Kompyuta Ofisi ya DPP zenye kesi za Uhujumu Uchumi zaibwa

Uchaguzi ujao unahitaji pesa zisizoweza kuhojiwa sababu sina undugu na wafanyabiashara!!
Hakuna upelelezi utakaofanywa hapo,ni kama tukio la kupigwa risasi lisu
 
Taarifa za chinichini zinasema kwamba lipo kundi la viongozi Wa juu wastaafu linapanga njama za kumuhujumu jpm, Na kundi hili lina watu wake waliopo serikalini ngazi za juu. Pia kundi hill lina baadhi ya watuhumiwa Wa escrow.Hivyo swala hill huenda wanahusika.
Una umri gani mkuu?
 
Kwanza hongera na karibu kwenye platinum club mkuu.

Hapa naona iko namna, kama mti mbichi unafanyiwa hivi, mkavu itakuaje? Ofisi ya DPP kuibiwa fedheha sana ujue.

Na wakatoka kifua mbele kabisa habari imeandikwa kwa gazeti, na kibwagizo kidogo kimesisitiza eti kwenye hizo compyuta zilizoibiwa kuna taarifa za wahujum uchumi na mafisadi walioomba kusamehewa na kurudisha pesa.

Najiuliza, hao jamaa walipeleka email au barua hard copy?

Pesa zinawekwa kwenye kompyuta au bank?

Kwamba kompyuta zimeibiwa, sawa! Ni kusema kitu gani kimeathirika, majina au pesa walizoahidi kulipa zimepotea au kumbukumbu gani hazipo na zitaathiri vipi hili movie letu jipya?

Bado natafakari kitu gani hasa tunataka kuonyeshwa hapa.

Uzuri mkuu wetu aliwahi kusema wasifikirie watanzania ni wajinga kiasi cha kuamini kila sarakasi.
Na hapa ndio tutaelewa kwanini watuhumiwa waliambiwa kuandika barua peke yako na sio kupitia wakili. Hii maana yake nakala zote zilipelekwa ofisi ya DPP hivyo hakuna uthibitisho ni wangapi walikiri.
 
"Data" siku hizi hazipotei hata ukiiba "computers" zote.

Ikiwa visimu vyetu tu vina "data backups" za Kimatakfa itakuwa data za sehemu nyeti kama hiyo? Fikiri.

Na kama walikuwa hawana "backups" za uhakika basi hiyo ofisi wote wachukuliwe hatua kali sana kuanzia DPP mpaka mfagizi wa ofisi.

Watakuwa wote wamesomea ujinga.
Kimatakfa×
Kimataifa✓
 
WASHITAKIWA WIZI OFISI YA DPP WAONGEZEKA
Na Happiness Katabazi

IDADI ya washtakiwa wa wizi wa gari na kompyuta, mali ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) inazidi kuongezeka kutokana na mshtakiwa mwingine kufikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam.

Mshtakiwa huyo Abubakari Kamugisha (31) ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Kinyerezi, jijini, alifikishwa mahakamani hapo mwishoni mwa wiki na kusomewa shtaka la wizi wa kutumia silaha.

Kuongezwa kwa mshtakiwa huyo katika kesi hiyo kunafanya idadi ya washtakiwa wanaokabiliwa na tuhuma hizo kufikia 12.

Akisomewa mashtaka hayo na Inspekta Emma Mkonyi alidai Machi 5, Tabata Liwiti CCM, Kamugisha aliiba gari STK 5002 Toyota Hiace modeli mpya lenye thamani ya sh 56,972,000, komyuta sita zenye thamani ya sh 4,250,000, printa zenye thamani ya sh 7,435,000, seti ya UPS, laptop na vitabu vya sheria mali ya ofisi ya DPP na vitu vyote hivyo vikiwa na jumla ya thamani ya sh 111,500,000.

Alidai kwamba kabla ya kuiba vitu hivyo alimtishia kwa bunduki Alfa Makamba, mlinzi wa gereji ambayo gari hilo lilikuwa limelazwa.

Mshtakiwa alikana tuhuma hizo mbele ya Hakimu Mkazi, Eva Nkya, na kupelekwa rumande kuwa kesi hiyo haina dhamana kisheria.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni dereva ofisi ya DPP, Ally Ramadhani Mustapha, Haji Mwanga, Bakari Makara, Deogratus Coster, Philipo Jose, Athony Mengi, Mary Lyimo, Jacob Mosha, Wilfred Maleko, Alex Kimario na Hajat Faraji Kileo.

Chanzo:Gazeti la Tanzania Daima la Jumanne, Mei 19, 2009

Inanikumbusha kilichotokea mwaka 2009!
Mbona wengi hapo ni wachaga?
 
Back
Top Bottom