Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Hahaha mkuu sisi tulikua tunawarudisha nyuma alipo toka yani kila akienda mbele sisi tunamvuta nyuma tukichoka tunamuulia mbali ila ukimkanyaga imekula kwako
Ni kweli kabisa huyu ukimkanyaga umeumia ....hata ndugu yangu alivyoumwa na huyu mdudu chanzo alimkanyaga bila kumwona wakati anavuka barabara
 
Ukiwa unamsogelea anatoa sauti ya kukuonya siyo kwamba anakua kajikausha kua anakuogopa.

Isipokua sauti hua anaitoa kwa chini mno na kwa vile mara nyingi kukutana naye ni porini unaweza kuhisi ni majani ndiyo yanatoa mlio.

Na puff ader ndiyo death adder, mnyama kukabidhiwa jina hilo siyo shughuli ndogo.
Hakika nimevutiwa na maelezo yako kuhusu huyo nyoka kifutu kutoa sauti umsogeleapo. Umenikumbusha nilipoemushwa na Mungu kutoka kwenye kifo na hatari ya nyoka huyo. Nikiwa mdogo sana mkoa fulani hivi, nikiwa nimeinama kwenye shamba la mpunga uliokuwa katika hatua za kung'olea, sikuwa na hili wala lile huku kando yangu kukiwa na watu wengine wakiendelea na shughuli za ng'olezi(wakulima wa mpunga najua wanajua) nikawa nasikia sauti, sikujua kabisa ile sauti na ya nini, lakini kiasi inafanana na sauti ya paka mtoto aliyebanwa mahali.
Kadiri nilipokuwa namsogelea, ndipo ile sauti ilizidi, sikuwa najua masikini ya Mungu. Mpaka kuja kushtuka, nilishamkaribia sana, yaani nilikimbia umbali wa karibu mita 100, kuelekea mahali walipo watu ili kuomba msaada, mwili unatetemeka sana, kumbuka nilikuwa dogo tu. Watu walipofika kumtazama, tayari alishaondoka. Yaani picha inanijia kabisa, hakuwa mrefu ni kiasi cha rula zile tunazotumia shule kupigia mistari kwenye daftari. Dah, Mungu ni mwema na wallah! leo nimekumbuka kwakweli tukio zima. Ile sauti inanijia na nakumbuka tukio zima. Tumboni kama ana unjano fulani hivi, ila mgongoni ana vijibaka.
 
Puff adder bite
puff adder bite.jpg
 
K

Kama hakufa au kupata ulemavu wa kudumu shukuru mungu.
Yeah tunashukuru alimuuma pindi ana umri wa miaka minne now ana 11 ni mzima wa afya kabisa mungu ni mwema
 
Mkuu huyo nyoka na mjua vizuri sana nimesoma uko tabora boys wapo wengi tu akisikia binadam anajongea sehem alipo hua anafoka kukujulisha nipo maeneo haya so usimzuru na unaweza pishana nae bila tatizo lolote.sisi tulikua tukiona ana vuka barabara tuna mchezea kwa kumvuta nyuma alipo toka anaishia kufoka tu ila hiyo mashine nyingine ilishawahi kuzingua watu makabulini akuna aliye baki nahisi ata marehem asinge kua ndani ya jeneza angekimbia
teh teh teh teh we jamaa duh asee!
 
Huyu tembea yake huwa kama kinyonga tatizo usije mkanyaga, ila niliwahi ona akitoka mbio kuliko koboko tulipokuwa tunachoma rundo la majani kumbe alikuwemo, alitoka speed kali utadhani msafara wa magu vijijini, halafu kinyonga nae huwa maringo nishakuta kinyonga akienda speed ya mjusi akikimbia moto uliokuwa unachoma msitu,
teh teh teh teh teh mkuu kwann umesema msafara wa magu vijijin
 
Wana zindiko 1 la nyumba lile kiboko, kama mwanga akisogelea anakita nyumba imezungukwa na ziwa, watu asubuhi wanapita kwenda mashambani, wanakuta mtu anapiga mbizi kwenye majani au matuta, hawa jamaa ni kiboko aisee wana watu wao wanazindika wachawi kwamba akirudi tu anakufa wenyewe wanawaita kamchape
mktuu namm hao nawapata furesh
 
Hivi nyoka anaeitwa "Moma" ndio koboko? Maana hata huyo kifutu sehemu nyingine wanamwita "Kipili"
 
Asee....mkuu umezidi kuniogopesha na huyu nyoka!

So ndo hakupatikana hadi leo?

Huwa wanaishi miaka mingapi?
Sjajua anaweza kuishi miaka mingapi?

Ila sjawahi kuskia habar ya kupatkana kwake mpk Leo hii
 
Sasa hebu ngoja niwape kisa kimoja kimchompata mtoto wa mganga wa jadi kule tabora

Katika msako wa Koboko kwa njia ya mtego wa bangi ajili ya shughuri za kawaida za matibabu ya uganga wa jadi alzokua akifanya baba ake.
 
Sasa hebu ngoja niwape kisa kimoja kimchompata mtoto wa mganga wa jadi kule tabora

Katika msako wa Koboko kwa njia ya mtego wa bangi ajili ya shughuri za kawaida za matibabu ya uganga wa jadi alzokua akifanya baba ake.
Kiweke hapa mkuu nakisubiria
 
Naskia!
Anapenda sana harufu ya moshi wa bangi au sigara ya nyota

Penye mazingira hayo, Mara nyingi utamkuta.

Wawindaji wa hawa nyoka, huchoma bangi kwenye karai.

Kisha hukaa kwa mbali penye mwinuko kuangalia atakapotokea.
Duh ....itakuwa inamfanya anakuwa aggressive huyoo...

Huyu atakuwa anakula bangi mbichi huko vichakani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom