Kombe la Dunia 2022: Droo ya Hatua makundi

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,909
25,183
thumbs_b_c_1bfd972445bd82f7262d5dd703a9ccb2.jpg


Ikiwa imesalia miezi michache kwa kombe la Dunia mwaka 2022 kuanza, leo hii itafanyika Droo ya hatua ya makundi ya michuano hiyo mjini Doha. Droo hiyo itafanyika katika Kituo cha Maonyesho na Mikutano cha Doha, huku washindi wa zamani wa Kombe la Dunia kama vile Cafu na Lothar Matthaeus wakiwa kati ya wasaidizi wa droo hiyo.

Washindi wa mwisho wa Kombe la Dunia Ufaransa itakuwa katika kundi la Kwanza litakalojumuisha mataifa saba ya juu katika viwango vya FIFA na vile vile Qatar wanaoshiriki kwa mara ya kwanza, wakiwa katika nafasi ya 51 kwa ratiba ya FIFA wakijumuishwa kwenye kundi hilo kwa kuwa wao ni wenyeji wa mashindano ya mwaka huu. Kundi hilo litajumuisha timu pia timu ya taifa ya Brazil, Ubelgiji, Argentina, Uingereza, Uhispania na Ureno. Hiyo pia inamaanisha Ujerumani, baada ya kuondolewa nje ya Kombe la Dunia katika hatua ya makundi mwaka wa 2018, ndio jina kubwa zaidi katika Chungu cha Pili, ambacho pia kina Uholanzi na Croatia.

Mabingwa wa Afrika Senegal, Japan na Poland ni miongoni mwa timu katika chungu cha tatu, na Canada watakuwa katika chungu cha nne katika mechi yao ya kwanza tangu 1986.

Karibuni tupate updates mbali mbali.

==
Pots za droo ni kama ifuatavyo
WORLD_CUP_POTS.png

==
Official mascot wa kombe la dunia 2022

20220401_190515.jpg


==
Baada ya burudani na maneno mbali mbali ya ufunguzi kutoka kwa viongozi mbali mbali zoezi linatarajia kuanza sasa.

==
Droo kamili ni kama ifuatavyo

GROUP A
Qatar
Ecuador
Senegal
Netherlands


GROUP B
England
Iran
USA
Wales or Scotland or Ukraine


GROUP C
Argentina
Saudi Arabia
Mexico
Poland


GROUP D
France
UAE or Australia or Peru
Denmark
Tunisia


GROUP E
Spain
Costa Rica or New Zealand
Germany
Japan


GROUP F
Belgium
Canada
Morocco
Croatia


GROUP G
Brazil
Serbia
Switzerland
Cameroon


GROUP H
Portugal
Ghana
Uruguay
Korea Republic

=====

FPRmMBwWYBAykL5.jpeg
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom