Koboko (Black Mamba) - Nyoka hatari zaidi duniani

Ila Pia Koboko aka Black mamba Anakimbizwa mpaka ana panda Kwenye mti,Anakimbizwa na Nguchiro,hawa ambao hats hapa Dar wapo,mi ninao
Google andika Fight Mangroves Vs Black mamba.
Namjua vizuri sana huyu kiumbe
Ukiangalia post za nyuma utaona nilichoandika
Ila hii imenishangaza ya koboko kumshangaa panya
Sio kawaida yake kwani ni mkorofi sana na mshari
 
Huyu nyoka bhana usitake kusikia tu maelezo yake ni balaa ,hata kama ulikuwa hujawahi kumwona ila siku ukimuona tu bila hata kuambiwa ndio koboko huyu we mwenyewe utakubali tu jeuri yake aliyonayo
 
Hapana mkuu umechanganya kidogo, huyu koboko ni puff adder kama sijakosea huwa ni mfupi na mnene. Black mamba ni mrefu na mwembamba ndie huwa anaitwa kiss of death
Kiss of death Ni pale anapokugonga au bites na Ni nyoka yeyote anaweza kukupatia hiyo kiss of death lakini sasa most of kiss of death literally zinakuwani dry bite ambazo hazina sumu Seema Ni shock huwa zinawauwa watu wengi kwa maana sumu kwa nyoka Ni digestive enzymes na hivyo Ni ghali kutengeneza pale anapokupatia hizo dry bites ya Kwanza mpaka ya pili au tatu Ni warning stay away if you persist ndo anakupa full dose lakini kwake yeye Ni hasira kwani you are too big for him or her to it so imekuwa wastage.
 
watakuwa hawa wa kawaida hao uliokuwa unawauwa

hii kitu ni hatari kwelikweli ipo siku nilikuwa naenda kuloga sehemu nipo kwenye bodaboda hili likitu likawa linakatisha barabara tahadhari ya kwanza ni dereva bodaboda aliniambia nitulie tuli na yeye akatulia tulii kimya mpaka likakatisha kuja kumuuliza akaniambia blackmamba alikuwa anakatisha barabara angethubutu kumbugudhi maiti zetu zingeokotwa na walozi wenzangu maana hiyo ni njia ya kwenda ulozini kule uchira moshi
Haaahaaa eti kuloga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kimsingi nyoka ni viumbe ambao wamepewa jina la jumla yaani nyoka, lakini viumbe hawa wapo wa aina mbalimbali na wa majina tofauti tofauti, wapo nyoka wazuri, wapole, wakali, wanaotisha nk, kwa leo nataka niwazungumzie nyoka wawili maarufu wa kwanza ni kibisa na wa pili ni koboko (black Mamba), kimuonekano viumbe hawa wote wana rangi nzuri na za kuvutia, tofauti yao ni moja tuu wakati mmoja msatarabu mwingine ni mtata balaa na ninaposema mtata elewa mtata kweli, mwenye hasira na mkatili.
Nyoka katika makazi wamegawika sehemu mbili, wapo ambao huishi sehemu ambazo wanadamu wanafanya shughuli zao, hawa si wakali sana na sifa yao ni kwamba wanapomuona binadamu hukimbia na ukiona amekugonga ni ama umemkamkanyaga au umemshitua alipojificha na akahisi hatari, hivyo nyoka ambao huchangamana na binadamu hata wanaouma huwa si wakali.

Nyoka wa aina nyingine ni wale ambao hawataki kabisa kuchangamana na binadamu, na hata katika makazi yao binadamu wakianza kuonekana onekana nyoka hao huachana na makazi hayo, ogopa sana kukutana na nyoka wa aina hii hawa huwa hawaogopi mtu kwanza wengi wao wanambio, pili ni wakali sana na tatu yeye akikuona binadamu ndio kwanza hakimbii bali atakukimbiza, kundi hili ndio hata koboko anapatikana, nyoka hawa mbali ya ukorofi lakini wanaogopwa sana, mfano kuna nyoka anaitwa #Sawaka hata tembo akimuona anakimbia utakuwa wewe !

Asilimia kubwa ya nyoka wanaoweza kuchangamana na binadamu huuma tuu, lakini hawa wengine wapo ambao huuma na wapo ambao hurusha mate kama kinga, na wapo ambao humeza kabisa kama boss chatu.

Kwa utangulizi huo turudi sasa katika mjadala wetu !

KIBISA
Kibisa ni nyoka ambao wamejizolea umaarufu mkubwa sana, kwakuwa jina lao hutumiwa pia kuwaita wanaume ambao huwa na aibu kuwaeleza wanawake hisia zao kimapenzi, na kwanini wait we kibisa ? Jibu ni moja tuu nyoka huyu haumi hata umfanye nini ! ni nyoka asiye na madhara kabisa, mpole, mzuri na anaishi katika sehemu ambazo binadamu hufanya shughuli zake kama kilimo nk.

