Makyomwango
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 322
- 79
Great thinkersKama mnavyoelewa bajeti iliyosomwa na mkulo majuzi ilipendekeza kufutwa kwa kodi ya mapato katika posho zote zinazolipwa kwa watumishi wa umma walioko katika serikali kuu, serikali za mitaa ma taasisi nyingine ambazo zinapata ruzuku kutoka serikalini. Pendekezo hili lina lengo la kuwaaminisha wazalendo na watanzania kwa ujumla kwamba serikali imekuwa ikikusanya kodi hizo kutoka kwa watumishi husika. Ukweli ni kwamba watumish hao ambao ni wachache sana (Mawaziri, Makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa idara nakadhalika) wamekuwa hawakatwi kodi katika malipo hayo na hata katike salary slip zao hayaonekani.Posho hizo ambazo ni pamoja na Housing allowance, Utility allowance, transport allowance zinatakiwa kuatwa kodi kwa mujibu wa sharia ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 kifungo kidogo cha 2 (a) kikisomwa pamoja na kifungu cha 81 kifungu kidogo cha (1) na (2).Serikali, ama kwa uzembe au kwa makusudi (kwa ufisadi) imekuwa haikusanyi kodi hiyo kutoka kwa vigogo hao na sasa inataka kufuta makosa hayo kwa kusamehe kodi hizo kisheria. Pendekezo la kufutwa kwa kodi ya posho hizo siyo tu lina lengo la kuficha uozo na upendeleo katika kuwakata watumish kodi ya mapato bali pia kuwapendelea watumishi hao wachache na hivyo kuongeza pengo la kipato cha chini na cha juu Napendekeza makamanda walioko bungeni pamoja na wabunge wengine wazalendo wamtake mkulo na serikali kwa ujumla kufanya yafuatayo:a) Kulitaarifu bunge kiasi ambacho imekusanya kodi ya mapato kupitia posho hizo kwa miaka mitano iliyopitab) Kulitaarifu bunge idadi ya watumishi na vyeo vyao watakaofaidika na msamaha wa kodi hiyo.c) Kulitaarifu bunge juu ya watumishi ambao hawajahi kukatwa kodi hizo na hatua zitazochukuliwa kwa watimishi hao na viongozi wao kwa kukwepa kulipa kodi kwa mujibu wa shariaNawasilisha