Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Black mamba is the fastest snake in the world, inasemekana huyo koboko ana sumu kali zaidi, pia ndo nyoka anaeongoza kwa kuua watu duniani, ila huyu nyoka anapatikana afrika, anaua ndani ya dakika 20 tu.

HATARI SANA:

Wanasema asilimia kubwa ya nyoka hawana sumu, ila kwa kuwa watu hatuna utaalamu wa kufahamu ni yupi mwenye sumu na asie nayo bora kukaa nao mbali.. ila nyoka yeyote bwana sina urafiki nae, nawaogopa mbaya nikimuona mwili unasisimka, hata kumuua nampiga kwa nguvu zote pigo moja tu nahakikisha anakufa
 
BLACK MAMBA

Black mamba (koboko) aliefikia ukubwa huu ni hatari sana. Huyu ni territorial snake. Ukiingia katika eneo ambalo ni territory yake anakufata kukushambulia! Ni kati ya nyoka wachache wenye kushambulia (aggressive) na wenye kuogopwa sana. Hata wachezea nyoka hawapendi kuwatumia aina hii ya nyoka kutokana sumu kali waliyonayo na uharaka wa ushambuliaji na pia wanadai nyoka huyu mwenye hasira na sumu kali hua anakufa akifugwa kutokana na kudhuriwa na sumu na hasira zake mwenyewe (japo hilo sijathibitisha).
Maranyingi anaweza kutembea huku robo tatu ya mwili wake pamoja na kichwa vikiwa juu huku akienda kushoto ama kulia kwa kasi. Watu wenye imani za nyoka wanasema nyoka wote wenye mwendo wa namna hiyo wana asili ya kijini(pia siwezi kuthibitisha hilo) Inashauriwa unapokutana nae porini uso kwa uso usimame kimya ataondoka kwani pia ana aibu. Lakini ukijaribu kukimbia na ulikua karibu nae atakukimbiza na atakugonga, tena si mara moja nakisha kwa speed ya ajabu atakimbia!
Mimi naamini kama nyoka huyu angekua anapatikana bara la Ulaya au Amerika ya kaskazini angefanyiwa promo kubwa sana kama kiumbe wa aina yake lakini huku kwetu tunaona kama ni viumbe ambao inabidi wafutike duniani! Nakumbuka Nyalandu akiwa Waziri wa Maliasili aliwahi kupeleka kikosi cha askari wa wanyama pori wilayani Urambo ambapo nyoka hao wapo kwa wingi ili wakawauwe! Japo ni vizuri na ni haki kulinda maisha ya binadamu, lengo isiwe kufanya distinction ya hii species ya nyoka, wangefanya namna ya kuwa reserve katika maeneo maalum kama ilivo kwa wanyama wengine wakali. Ni nyoka mwenye simulizi nyingi za kusisimua kuliko nyoka wengi
-
 
Sasa wanaua watu hivyo bora wauliwe tu. Yani mm nikutane na nyoka uso kwa uso kisha nisimame eti ana aibu, thubutu kama ni kunigonga atajijua mwenyewe huko mie nakula zangu mbio kumtoroka.
 
Hahahaa Mkuu, huna mbio za kumshinda labda kati yenu kuwe na distance kubwa kidogo
 
Anaitwa Mamba mweusi wa Africa
The African Black Mamba! (KOBOKO)
Anapatikana katika Bara la Africa tu. Ndie nyoka hatari kabisa! Anatoa sumu aina mbili na zote ni noooma! Anatoa sumu inayojulikana kama "Neurotoxin hii huathiri mfumo wa neva, na pia anatoa sumu nyingine aina ya Cardiotoxin hii hushambulia mfumo wa moyo. Nyoka huyu akikuuma unaweza kufa ndani ya dakika 20!

Black Mamba ni nyoka mkorofi, katili anasumu kali, anasifa ya urefu kama unavyomuona anafika hadi miguu 14 kwa hesabu za kiswahili! Ye huwa hana mwili mkubwa kama kina Python(Chatu) Mungu ni fundi sana huwa hakosei! Huyu nyoka ana roho mbaya sana kwanza amejaaliwa mbio kuliko nyoka wote! Ukikutana nae kuna ishara kuu mbili atakuonyesha kuwa Mimi African Black Mamba... Nyoka niliye jaaliwa sumu kali kuliko nyoka wote!

Ulaya hayupo huyu lkn Wazungu wanamtambua vema wakitaka kuja Afrika kuna viumbe kwanza wanaambiwa mkifika huko mnapaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu na viumbe hivi hatari.. Ktk list huyu nae yumo! So ukipata bahati yakukutana nae kwanza atakutisha! Ata achama kinywa ama mdomo wake wenye rangi nyeusi kwa ndani! Kinywa chake ni cheusi kwa ndani na ndio kimefanya aitwe Black Mamba!

