KLH News Alert:: Zitto Azuiwa Kuhutubia Moshi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Leo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe amezuiwa tena kuhutubia katika mkutano wa hadhara eneo la TPC kule Moshi. Huo ulitakiwa kuwa ni mkutano wa hadhara katika kuimarisha chama chake na pia kusaidia kampeni za udiwani za Kata ya Kilema ambapo uchaguzi utafanyika Novemba 4.

Kwa wale wanaofahamu watakumbuka wiki chache zilizopita Bw. Zitto alikataliwa kuhutubia kwenye Chuo Kikuu pale Jijini Dar hasa baada ya wakuu wachuo hicho kudai kuwa taratibu za kumualika zilikiukwa. Tutawaletea taarifa kwa kadiri zinavyoendelea. Inaonekana hata hivyo kuwa timu hiyo ya wapinzani wataenda kuhutubia mahali pengine...
 
Kuna watu hapa kila siku wanapondea kuwa kina Zitto hawaendi mikoani wakati mizengwe huko (ambayo hairipotiwi ni kibao).

Mkjj, tuhabarishe zaidi ukipata habari kuhusu hili!
 
Duh,mwaka huu kuna mengi,ila najua Moshi huko Kilimanjaro upinzania itachukua tu,hata kama Zitto atazuiwa kuhutubia.
 
Ndiyo kwa sababu kuna kiti cha Udiwani cha kata ya Kilema kinachogombaniwa. Na nadhani CCM haitaki kukipoteza kiti hicho.
 
Leo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Mhe. Zitto Kabwe amezuiwa tena kuhutubia katika mkutano wa hadhara eneo la TPC kule Moshi. Huo ulitakiwa kuwa ni mkutano wa hadhara katika kuimarisha chama chake na pia kusaidia kampeni za udiwani za Kata ya Kilema ambapo uchaguzi utafanyika Novemba 4.

Kwa wale wanaofahamu watakumbuka wiki chache zilizopita Bw. Zitto alikataliwa kuhutubia kwenye Chuo Kikuu pale Jijini Dar hasa baada ya wakuu wachuo hicho kudai kuwa taratibu za kumualika zilikiukwa. Tutawaletea taarifa kwa kadiri zinavyoendelea. Inaonekana hata hivyo kuwa timu hiyo ya wapinzani wataenda kuhutubia mahali pengine...

Hii ni aibu kwa Serikali ya CCM kumzuia Mbunge kuhutubia kwenye mikutano ya hadhara. Wanaogopa nini?
 
Jamani pateni sababu kwanza kabla ya kulaumu. Kama hatujaridhika na hiyo sababu basi ndio tuanze kupiga kelele.

Wakati wote shilingi ina pande mbili. Angalia kule kwa mama Mbatia jinsi tulivyomlaumu dereve wa Fuso, kumbe na yeye ni victim tu.
 
Sifikiri kuna sababu ya msingi hapa ni ujinga tu wa hawa watu wa Serikali ya CCM. Mnaweza kutuambia leo hii ni mbunge gani wa CCM aliyewahi kuzuiwa kuhutubia kwenye mkutano wa hadhara. Acheni mambo ya uchama hapa na angalieni picha kubwa Utanzania. Kama usipokuwa na chama tawala kila kitu kinakuwa kigumu kwa nini? Je wanaopenda kuwania kama watu binafsi itakuwaje ikiwa vyama vingine vinazuiwa?
 
Sijui kule kwa warombo vipi maanake nasikia upinzani kidogo kule umetekwa.Moshi mjini CCM hawapawezi hata kidogo kule ni maji ya shingo ila wanasiasa wakali zaidi wanahitajika kukabiliana na CCM ya Mwaka 2010 kwani wamepania kweli kweli na wana sweat na Ndesa kwenye Ubunge.

Wacha wazuie tu lakini watoe sababu za Msingi la sivyo mambo yatabadilika.Pia kuna kata moja ya Korongoni nasikia ina shida kwenye Udiwani ila sina data za kutosha mambo yakoje
 
Jamani pateni sababu kwanza kabla ya kulaumu. Kama hatujaridhika na hiyo sababu basi ndio tuanze kupiga kelele.

