Kobe wemeendaga wapi mbona utotoni tumewaona sana

Kobe wemeendaga wapi mbona utotoni tumewaona sana

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,065
Reaction score
61,402
Nakumbuka kipindi Cha kifuku/masika enzi hizi nipo shule ya msingi tulikuwa tunawaona Sana Hawa wanyama yaani kukutana naye mtaani ilikuwa ni Jambo la kawaida na hata wengine waliwabeba wakajaribu kuwafuga.

NI miaka mingi imepita Mara ghafla nashangaa sionani Tena na Kobe wa aina yoyote Nina miaka zaidi ya 7 nikikadiria sijakutana na Kobe pamoja na kufanya kazi nyingi za fielld na kutembelea maporini mengi Sasa nawauliza waungwana Nini kimesibu?
 
Dar utawaonea wapi? Rudi shamba ulikokulia bado wapo.
 
Nakumbuka kipindi Cha kifuku/masika enzi hizi nipo shule ya msingi tulikuwa tunawaona Sana Hawa wanyama yaani kukutana naye mtaani ilikuwa ni Jambo la kawaida na hata wengine waliwabeba wakajaribu kuwafuga..
NI miaka mingi imepita Mara ghafla nashangaa sionani Tena na Kobe wa aina yoyote Nina miaka zaidi ya 7 nikikadiria sijakutana na Kobe pamoja na kufanya kazi nyingi za fielld na kutembelea maporini mengi Sasa nawauliza waungwana Nini kimesibu?
Wapo mi ninavyoendaga kung'owa uyoga wakati wa mvua nawaona.Hata baadhi ya majimbo katoliki hasa yaliyondani ya uwigo wapo
 
Dar utawaonea wapi? Rudi shamba ulikokulia bado wapo.
Sipo dar mkuu nipo maeneo yenye maliasili nyingi Sana za wanyama between selous na ruvuma River katikati hapo..na NImesoma sekondary kaskazini Ila sikuwahi kuwaona... at least kidogo primary ndo NImewaona wengi
 
Njoo kipindi cha mvua kuanzia kidugaro , magindu , msua , kwara mpaka ruvu station aseee ni wengi sana , mkoa wa pwani !!!
 
Kobe ni nyara ya serikali
Hafugwi ovyo sahvi
We jaribu kujifugia kobe uone mziki wake mzee

Ova
Hii inchi ina visheria fulani amazing ambazo ukikaa chini na kutafakari unagundua tunaongozwa na watu wanaopenda ushirikina na ulozi.

Maana katika hali ya kawaida mimi kufuga pundamilia , pofu, ng'ombe, twiga, nyati nyumbani kwangu si ni sehemu ya utalii wa ndani na kuongeza kipato cha ndani kwani hawa wanyama wanaweza tumika kama kitoweo siku za sikukuu imagine biriani nyumbu, chipsi mbuni, pilau ya pofu, mishkaki ya swala,supu ya ngongoro za nyati, mjohoro wa utumbo wa Kudu, etc.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
... ndio hivyo Mkuu. Ndege kama tausi ni mali ya Rais; haitegemewi afugwe au amilikiwe na mtu au taasisi nyingine yeyote ndani ya Tanzania.

Na popote atakapoonekana ndani ya mipaka ya JMT anatakiwa apelekwe Ikulu as soon as possible bila kumdhuru, kumpiga picha, au kumtumia kwa namna nyingine yoyote.
 
Angalau Leo umekuwa kiakili umeleta Uzi wa maana-sio zile nyuzi zako za Chadema na CCM.
Kuna siku unaleta nyuzi mpaka mtunanadhania jamaa kapatwa na mtindio wa ubongo.
 
Unadhani kuna biashara harumu inafanyika juu ya viumbe hawa-Wachina ni janga katika hii Dunia ni kama ile.biashara ya nyama ya punda.
 
Angalau Leo umekuwa kiakili umeleta Uzi wa maana-sio zile nyuzi zako za Chadema na CCM.
Kuna siku unaleta nyuzi mpaka mtunanadhania jamaa kapatwa na mtindio wa ubongo.
Mkuu we uko dunia ya wapi...Mimi ilikuwaga zamani ndo napiga kelele za uccm na chadema baada ya kulambishwa asali nimetulia tuli..fuatilia nyuzi zangu za miezi 8 iliyopita.
 
Ni wanyama wanaoendena na uoto wa asili usiochakachuliwa mfano ardhi,mabwawa asilia,mvua nk,kwa miaka hii hivyo vitu ni mtihani.
 
Kipindi cha nyuma ukisafiri kupitia mikumi ilikuwa kawaida kuwaona mbuni,faru ila sasa hivi kuwaona hao wanyama labda wawe kwenye cage!
 
Are almost in danger to be Extinct animals. Around 2050 hawatoonekana kamwe. Tangu 2010 sijawaona tena hao viumbe
 
Nahisi wewe ulikuwa unaona wale konokono wenye nyumba mgongoni.

Kama ni kobe kweli tuombe ufafanuzi kwa yule Mheshimiwa wa trafikii
 
... ndio hivyo Mkuu. Ndege kama tausi ni mali ya Rais; haitegemewi afugwe au amilikiwe na mtu au taasisi nyingine yeyote ndani ya Tanzania.

Na popote atakapoonekana ndani ya mipaka ya JMT anatakiwa apelekwe Ikulu as soon as possible bila kumdhuru, kumpiga picha, au kumtumia kwa namna nyingine yoyote.
Hapa uliwapiga watu na kitu kizito
 
Tausi ukiamua unampata
Sema we andaa taratibu za kumfuga tu

Ova
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom