Kodi ya Watengeneza Maudhui Mtandaoni: Ubunifu unakufa taratibu

Kodi ya Watengeneza Maudhui Mtandaoni: Ubunifu unakufa taratibu

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Ni Desemba 16, 2025, Kampuni ya Meta ilithibitisha rasmi kupokea ombi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) la kukata kodi ya asilimia 5 kwa kila malipo yanayolipwa kwa Watengeneza Maudhui (Content Creators) wanaoishi Tanzania. Utekelezaji wa mfumo huu unaanza Desemba 21, 2025, hatua inayozua mjadala mpana kuhusu mustakabali wa ubunifu wa kidijitali nchini.
1765950182141.jpg

Kwa mujibu wa utaratibu huu, mtengeneza maudhui aliyepaswa kulipwa TSh milioni mbili atalazimika kukabidhi TSh 100,000 kama kodi, bila kujali ukubwa wake au changamoto alizopitia kufikia kiwango hicho. Makato haya yanahusu mapato yanayotokana na programu za Facebook kama Stars, Subscriptions, Bonuses na Content Monetisation Beta, pamoja na Instagram kupitia Gifts, Subscriptions na Bonuses.
images - 2025-12-17T090619.680.jpeg

Meta inajiunga na YouTube, ambayo tayari imeanza makato ya aina hii tangu Julai 2025. Hata hivyo, swali kubwa linalobaki ni: Je mfumo huu unahamasisha ubunifu au unauua kabsa?
images - 2025-12-17T090533.994.jpeg

Kwa uhalisia, kodi hii inaumiza zaidi watengeneza maudhui wadogo—wale wanaojitahidi kukuza akaunti zao, kununua vifaa, intaneti na muda. Asilimia 5 kwa mkubwa na mdogo ni sawa kisheria, lakini kiuchumi ni pengo kubwa. Mbaya zaidi, makato haya yanakuja juu ya mlolongo mrefu wa kodi zingine: vocha, miamala ya simu, benki na huduma za mtandao ambazo poa TRA huchukua kodi.
images - 2025-12-17T090448.326.jpeg

Badala ya kujenga mazingira rafiki ya uchumi wa kidijitali, hatua hii inaonekana kama kukata tamaa ya ubunifu kabla haujakua. TRA inaonekana mahiri sana katika kubuni njia za kukusanya kodi, lakini dhaifu katika kueleza wazi matumizi ya fedha hizo kwa maendeleo ya wananchi.
1765950182141.jpg

Swali la msingi linabaki: Je Tanzania inataka kukuza uchumi wa ubunifu au kuudhibiti mpaka ufe? Kama sera hazitatazamwa upya, huenda ndoto ya vijana wengi wa kujitegemea kupitia maudhui ya mtandaoni ikabaki kuwa hadithi tu. Wataalamu wenu wa masuala ya ushauri wa kodi wanawashauri vitu gani?
 
Aliyekudanganya ccm wanataka kukuza ubunifu nani,wao wanataka hela walipane vizuri hayo ya ubunifu baki nayo wewe.

Hope inaenda mpaka kwa wasanii wanaojipendekeza kwa watawala,hii itawafundisha namna nzuri ya kuwajua hawa wanasiasa walivyo.
 
Na mambo yanazidi kuwa magumu zaidi
 
Sawa tu sisi wafanyakazi mbona tunakatwa 10%
Ushawahi jiajiri mitandaoni ndugu? Ile stress yake?
Nyinyi at least hata mna pa kukimbilia kibarua chenu kikiota nyasi.
Huko mitandaoni ukipata shida ni kuandika email hadi kuchoka.
Na bado twitter imefungwa, Tiktok nk

Hii ni malipo yangu ya juzi. Nilikatwa laki Sita kabisa kama táx.
Screenshot_20251217-103429~2.jpg
 
M
Ushawahi jiajiri mitandaoni ndugu? Ile stress yake?
Nyinyi at least hata mna pa kukimbilia kibarua chenu kikiota nyasi.
Huko mitandaoni ukipata shida ni kuandika email hadi kuchoka.
Na bado twitter imefungwa, Tiktok nk

Hii ni malipo yangu ya juzi. Nilikatwa laki Sita kabisa kama táx.
View attachment 3516488
Kuu hapo naona $156 makato ndio 600k au kuna makato hayaonekani hapo?
 
Ushawahi jiajiri mitandaoni ndugu? Ile stress yake?
Nyinyi at least hata mna pa kukimbilia kibarua chenu kikiota nyasi.
Huko mitandaoni ukipata shida ni kuandika email hadi kuchoka.
Na bado twitter imefungwa, Tiktok nk

Hii ni malipo yangu ya juzi. Nilikatwa laki Sita kabisa kama táx.
View attachment 3516488
Duuh aisee mbona noma sana
 
Back
Top Bottom