Kompyuta Ofisi ya DPP zenye kesi za Uhujumu Uchumi zaibwa

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,634
30,000
Kuna ka habari kanatrend sehemu kwamba Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) ofisini kwake kumetokea uhalifu wa kuibiwa kwa CPU za kompyuta zote zenye data.



---
Kamanda wa Kanda Maalum ya Kipolisi, Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, amekiri kwa njia ya simu kwamba tukio hilo ni la kweli.

"Kweli tukio hilo limetokea na polisi tumepokea taarifa Jumanne asubuhi, mpaka sasa hakuna mtu anayeshikiliwa kuhusiana na tukio hilo," alisema Kamanda Mambosasa kwa njia ya simu wakati akizungumza na Nipashe.

Akifafanua zaidi alisema kwa sasa jeshi lake linaendelea na uchunguzi kuhusu tukio hilo.

Hata hivyo, DPP alipopigiwa simu yake ya mkononi mapema jana kuhusu tukio hilo na idadi ya kompyuta zinazodaiwa kuibwa, alisema kwamba yuko kwenye kikao.

"Ndiyo nakusikia kwa sasa niko kwenye kikao," alisema DPP na kukata simu.

Kwa mujibu wa chanzo cha Nipashe Jumanne, Oktoba 15, mwaka huu, asubuhi ilibainika kuibwa kwa kompyuta hizo.

Baadhi ya kesi zilizopo katika hatua ya makubaliano ni ya uhujumu uchumi inayowakabili vigogo wa IPTL, Harbinder Sethi na James Rugemarila, wanaodaiwa kutakatisha zaidi ya Sh. bilioni 309.

Watuhumiwa wengine ni mwandishi wa habari za uchunguzi, Erick Kabendera, anayetuhumiwa kukwepa kodi na kutakatisha jumla ya Sh. milioni 173.

Mtuhumiwa mwingine ni Yusuf Ally, maarufu Mpemba wa Magufuli anayetuhumiwa kusafirisha nyara za serikali zenye thamani zaidi ya Sh. milioni 200.


Chanzo: Nipashe
 
Bado kuna fungu anaendelea kupokea ..sijui kama tutabaki salama
b67bcfbf-8ad9-4db5-b79b-228d08f35162.jpg
354ae314-8e17-470e-b375-7907c0b8b342.jpg
 
Kigogo kaipata Kwa aliyenipatia nadhan

Ambaye hana Jina? Hebu mtaje ili nami nijiridhishe kwa Jina la Mtu Mmoja hivi niliyepewa Mkuu. Najua hutoaniangusha kwa hili. Nahisi atakuwa ni Mtu huyo huyo henu nitajie halafu na Mimi nitakujia Mtu mwingine ili Siku zingine ukiwa unataka taarifa za ndani kabisa uwe unamtafuta Yeye Mkuu sawa? Wewe ni Rafiki yangu halafu hujawahi hata Kuniangusha na tupo wote pia katika haya Mapambano. Nasubiria Mkuu kabla sija ' Log Out ' hapa dakika 29 zijazo.
 
Back
Top Bottom