Unaposikia Kibisa usije fikiri ni nyoka wa aina flani ! kama alivyo chatu, cobra nk, hapana nyoka hawa wapo wa aina mbalimbali na watofauti wataalamu wa sayansi huweza kuwavainisha kwa majina yao, wapo wa kijani, wapo wa njano na weusi weusi kidogo, wapo wa rangi ya ugoro nk, kifupi ni wapole na wana sura ya kuvutia sana na rangi zao huwafanya wapendeze zaidi.

Kama ilivyo kwa nyoka wengine kibisa hula nyama hutumia wadudu wadogo wadogo kama chakula, kutokana na upole wake muda mwingi hutumia kujificha ili asionekane na maadui.

SIFA ZAKE

1. Huwa haonekani hovyo.
2. Unaweza ukaishi naye ndani kwako kwa muda na usijue yupo, ili mradi tuu uwe na mende, mijusi wadogo, panya, nk.
3.haumi wala harushi mate.
4.hupendelea kujifukia chini.
5. Pamoja kwamba haumi mkwala wake ni hatari sana, ukitutana naye ili usimdhuru haraka sana hukimbilia mwilini mwako na hujiviriga katika mguu wako kisha anatulia, kama utampiga muumie wote ! (Kama nakuona ndio kajifunga mguuni kwako unavyoutupatupa huo mguu) na wale mnaopendelea kuvaa pensi au sketi harahara akiona nafasi ndio atazidi kupanda juu, sasa sijui itakuwaje akifika mwisho huko ! sipo.....!

KWA UCHACHE HUO TUMTIZAME KIDOGO NA KOBOKO.

koboko ni nyoka mkali sana na ninaposema mkali uelewe ukali wenyewe, nyoka huyu huanza ukatili tangu anapotoka katika yai tuu, huweza kujitegemea na kupambana kuanzia hapo tuu, kiwango cha sumu anachokuwa nacho anapotoka kwenye yai ndio hicho hicho ambacho huwa nacho mama yake, hivyo chunga sana usije ukakadharau kwakuwa eti kadogo utaumia ! wakati nyoka wengine wakiuma na meno yao wakiacha walipouma hadithi hiyo haipo kwa koboko, yeye akiuma meno yake bado huwa mali yake !
Akikuuma nyoka huyu huwezi kumaliza dakika 30, sumu yake husambaa haraka na huaribu mfumo mzima wa mwili sambamba na moyo.

Koboko ana rangi nzuri sana cha ajabu mdomo wake ndani ni mweusi tii wakati viumbe wengine ndani huwa wekundu, ndio nyoka mwenye mbio sana huwezi mshinda akikutaka hata uwe na baiskeli ! mbali na kutomshinda lakini hata ukitaka kumpiga pia sahau huwezi kabisa anajua sana kukwepa, akikukimbiza akakufikia atakaa mbele yako na atasimama mbele yako kwa urefu wa kimo chako huku akikenua meno ambayo huwa na matone ya maji maji na hiyo ndio sumu yake !

Ana spidi ya kila kitu unapokuwa katika hali kama hiyo usithubutu kutaka kupambana naye, kabla hujafanya unachotaka atakuwa tayari amekuadhibu kwani yupo shapu sana na ni mwelevu pia na endapo utatia huruma sana ukadondosha na chozi koboko anaweza kukusamehe uende zako, kumbuka hii ni ikiwa hujamsumbua kabisa yaani umeshituka tuu huyu hapa !

Watu wengi hudhani nyoka huyu ana mabawa lakini ukweli ni kwamba anaweza kuruka kama warukavyo ndege lakini mwili wake ni kama nyoka wengine tuu, safari yake ya kuruka huianza awapo juu ya mti na kuruka kwake huwa si kwa umbali mrefu sana na ukiona kaanza michezo hiyo ujue kuna shambulio anataka kulifanya karibuni, au anawakimbia ndege waliomshitukia akifanya uharibifu katika viota vyao.

Nyoka huyu kama walivyo nyoka wengine naye ana sifa zake, pia ana wababe wake, pia ana namna ya kukabiliana naye ikiwa ni pamoja na namna ya kumuepuka, nitamchambua vyema katika gazeti la Mtanzania hakikisha unaendelea kujipatia nakala yako kwa kumfahamu zaidi koboko (black Mamba) na wanyama wengineo.

Ila la mwisho nawaza tuu, huyu jamaa huwa mkali na mkorofi sana ukimpigia kelele, unapokuwa msituni ukipiga mluzi tuu unamkera, sasa najiuliza kwa kelele kama zile za kariakoo ukiwatupa kumi tuu sijui itakuwaje ?
Nadhani ndani ya saa moja patakuwa kimyaa utafikiri ni usiku kwani watu wote watakuwa wamelala !
Na bendera yaweza kupepea nusu mlingoti labda miezi sita hivi.


Jioni Njema.
 
Uchambuzi mzuri sana mkuu,hivi hapa Tanzania black mamba wanapatikana hasa sehemu zipi?
 
Back
Top Bottom