Wakati wote shilingi ina pande mbili. Angalia kule kwa mama Mbatia jinsi tulivyomlaumu dereve wa Fuso, kumbe na yeye ni victim tu.

Hiyo tu kwamba amezuiwa leaves a lot to be desired in a country that claims to be embracing democracy wholeheartdaly! We don't expect these things to happen in our country. Wafute mfumo wa vyama vingi tujue moja kama umewashinda kustahimili. Hata hivyo ngoja tusibiri hizo sababu tuone kama zinashikika.
 
Habari kamili za kuzuiwa Zitto ni hizi
Leo asubuhi Mkuu wa Wilaya kamwagiza OCD kuwaandikia Chadema na kuwaagiza kusitisha mkutano wao wa kawaida kabisa kwa taratibu zote . Sababu kubwa Mkuu wa Wilaya na OCD wanasema wenye kiwanda cha TPC hawakuwa na habari na hawakupenda Zitto aungurume hapo . Hiyo ndiyo sababu pekee ambayo wame eleza hawa wakubwa .Zitto kamaliza mkutano wake sasa katika kijiji cha Mvuleni , na kumbuka huu ni mkutano baada ya kuzuiwa kule alikotakiwa kuwa. Kesho Zitto ataunguruma Mererani na naamini moto utawaka huko.

Chama chetu cha mapinduzi kinazidi kutujengea Nchi na kuendelea Demokrasia ya Nchi.

Hope and pray kwamba hawatamzuia tena kuunguma kwa washinda hoi wa Mererani ambao walikodisha ndege kuja Dar kumlaki na ambao wanamlipa mshahara baada ya kuwekewa zengwe Bungeni .
 
Kuzuiwa ni kitu cha lazima hasa kwa watu hawa wanaopanda mbegu ya chuki,Tanzania ninchi ya amani na utulivu,lakini nia na lengo la watu hawa ni kujenga fitina baina ya wananchi na uongozi,kitu ambacho mizizi yake ikishika na kuota basi mjue kuwa mwisho wake itachanua na Tz ya jana na leo itakuwa kumbukumbu tu,nikikatisha maneno itakuwa hapatawaliki,na hakuna serikali itakayokaa madarakani ikaongoza ,mambo yatakuwa haya haya au zaidi ya haya ya kupandikiziana chuki,amani tuliyonayo itapotea kabisa na kurudi kwake itakuwa kwa mbinde,nasema watu hawa kama wana ushahidi wa uhakika kwa nini wasifungue kesi mahakamani,sababu wanayo sheria zipo,leo kupita Tanzania nzima kueneza sumu ambayo hata wao wakiachiwa madaraka basi wasifikirie kuwa sumu wanayoipanda itakuwa imekuwa diluted kwa kuwepo kwao kwenye ngazi za uongozi,huko itakuwa kujidanganya na kutudanganya,haya mambo hayafai kuzungumzwa na kukaa kama makonda wanaopiga debe safari za mabasi wataishia kupigana wenyewe kwa wenyewe wakati abiria yuko ndani ya basi.
Huu ni uzushi ambao wapinzani hawa wanaojidai kuungana mbele ya macho ya Watanzania ,wakidhani watavuka salama na kujinyakulia wapiga kura wengi kwa chaguzi zijazo kwa kuwavunga au kwa kuvujisha siri za walioko madarakani,uzushi ambao bila ya wasiwasi wowote naamini kabisa katika mtandao wa walaji kuna waliozikwa na kuachwa kwenye mataa.
Nasema tena kwa kichwa kipana waswahili tuna methali isemayo dua ya kuku haimpati mwewe.
Hawa sasa watasema na kuitisha vikao mpaka waulizane mbona fedha inayotumika kwa vikao ni nyingi na huku Muungwana amekwisha mwaga vumbi akiwaambia hizo kelele ni za mlango hazimsitui mwenye nyumba.
 
