mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,664
- 18,039
Kukosekana kwa wachezaji fulani kwenye Kombe la Dunia kunachangia kutukosesha vionjo tulivyovitarajia. Kwa mfano kokosekana kwa mchezaji bora wa Dunia kwa sasa Benzema (mtaalam wa kutupia), kukosekana kwa Halaand (mtupiaji mwenye mabavu), kukosekana kwa Mane (mtalaam wa kutupia), kukosekana kwa Mohamed Salah (mshambuliaji machachari).
Wachezaji hawa aidha ni majeruhi au mataifa yao hayakufuzu kuingia kwenye kinyang'anyiro cha Kombe la Dunia. Nguli waliopo wamepoteza sana makali kama vile Christiano Ronaldo na Messi ambao hawapo kwenye kiwango chao kutokana na umri (pengine).
Kiukweli hakuna anayeweza kutusahaulisha vionjo kama vya kina Zinedane Zidane, Ronaldinho, Ronaldo wa ukweli (the phenomenone), n.k.
Kwa kweli vitu adimu hatujaviona kabisa hadi sasa! Kwa wakongwe kwenye ushabiki wa soka wananielewa! Pasi zenye macho na 'free kick' kama za David Beckham zimekuwa simulizi za kale! Naona kama Kombe la Dunia linakuwa la kawaida sana!