Historia ya Komandoo Tarimo

Wadau niko njiandaa kuandika historia ya komandoo wa kitanzania aliye kuwa akitwa Tarimo, kijana huyu alipata mafunzo yake kule Cuba, na baadae kurejea nyumbani Tanzania.

Je kuna mtu awaye yeyote mwenye ufahamu wa ili Jambo? naomba michango yenu zaidi.

Thread yako haijatosheleza tueleze baada ya kupata mafunzo Cuba aliifanyia nini nchi yake hadi atambuliwe na jf maana kama ni makomandoo tunao wengi waliosoma CUBA, ISRAEL, URUSI, MAREKANI NA kwingineko Duniani kuna nini special juu ya huyu Tarimo wako? Kama hakuna nenda kwao watakupa kila kitu.
 
Uliza familia yake, tafuta picha yake uweke pamoja navitu aliofanyia taifa si kuleta porojo.
 
Mimi namkumbuka komando halisi TAMIM!! Wangapi mnamkumbuka huyu na alifanya nini? Hint: Unamkumbuka uncle Tom? Haya vijana somo la historia ya nchi yenu, waulizeni wazee wenu waliohai!!

Ndinani, umenikumbusha mbaaali sana, miaka ya 1983 au 1984 nikiwa shule ya msingi. Nilikua nafuatilia story za hawa jamaa waliokuja kujulikana sana baadae katika 'Kesi ya Uhaini'. Moja ya story ya Captain TAMIM ya kusisimua ni ile katika kukimbia asikamatwe na askari kanzu akaona lorry/gari ya wazi nyuma ikiwa imebeba crate kibao za bia akarukia na kudandia gari lile akaanza kuwavurumishia chupa za bia askari waliokuwa wanamfukuza ili wamkamate..., it is so sad kuwa ultimately akapigwa risasi na kuuwawa!

Two weeks ago nilienda Bukoba, pale airport nilikutana na mwenzao katika kesi ile, kama sijakosea anaitwa Captain Roberts. Wameshakuwa aged sasa hawa watu, unfortunately alikuwa kalewa sana. Angekua katika akili ya kawaida nilitamani kuongea nae nijue wakati huo walikusudia kuifanyia nini nchi zaidi ya kile tulichokuwa tunafanyiwa na viongozi wetu wakati ule.
 
Mimi namkumbuka komando halisi TAMIM!! Wangapi mnamkumbuka huyu na alifanya nini? Hint: Unamkumbuka uncle Tom? Haya vijana somo la historia ya nchi yenu, waulizeni wazee wenu waliohai!!

Ndinani mbona umeogopa kumalizia? Kweli kaka huyu komandoo alikuwa anaitwa MOHAMED TAMIMU alichofanya ndicho kilisababisha asafiri safari wasiyorudi mnamo miaka ya 1982/83 mwezi sikumbuki
 
Mmenikumbusha mbali kuhusu Komandoo Tamimu. Habari ile ingeweza kutengeneza filamu (based on a true story). Kweli stelingi hafi. Alipouawa Tamimu tu na ladha ya story ikabadilika. Maskini Tamimu! Hivi hakumbukwi kama shujaa?
 
Mimi namkumbuka komando halisi TAMIM!! Wangapi mnamkumbuka huyu na alifanya nini? Hint: Unamkumbuka uncle Tom? Haya vijana somo la historia ya nchi yenu, waulizeni wazee wenu waliohai!!

Uncle Tom alipigwa risasi na kuuawa siku moja kabla ya siku ambayo yangefanyika mapinduzi ya serikali ya Tanganyika.

Baada ya maiti yake kupekuliwa alikutwa na karatasi yenye majina ya viongozi mbalimbali wa jeshi pamoja na mawasiliano yao jambo ambalo liliwatia mashaka wana Usalama maana uncle Tom alikuwa most wanted na ilikuwa ishatolewa amri ya kukamatwa au kuuawa pale atakapoonekana ndani ya Tanganyika.

Ndipo ukaanza msako wa kukamata kila aliyeonekana kwenye ile karatasi na mpango mzima wa mapinduzi kuwa wazi....
 
Ndinani mbona umeogopa kumalizia? Kweli kaka huyu komandoo alikuwa anaitwa MOHAMED TAMIMU alichofanya ndicho kilisababisha asafiri safari wasiyorudi mnamo miaka ya 1982/83 mwezi sikumbuki

Bukombe kuna sehemu lakini unaelezea watu humu Jamvini jinsi wanavyorudi, au umeisha sahau ndugu yangu?
 
Back
Top Bottom