Kodi inayoombewa kufutwa katika posho za watumishi wa Umma haijawahi kukusanywa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kodi inayoombewa kufutwa katika posho za watumishi wa Umma haijawahi kukusanywa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Makyomwango, Jun 11, 2011.

 1. M

  Makyomwango JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 323
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Great thinkersKama mnavyoelewa bajeti iliyosomwa na mkulo majuzi ilipendekeza kufutwa kwa kodi ya mapato katika posho zote zinazolipwa kwa watumishi wa umma walioko katika serikali kuu, serikali za mitaa ma taasisi nyingine ambazo zinapata ruzuku kutoka serikalini. Pendekezo hili lina lengo la kuwaaminisha wazalendo na watanzania kwa ujumla kwamba serikali imekuwa ikikusanya kodi hizo kutoka kwa watumishi husika. Ukweli ni kwamba watumish hao ambao ni wachache sana (Mawaziri, Makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa idara nakadhalika) wamekuwa hawakatwi kodi katika malipo hayo na hata katike “salary slip” zao hayaonekani.Posho hizo ambazo ni pamoja na “Housing allowance”, “Utility allowance”, “transport allowance” zinatakiwa kuatwa kodi kwa mujibu wa sharia ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 kifungo kidogo cha 2 (a) kikisomwa pamoja na kifungu cha 81 kifungu kidogo cha (1) na (2).Serikali, ama kwa uzembe au kwa makusudi (kwa ufisadi) imekuwa haikusanyi kodi hiyo kutoka kwa vigogo hao na sasa inataka kufuta makosa hayo kwa kusamehe kodi hizo kisheria. Pendekezo la kufutwa kwa kodi ya posho hizo siyo tu lina lengo la kuficha uozo na upendeleo katika kuwakata watumish kodi ya mapato bali pia kuwapendelea watumishi hao wachache na hivyo kuongeza pengo la kipato cha chini na cha juu Napendekeza makamanda walioko bungeni pamoja na wabunge wengine wazalendo wamtake mkulo na serikali kwa ujumla kufanya yafuatayo:a) Kulitaarifu bunge kiasi ambacho imekusanya kodi ya mapato kupitia posho hizo kwa miaka mitano iliyopitab) Kulitaarifu bunge idadi ya watumishi na vyeo vyao watakaofaidika na msamaha wa kodi hiyo.c) Kulitaarifu bunge juu ya watumishi ambao hawajahi kukatwa kodi hizo na hatua zitazochukuliwa kwa watimishi hao na viongozi wao kwa kukwepa kulipa kodi kwa mujibu wa shariaNawasilisha
   
 2. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Miaka na miaka nijuavyo mimi watumishi wa serikali posho zao hazikatwi kodi, mkullo alikiwa anasherehesha hotuba yake tu!
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Wakuu lazima mfahamu kwamba Mkullo alikuwa akicheza karata za kisiasa kuonyesha kwamba watumishi wa Umma walikuwa wakilipa kodi hizo hivyo kumweka hatiani Dr.Slaa kwamba halipi kodi za posho..

  Hii ni mchezo umepachikwa harakaharaka lakini maadam umegundulika itabidi viongozi wote nchini na watumishi wote nchini wakatwe hizi kodi kwa sababu hazijawahi kukusanywa na nijuavyo mimi hakukuwa na kitu kaa hiki toka enzi za Mwalimu, Mwinyi hadi Mkapa. Wametunga tu sheria haraka ili kumbana Dr.Slaa..
   
 4. SG8

  SG8 JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 3,198
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Wakiendelea kumsumbua Dr Slaa tutawaumbua, mbona watumishi wengi tu wanalipwa posho zilizozidi kima cha chini ambazo zilitakiwa kukatwa kodi?
   
 5. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2011
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  kilichofanywa na Mkullo ilikuwa ni kubariki tu hizo posho kutokatwa kodi lakini siku zote zilikuwa hazikatwi kodi.taasisi zinazopata ruzuku ya serikali ni pamoja na vyama vya siasa japokuwa sina uhakika kama vyama vya siasa vinaangukia katika definition ya government funded institutions.
   
 6. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #6
  Jun 11, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hii bajeti ya Mkullo ni usanii mtupu. uliwahi kuona wapi bajeti inawasilishwa wakati bado kuna maamuzi muimu yanayoguza vyanzo vya mapato ambayo hayajapatiwa ufumbuzi! Viloja kama hivyo ndivyo vilivyopo katika bajeti ya Mkullo. Kwa mfano hivi sasa kuna tozo 20 katika bei ya mafuta ya petroli Mkullo amesema serikali inakusudia kupunguza tozo hizo kwa lengo la kushusha bei ya mafuta ya petroli. Hata hivyo uamuzi juu ya suala hilo hautatolewa mpaka baada ya bunge kuridhia mapendekezo yake ya bajeti. Mtu anajiuliza hao wabunge wetu wataridhiaje hayo mapendekezo ya bajeti ambayo hayajakamilika. Ikumbukwe katika mapendekezo yaliyotolewa kwenye hotuba hiyo ya bajeti lipo pia pendekezo la kuongezo mapato yanayokusanywa na halmashauri kutoka kwa wastani wa asilimia 3 ya pato la taifa hadi asilimia 5 kwa kurejesha baadhi ya kodi zilizokuwa zikikusanywa na halmashauri hizo zilizofutwa. Hata hivyo uamuzi wa ni kodi gani zitarejeshwa nao haujatolewa. Kwakuwa suala hili linaguza moja kwa moja maisha ya watu masikini walioko vijijini itakuwa ni jambo la ajabu ikiwa wabunge wetu wataridhia mapendekezo ya hotuba ya bajeti bila kwanza kupata ufafanuzi juu ya jambo hilo.
   
 7. B

  Bukyanagandi JF-Expert Member

  #7
  Jun 12, 2011
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 7,534
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Jamani mbona nimeshtuka sana! Are you sure GOVT employees hawakatwi kodi za posho? Damn! Je huu siukwepaji wa ulipaji kodi of a centuary, nchi za wenzetu zilizo endelea unaweza kufanya makosa mengine ukaonywa lakini si ukwepaji wa kulipa kodi, kwao hiyo ni fedhea na kosa la jinai culprit anaishia kuswekwa lupango bila kujali kama ni Raisi, waziri mkuu and what have you! Labda Hon Mkullo na Mr. Kitilya wa TRA wana majibu ya kulidhisha kuhusu SCAM hii, waseme wata-recover hizo kodi kivipi kutoka kwa wafanya kazi Serikalini.
   
 8. S

  Shidoto Member

  #8
  Jun 12, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Vile vile tusisahau kuna bahasha za khaki ambazo ndani yake huwekwa pesa (posho) kwa viongozi wakialikwa kwenda kufungua au kufunga mikutano, je hizo hukatwa kodi? Mara nyingi hizi huwa nyingi kuliko sitting allowance au per diem.
   
 9. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #9
  Jun 12, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  it is very likely hizo posho hazikatwi kodi ndo maana wakakimbilia kusema hawataka kodi kwa posho za wafanyakazi wa serikali au taasisi zinazopata ruzuku za serikali. najua wameamua kuwatenga wafanyakazi wa kwenye taasisi zisizo za serikali (mfano NGOs) kwa sababu kundi hili ndo linakatwa kodi.. kwa maneno mengine, kodi aliyosema Mkulo inaktwa kwa wafanya kazi wa NGO na taasisi nyingine zisizo za serikali na wafanyakazi walio wengi wa serikalini hawakatwi kodi hii!!.
   
 10. THE GAME

  THE GAME JF-Expert Member

  #10
  Jun 12, 2011
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 441
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Hii bajet ni usanii mtupuu..
   
Loading...