Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,998
Leo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe amezuiwa tena kuhutubia katika mkutano wa hadhara eneo la TPC kule Moshi. Huo ulitakiwa kuwa ni mkutano wa hadhara katika kuimarisha chama chake na pia kusaidia kampeni za udiwani za Kata ya Kilema ambapo uchaguzi utafanyika Novemba 4.
Kwa wale wanaofahamu watakumbuka wiki chache zilizopita Bw. Zitto alikataliwa kuhutubia kwenye Chuo Kikuu pale Jijini Dar hasa baada ya wakuu wachuo hicho kudai kuwa taratibu za kumualika zilikiukwa. Tutawaletea taarifa kwa kadiri zinavyoendelea. Inaonekana hata hivyo kuwa timu hiyo ya wapinzani wataenda kuhutubia mahali pengine...
Sijafahamu bado.. naendelea kufuatilia...
Jamani pateni sababu kwanza kabla ya kulaumu. Kama hatujaridhika na hiyo sababu basi ndio tuanze kupiga kelele.
Wakati wote shilingi ina pande mbili. Angalia kule kwa mama Mbatia jinsi tulivyomlaumu dereve wa Fuso, kumbe na yeye ni victim tu.
Hiyo tu kwamba amezuiwa leaves a lot to be desired in a country that claims to be embracing democracy wholeheartdaly! We don't expect these things to happen in our country. Wafute mfumo wa vyama vingi tujue moja kama umewashinda kustahimili. Hata hivyo ngoja tusibiri hizo sababu tuone kama zinashikika.
Kuzuiwa ni kitu cha lazima hasa kwa watu hawa wanaopanda mbegu ya chuki,
...
Huu ni uzushi ambao wapinzani hawa wanaojidai kuungana mbele ya macho ya Watanzania ,wakidhani watavuka salama na kujinyakulia wapiga kura wengi kwa chaguzi zijazo kwa kuwavunga au kwa kuvujisha siri za walioko madarakani,uzushi ambao bila ya wasiwasi wowote naamini kabisa katika mtandao wa walaji kuna waliozikwa na kuachwa kwenye mataa.
Nasema tena kwa kichwa kipana waswahili tuna methali isemayo dua ya kuku haimpati mwewe. Hawa sasa watasema na kuitisha vikao mpaka waulizane mbona fedha inayotumika kwa vikao ni nyingi na huku Muungwana amekwisha mwaga vumbi akiwaambia hizo kelele ni za mlango hazimsitui mwenye nyumba.
Kuzuiwa ni kitu cha lazima hasa kwa watu hawa wanaopanda mbegu ya chuki,Tanzania ninchi ya amani na utulivu,lakini nia na lengo la watu hawa ni kujenga fitina baina ya wananchi na uongozi,kitu ambacho mizizi yake ikishika na kuota basi mjue kuwa mwisho wake itachanua na Tz ya jana na leo itakuwa kumbukumbu tu,nikikatisha maneno itakuwa hapatawaliki,na hakuna serikali itakayokaa madarakani ikaongoza ,mambo yatakuwa haya haya au zaidi ya haya ya kupandikiziana chuki,amani tuliyonayo itapotea kabisa na kurudi kwake itakuwa kwa mbinde,nasema watu hawa kama wana ushahidi wa uhakika kwa nini wasifungue kesi mahakamani,sababu wanayo sheria zipo,leo kupita Tanzania nzima kueneza sumu ambayo hata wao wakiachiwa madaraka basi wasifikirie kuwa sumu wanayoipanda itakuwa imekuwa diluted kwa kuwepo kwao kwenye ngazi za uongozi,huko itakuwa kujidanganya na kutudanganya,haya mambo hayafai kuzungumzwa na kukaa kama makonda wanaopiga debe safari za mabasi wataishia kupigana wenyewe kwa wenyewe wakati abiria yuko ndani ya basi.
Huu ni uzushi ambao wapinzani hawa wanaojidai kuungana mbele ya macho ya Watanzania ,wakidhani watavuka salama na kujinyakulia wapiga kura wengi kwa chaguzi zijazo kwa kuwavunga au kwa kuvujisha siri za walioko madarakani,uzushi ambao bila ya wasiwasi wowote naamini kabisa katika mtandao wa walaji kuna waliozikwa na kuachwa kwenye mataa.
Nasema tena kwa kichwa kipana waswahili tuna methali isemayo dua ya kuku haimpati mwewe.
Hawa sasa watasema na kuitisha vikao mpaka waulizane mbona fedha inayotumika kwa vikao ni nyingi na huku Muungwana amekwisha mwaga vumbi akiwaambia hizo kelele ni za mlango hazimsitui mwenye nyumba.
Kitila,
Najua TZ bado tuko nyuma katika haya mapambano ya demokrasia, ingawaje sasa ni nafuu sana kuliko enzi za Mkapa wakati akina Mrema walikuwa wanapigwa mabomu ya machozi kila siku, na watu kuuawa kule Zanzibar.