekani haka kamchezo kakawa kanaendelea hawa jamaa wako kimya namna hii!! Wanataka kuharibu ushahidi wa mambo mengi ikiwa na ufisadi pia. Yetu macho...
   
 16. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2009
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Mmmmmm bhagosha,

  Hii ni kali ya mwaka na yasikitisha sana wizi wa kwenda kuiba ktk nyanja muhimu sana nadani nchi hii duuuh ni masikitiko yalio kithiri ningependa kuongea haya kwanza kwa kuuliza,

  1: Surveillance Camera matumizi yake ni nini katika maoffice? na je zipo kweli ktk office nyeti kama TAKUKURU,IGP,DDP,MKEMIA MKUU WA SERIKARI,DCI,USALAMA WA TAIFA,MWANA SHERIA MKUU WA SERIKALI? Jamani kweli kweli inafikia tunakuwa na mzaha mpaka mtu anaweza ingia office nyeti na kuiba information muhimu? alafu ati zisha pita week 2 na ati uchunguzi unaendelea, hapo ndipo ni mehoji umuhimu wa camera maoficen kwa ujumla Department ya police yapaswa kuwa na very advance and current securty system iwe ya camera, data storage na vinginevyo unless hapa pataendelea kuwa na mchezo huu wakusema bado uchunguzi waendelea. Na hii sio tu kwa police bali idara zote nyeti hapa nchi zatakiwa kuwa na advanced securty system za aina nyingi tu ili kuhifadhi nyaraka.

  2:Crime Scene Equipments.
  kuna haja ya kuwa na ufahamu wa mambo kadhaa hapa mfn pakitokea matukio hayo ya wizi huwa call yao ya kwanza ni ipi ktk kufanya emergecny investigation?, Tumeambiwa ati walichukua Finger Print tuuu? jamani twahitaji kitu kama hichi [FONT=&quot]"AFIS & APIS - Automated Fingerprint & Palmprint Identification Systems"[/FONT][FONT=&quot][/FONT] je Jeshi letu la police linavyo ivyo vifaaa hapa ndipo narudi kwenye hoja yangu, Do realy have Crime Scene Labaratory?? me naona idara ya police wamepungukiwa na vitendea kazi vingi na wana mambo mengi sana ya kuyakabiri ktk utendaji wao wa kazi na ndivyo ivyo hukwamisha shughuri zote za kiuchunguzi ktk ufuatiliaji wa kesi. kwanza police wao walitakiwa wawe na central database system yao kubwa tu ya kutosha sasa hapo wao ndio wanatakiwa wajipange ni vipi waitumie kuboresha utendaji kazi zao.

  3. KIMEUNDWA KIKOSI MAALUMU KWA UCHUNGUZI HUO
  Ivi wandugu ni kila siku huwa tuna kuwa ni watu wa kuunda tumeeee tumeee, kikosi maaaluummm weeeee mpaka lini jamani hii nchi m'isha ifanya kama kichwa cha wenda wazimu kwanini kila mnapo wapeleka watu huko USA,UK, Israel kujifunza mbinu nyingi za kijeshi huwa hamuji na kuzi implement??? kulipsaw unda vikosi maaalum kwa ajiri ya matukio mengi yajayo na sio kusubili ati patokee tukio ndio kuundwe kitu fulani ndichio kifuatilie, kweli tumekuwa mbumbu kiasi gani kutofikilia mambo ya nyakati tulizo toka na tulizopo na tunako kwenda?kwa nini hatujiandai mapema na haya mambo, hapo ndipo kweli sector zote za nchi hii zinapungukiwa na hicho kitu kufanya mambo pindi gharika rimetukuta wala hatuna cha tahadhali ati, ndio maana kila kukicha matukio yasiyo epukika wa tibika na ufisadi unapitia humo humo viongozi wanashinda panaga mikakati ya kukwamisha au kufanya system nzima kuonekana ni ngumu kiutendaji na kiuwajibikaji. wenzetu USA unakuta wana NYPD,FBI,CIA,Home Land Security,DOJ na kadhalika hapa kwetu huliza kama ivyo vyombo husika tunavyo??


  mimi nasema huo ni uzembe mkubwa na wawajibishwe wote wanao acha nyaraka za serikali ovyo na kutozilinda nafikili mtu anapoingia office na kuna security policies ambazo hutakiwa fuatwa na mtu hu sign pale mfano uwe unafanya kazi Ernst & Young au kampuni ambazo ziko very stricted huwezi acha laptop hata kwa ndugu yako ovyo ovyo tu au labaratory waicha wazi na mtu anaingi huko bir security pass code au mtu anakwenda server room bila kupita security na ati hana security code ya mlangoni this is ridicules jamani.
   
 17. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  IGP alikuwa na milion 7!!!!! Yeye ni CASHIER??? How comes that anakuwa na cash yote phyically on his desk?? How is the financial system inavyo operate hapo? Hamna safe?? Hana ATM card? Zilikuwa ni makusanyo au ni malipo gani ambayo alitakiwa kuwa nazo cash mn7?? Something is not right here. I am only trying to think Loud as some JF member do.
   
Loading...