Pili utamsikia anatoa sauti kama msela anaita demu! Au kama tairi linalotoa upepo, Tatu utamuona anatanua shingo yake japo c kama ya Cobra!!! Hapo ujue uko mbele ya nyoka hatari kabisa! Uzidishe maombi! Vitu viwili usijethubutu kuvifanya!

Moja uskimbie, Maana huyu nyoka ana mbio zaidi ya Husein Bolt! Mamba anakimbia Maili 12 kwa saa... Na akikukimbiza hakubali hadi akugonge sehemu ya mwili wako. Ye ardhini huwa anateleza! Na ukimkimbia ni lazima tuu atakuunganishia! Na hatakukosa!

Pili kuna wale watu akiona tu nyoka ye anakimbilia fimbo au jiwe. Siku ukikutana na nyoka huyu jua umekwisha! Wataalam wanakwambia nyoka huyu hapigwi! Kwani hata hilo jiwe huenda usiwahi kulirusha au mfe wote! Kwani Black Mamba anasifika kwa Show za kikatili anashambulia vibaya sana! Ndio maana nilisema Mungu nifundi!

Pamoja na kumuumba nyoka huyu na Sumu kali mbio nyingi, hasira na urefu lkn hapo hapo nyoka huyu amejaaliwa huruma ndani yake ukikutana nae akianza kukuonyesha sarakasi zake kuwa mimi ndie nyoka hatari nawe Binaadam ukijishusha usikimbie wala usitupe jiwe ubaki unamuangalia tuu macho kwa macho! Unaambiwa atatuliza mzuka! Na wala hatakugusa ataingia zake mitini! Unaona Muumba alivyo wa ajabu!!

Mamba anataga mayai kama kuku tu kiota chake huwa ardhini. Jike anataga mayai 10-25 akishataga mayai yake huwa yanajiengua yenyewe tu baada ya miezi mitatu. Joto ni muhimu kwa ajili ya lncubation. na vitoto vyake vikisha jitotoa unaambiwa vinaanza mishe saa hiyo hiyo hujitegemea kwa kila kitu! Na vinakuwa na sumu kali kama Mama yao tu yaani haina kuremba!

Nyoka huyu anaishi hadi miaka 11 porini. Akiwa anafugwa anaweza kuishi hadi miaka 12. Mi nilishawahi muona huyu nyoka michezo aliyotuonyesha imenifanya nisitamani kukutana nae tena! Japo nawapenda wanyama na wadudu ila sio kwa black mamba.

Tahadhali kwenu madereva mnaoingia porini kuchimba dawa kiumbe hiki ni hatari sana! Usiombe kukutana nae.
IMG-20180410-WA0022.jpg
 
Tahadhali kwenu madereva mnaoingia porini kuchimba dawa kiumbe hiki ni hatari sana! Usiombe kukutana nae.View attachment 740150
Duuu boss mlijiokoa vipi kutoka kwenye 18 zake?
 
Kuna sehemu nipo huku mkoani Tabora sehemu nilikuwa nimekaa nikasikia watu wakimsimulia nyoka aina ya koboko ambaye inasemekana anapatikana Tabora ,Shinyanga,Singida na Kigoma.

Kuna mtu mmoja katika mazungumzo yake alikuwa akisema ni bora ukutane na simba au chui unaweza ukapona kuliko koboko. Nilipojaribu kumuuliza alisema hayupo tayari kumuongelea kiundani wala kumtaja kwasababu ukiwa ndani ya mkoa wa Tabora au Shinyanga ni marufuku kumtaja huyu nyoka jinsi alivyoniambia.

Sasa kwa wale wanaomfahamu hebu tuelezeeeni kwanini koboko anaogopeka kuliko simba au chui?

Black-Mamba-3.jpg

-----

Pia soma...
 
Ni nyoka wenye sumu kubwa sana,mfano tuu black mamba ambaye huku ndio tunamwita koboko anauwezo wa kukugonga mara 120 bila kuchoka wala kupunguza kiwango cha sumu anayotema kila anapokugonga,sumu ambayo inakwenda kuharibu neva za fahamu,pia chembe za kugandisha damu ili usitoke kwenye jeraha yaani platelets huwa haziwezi zuia damu isiache kutoka,na pia huathiri mfumo mzima wa damu,ni nyoka hatari sana,
 
Jamaaa wameniambia huyo nyoka huku watu hawapendagi kumuongelea wala kumtajaa ila hawajanielezea kwanini
Ni balaa hicho kifaa kinaweza kuua watu mia in 5min acha tu,huku kwetu ushirombo ndo vipo,kuna siku nimekutana nacho kinavuka barabara ya vumbi,nikasimama nikarudi nyuma na corola yangu nikakipitia shaaaaaah kumbe sikukigonga kikanasa chini ya gari,bahati nzuri nilikua naenda mwendo mrefu,kufika lami nikaona kitu kimeanguka kwa nyuma dah nikashukuru sana,nikawaza ni vp ninheenda nacho home?
 
Back
Top Bottom