Kompyuta Ofisi ya DPP zenye kesi za Uhujumu Uchumi zaibwa

Kwani ukiiba computa ndo data zinapotea?!!

Data zipo kwenye backup servers kama hawana basi hazikuibiwa ila wamezisogeza tu!! Kila siku lazima kuwa na backup na kila dakika 15 kunakuwepo na automatic backup katika institution yeyote ile duniani labda not applicable kwa Tanzania ni mpaka Rais akafanye kazi hiyo!
 
Mimi niliamini kuwa wezi hawa wamekwenda kuiba taarifa, na ndiyo sababu iliyowafanya waibe komputa. Kipindi sisi tunasoma IT, tulifundishwa kuwa data huwa zinakaa kwenye hard disk, na si kwenye Processor. Vipi siku hizi kuna modern machines ambazo zinahifadhi data kwenye CPU? Hiki kitu kinakuwa kigeni sana kwangu, na ndiyo maana huyo uliyem-quote ameuliza swali hilo alilouliza, mimi nadhani yuko sahihi
Shida hamuelewan mwenzio anajua cpu ni lile boksi kumbe ni processor ambayo ipo mle ndan ya lile boksi kifupi hard drive na cpu zote zinapatikana ndan ya lile boksi na data sheet nahitaj zinahifadhiwa ndan ya hard drive
 
Shida hamuelewan mwenzio anajua cpu ni lile boksi kumbe ni processor ambayo ipo mle ndan ya lile boksi kifupi hard drive na cpu zote zinapatikana ndan ya lile boksi na data sheet nahitaj zinahifadhiwa ndan ya hard drive

😂 😂 Na watu wengi wanajua CPU ni lile boksi
 
Kuna ka habari kanatrend sehemu kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ofisini kwake kumetokea uhalifu wa kuibiwa kwa CPU za kompyuta zote zenye data.



---
Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi, Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amekiri kwa njia ya simu kwamba tukio hilo ni la kweli.

"Kweli tukio hilo limetokea na polisi tumepokea taarifa Jumanne asubuhi, mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo," alisema Kamanda Mambosasa kwa njia ya simu wakati akizungumza na Nipashe.

Akifafanua zaidi alisema kwa sasa jeshi lake linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo, DPP alipopigiwa simu yake ya mkononi mapema jana kuhusu tukio hilo na idadi ya kompyuta zinazodaiwa kuibwa, alisema kwamba yuko kwenye kikao.

"Ndiyo nakusikia kwa sasa niko kwenye kikao," alisema DPP na kukata simu.

Kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe Jumanne, Oktoba 15, mwaka huu, asubuhi ilibainika kuibwa kwa kompyuta hizo.

Baadhi ya kesi zilizopo katika hatua ya makubaliano ni ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa IPTL, Harbinder Sethi na James Rugemarila, wanaodaiwa kutakatisha zaidi ya Sh. bilioni 309.

Watuhumiwa wengine ni mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera, anayetuhumiwa kukwepa kodi na kutakatisha jumla ya Sh. milioni 173.

Mtuhumiwa mwingine ni Yusuf Ally, maarufu Mpemba wa Magufuli anayetuhumiwa kusafirisha nyara za serikali zenye thamani zaidi ya Sh. milioni 200.


Chanzo: Nipashe

Magu bana na style Yale ya ujambazi wa kidola, tangulini awamu hii hela za umma zikalipwa cash badala ya GePG,
Alafu eti anapambana na ufisadi
 
Mimi niliamini kuwa wezi hawa wamekwenda kuiba taarifa, na ndiyo sababu iliyowafanya waibe komputa. Kipindi sisi tunasoma IT, tulifundishwa kuwa data huwa zinakaa kwenye hard disk, na si kwenye Processor. Vipi siku hizi kuna modern machines ambazo zinahifadhi data kwenye CPU? Hiki kitu kinakuwa kigeni sana kwangu, na ndiyo maana huyo uliyem-quote ameuliza swali hilo alilouliza, mimi nadhani yuko sahihi

Acha kukariri IT lectures. Jaribu kuelewa. Ningekuelimisha lakini nitakuwa nje ya mada.
 
"Data" siku hizi hazipotei hata ukiiba "computers" zote.

Ikiwa visimu vyetu tu vina "data backups" za Kimataifa itakuwa data za sehemu nyeti kama hiyo? Fikiri.

Na kama walikuwa hawana "backups" za uhakika basi hiyo ofisi wote wachukuliwe hatua kali sana kuanzia DPP mpaka mfagizi wa ofisi.

Watakuwa wote wamesomea ujinga.

Office Muhimu kama ile haiwezi kukosa vyote hivyo ulivyo viainisha hasa ukizingatia unyeyi wake ,tatizo nnalo liona hapa ni Nia ovu zilizo nyuma ya walio iba hizo Computer...
 
Hao jamaa walioingia kuiba siyo wajinga, walisha calculate risk ya tukio na uhakika wa kukamilisha lengo lao na usalama wa uwizi wao na hata kuhusisha watu wa ndani ya taasisi husika tena wenye nyadhifa na watoa maamuzi kwenye taasisi. Hivyo vitu kama vimefanywa na wabobezi wa mambo hayo sidhani kama hata wataacha ushahidi kwenye eneo la tukio na hata kama wakiacha itakuwa ni kwa ajiri ya kuwapoteza maboya na kuwasumbua wapelelezi.
 
Zilishaibiwa computer za taasisi flani walikuja hadi polisi wa picha kwa ajili ya kutafuta ushahidi wa wahusika ila hawakuambulia kitu. Hivi vitu huwa ni well planned
 
Kwani Mnajua maana ya HDD Pili System Unit tatu CPU?
britanicca ww hutakiwi huku, tutakusaidia ichunge Mada kwani muelekeo zilipokwenwenda kunaanza kujionesha kaa ufahamu wengi wanabofya tu humu JF kwa hiyo wanabwabwaja, km na hapa hawataelewa CPU zilizoibiwa ni zipi basi
1571412904821.png

List of Computer Hardware
  • Motherboard.
  • Central Processing Unit (CPU)
  • Random Access Memory (RAM)
  • Power Supply.
  • Video Card.
  • Hard Drive (HDD)
  • Solid-State Drive (SSD)
  • Optical Drive (e.g., BD/DVD/CD drive)
 
Hata kama zitakuwa zimeibiwa,mtu wa IT atakuwa na cha kujibu maana anatakiwa awe anafanya backup angalau kwa wiki mara moja,kwahiyo sidhani kama kutakuwa na uzembe wa kiasi hicho kwa issue sensitive kama hiyo...
taarifa hizo haziwezi kusambaa kihivyo nahisi ni Computer moja tu ya Boss ndio ina siri hizo
na kwanini walichelewa kumjibu Ruge maombi yake
britanicca na wengi mnakumbuka Rugakingila alivyororoka Keko (Uncle Tom) mbona ndio ikawa mwisho?
haya mambo yanafika mwisho (wakati Ukuta) km Mahakama imeshasema hela ni za PAP na VIP sasa kuwachunguza wengine ya nini kamatisheni mpunga km wengine (wale wa Gereza la Keko waliotoa na escort)
 
Back
Top Bottom