Komba, ulijuaje Nyerere atakufa hadi utunge nyimbo za maombolezo yake??

nakumbuka ilikuwa mida ya saa nne pale shuleni, tulikuwa tunajiandaa kwenda kunywa uji. mara tukatangaziwa baba wa taifa ameaga dunia. Hapo hapo tukaanza kusikia nyimbo za komba. Alikuwa ameshatoa album. je hiyo album aliitunga mda gani na alijuaje atakufa? kama wimbo wa haraka kukamilika unachukua hata wiki tatu je album itachukua mda gani? Naomba Komba unifafanulie. Hasa naomba ule wimbo uliobeba jina la album.(taifa lahuzunika pamoja twasema kwaheli..kwaheri baba..mwalimu nyerere).
Jamani mwacheni Komba ni geneous linapokuja issue ya kutunga nyimbo kwa hiyo wakubwa msishangae hata kidogo
 
Umenikumbusha mbali mkuu, yule waziri mkuu wa Israel Ariel Shalon aliwekewa hiyo life suppoting machine tangu mwaka 2004 nasikia mpaka sasa hawajalizima.

Na wakiizima dakika hii basi atatangaziwa kufa. Hiyo inaeleweka lakini hawawezi kuzima mpaka familia yake itoke ruhusa.
 
kepteni joni komba ALIKUA ANATANIA TU, walikua wanapiga story na BENJAMIN MKAPA NYERERE,basi benja akamtania tu kepteni komba kwamba JKN atakufa hivi karibuni,we fyatua albam nzima ya maombolezo,basi na kepteni nae akatania tu akafyatua kaalbamu kamoja tu cha maombolezo
 
hii kama inanishawishi hivi.......pengine

Bwana mdogo sisi tulikuwepo enzi zile, siyo nyinyi wa dot.com munadhani hizo internet services na simu zilikuwa accessible kwa wote kama iliivyo sasa.

Enzi zile kwa tz kuwa na email service tu ilikuwa dola 50 kwa mwezi sasa jaribu kufikiria ni wangapi walikuwa na uwezo huo? Na huko maofisini mabosi wazee walikuwa hawaelewi wala hawaoni umuhimu wa email na internet na walikuwa bado kwenye typewriter.

Taarifa yote ilikuwa wazi kwenye BBC kuhusu afya ya Nyerere na mpaka kifo chake, hakukuwa na cha ajabu wala cha kuficha. Sasa nyinyi kwa kuwa siku hizi munadonoa tu hebu jaribuni kusearch pengine mutaona mambo yalikwenda vipi.

Hapo pa kumzulia Mzee wa watu Mkapa kwamba alishiriki siyo fair hata kidogo.
 
mods toeni huu uzi kama mlivyotoa ule uzi wa ukweli ambao ulikuwa unamwaga hadharani ubadhirifu wa Slaa na Mbowe chadema

Kwa mara ya kwanza nimetambua JF huenda ina agenda flani hivi za siri, nilishangaa pia baadae kurudi kwa nia ya kufuatilia thread naona haionekani kumbe waliitoa! Sababu hasa ni zipi?
 
Swali limenasia,very interesting mimi niko upande wako kijana,kuna vichwa hapa jf si mchezo subiri wako busy watakuja tu kukujuza ukweli au wameamua kupotezea,kuna mtu anasema komba ni mjeshi alichukua biti za kijeshi fasta fasta mambo yakajipa HAKUNA KITU KAMA HICHO,bahati mbaya jf si rahisi kujua waliopo hapa wana fani gani,jf ni kila kitu hata wanajeshi wapo hapa huyo si kapteni tu kunawalio na vyeo zaidi ya hicho ninaowafahamu wapo jf mimi mwenyewe nilifanya kazi huko jeshini mambo ya huko,nayajua tatizo hapa ni muda uliotumika.
 
Mada ambayo mtoa hoja ameileta haina tija kwa jamii.Hilo ulilouliza Komba mwenyewe alishalitolea ufafanuzi kwamba zile ni beats za kijeshi.Kama utakumbuka Komba ni captain mstaafu wa jeshi na siyo hilo tu hata wana TOT wa awali wote awalikuwa waastaafu wa jeshi.Hivyo inawachukuwa muda mfupi kuweza kukamilisha wimbo.

Kwa manufaa ya wale ambao hakujaliwa kupitia jeshini wenzetu kwa utamaduni wa kijeshi wana taratibu nzuri sana za namna ya kuandaa na kuzika wanajeshi wao.
Huwa hawakurupuki tu.
Kwa kifupi Komba alitumia taaluma yake ya kijeshi na kunakili beats za jeshi ambazo tayari zipo, na kuweza kutoa nyimbo katika muda mfupi tu.

Ule wimbo maalum instrumental yake ndiyo iliyotumiwa na wanajeshi kushusha mwili kwenye ndege na kutembea nao kwa mwendo wa pole mpaka kwenye gari maalumu la mzinga ambalo lilitumika kubeba mwili wa mwalimu! Ni kweli kabisa ule wimbo ni common jeshini na waimbaji ishirini na nane kwa kikipindi kile walikuwa wastaafu wa jeshi pamoja na Komba mwenyewe.
 
MMK anaxema ni beat za wangoni. Mwingine anasema ni beat za kijeshi. Ni kama hesabu ya 22 gawa kwa 7.
 
kwani inachukua muda gani kutunga wimbo? kwa mtunzi wa ukweli masaa 4 yanatosha kabisa mbona kuna wasanii wa ubongo wa fuleva huwa wanatungia nyimbo studio na kurecord siku hiyo hiyo
Mkuu kuna wengine wanajisikia tabu saana kufikiri wao kila kitu ni shortcut.Hapo umeuliza swali la msingi sana.
 
hujui mambo ya muziki kaa kimya...nyimbo gani unaweza kutunga masaa 4??
Tatizo lako unataka unachoamini wewe na wengine waamini hivyo.HIvi hujaona uimbji wa freestyle wewe kwani wanatunga kwa masaa mangapi?kutunga nyimbo sio kama kusafiri kutoka dar hadi rukwa,au dar to lindi au dar to bukoba nyimbo inaweza kutungwa tena hata kwa nusu saa tu.
 
Katunga na wimbo wake pia?
Juzi nilimuona kajaa kama roba la mihogo la Tandale huku akijikongoja kwa fimbo kama kishaibu mwenye miaka 90 wakati nni mtu wa 1954??

Laana imeanza kumrudi mapema. Lakini kwa nini isianze na muuwaji BMW ianze na mshangiliaji wa kifo komba?
 
Ugonjwa na hali ya aliyokuwa nayo Nyerere huko Hospitali Uingereza hakuna ambae hakujuwa kuwa hiyo ndiyo ilikuwa safari.
 
nakumbuka ilikuwa mida ya saa nne pale shuleni, tulikuwa tunajiandaa kwenda kunywa uji. mara tukatangaziwa baba wa taifa ameaga dunia. Hapo hapo tukaanza kusikia nyimbo za komba. Alikuwa ameshatoa album. je hiyo album aliitunga mda gani na alijuaje atakufa? kama wimbo wa haraka kukamilika unachukua hata wiki tatu je album itachukua mda gani? Naomba Komba unifafanulie. Hasa naomba ule wimbo uliobeba jina la album.(taifa lahuzunika pamoja twasema kwaheli..kwaheri baba..mwalimu nyerere).
Mkuu umelenga kuporomosha kitambi cha komba ? Muimba kwaya atawezaje kujibu swali gumu kama hili ?
 
Back
Top Bottom