Hiyo tu kwamba amezuiwa leaves a lot to be desired in a country that claims to be embracing democracy wholeheartdaly! We don't expect these things to happen in our country. Wafute mfumo wa vyama vingi tujue moja kama umewashinda kustahimili. Hata hivyo ngoja tusibiri hizo sababu tuone kama zinashikika.

Kitila,

Ninafikiri unajua hayo mambo ya watu kuzuiwa yanatokea hapa UK, wakati Tony Benn na kundi lake wanazuiwa kuandama. Au kule USA yule mama anayeandamana kwa ajili ya mwanawe aliyekufa Iraq. Of course serikali inakuwa na sababu zake.

Ni vizuri kujua sababu kabla ya ku react.

Najua TZ bado tuko nyuma katika haya mapambano ya demokrasia, ingawaje sasa ni nafuu sana kuliko enzi za Mkapa wakati akina Mrema walikuwa wanapigwa mabomu ya machozi kila siku, na watu kuuawa kule Zanzibar.
 
Kuzuiwa ni kitu cha lazima hasa kwa watu hawa wanaopanda mbegu ya chuki,

...
Huu ni uzushi ambao wapinzani hawa wanaojidai kuungana mbele ya macho ya Watanzania ,wakidhani watavuka salama na kujinyakulia wapiga kura wengi kwa chaguzi zijazo kwa kuwavunga au kwa kuvujisha siri za walioko madarakani,uzushi ambao bila ya wasiwasi wowote naamini kabisa katika mtandao wa walaji kuna waliozikwa na kuachwa kwenye mataa.

Nasema tena kwa kichwa kipana waswahili tuna methali isemayo dua ya kuku haimpati mwewe. Hawa sasa watasema na kuitisha vikao mpaka waulizane mbona fedha inayotumika kwa vikao ni nyingi na huku Muungwana amekwisha mwaga vumbi akiwaambia hizo kelele ni za mlango hazimsitui mwenye nyumba.

mhhh,

nimeanza kupenda hii character ya mwiba!

Angalia, nchi inahitaji watu kama hawa ambao ni mafisadi na wanakiri hadharani ufisadi wao huku wakinyoosha kidole cha kati!
 
Kuzuiwa ni kitu cha lazima hasa kwa watu hawa wanaopanda mbegu ya chuki,Tanzania ninchi ya amani na utulivu,lakini nia na lengo la watu hawa ni kujenga fitina baina ya wananchi na uongozi,kitu ambacho mizizi yake ikishika na kuota basi mjue kuwa mwisho wake itachanua na Tz ya jana na leo itakuwa kumbukumbu tu,nikikatisha maneno itakuwa hapatawaliki,na hakuna serikali itakayokaa madarakani ikaongoza ,mambo yatakuwa haya haya au zaidi ya haya ya kupandikiziana chuki,amani tuliyonayo itapotea kabisa na kurudi kwake itakuwa kwa mbinde,nasema watu hawa kama wana ushahidi wa uhakika kwa nini wasifungue kesi mahakamani,sababu wanayo sheria zipo,leo kupita Tanzania nzima kueneza sumu ambayo hata wao wakiachiwa madaraka basi wasifikirie kuwa sumu wanayoipanda itakuwa imekuwa diluted kwa kuwepo kwao kwenye ngazi za uongozi,huko itakuwa kujidanganya na kutudanganya,haya mambo hayafai kuzungumzwa na kukaa kama makonda wanaopiga debe safari za mabasi wataishia kupigana wenyewe kwa wenyewe wakati abiria yuko ndani ya basi.
Huu ni uzushi ambao wapinzani hawa wanaojidai kuungana mbele ya macho ya Watanzania ,wakidhani watavuka salama na kujinyakulia wapiga kura wengi kwa chaguzi zijazo kwa kuwavunga au kwa kuvujisha siri za walioko madarakani,uzushi ambao bila ya wasiwasi wowote naamini kabisa katika mtandao wa walaji kuna waliozikwa na kuachwa kwenye mataa.
Nasema tena kwa kichwa kipana waswahili tuna methali isemayo dua ya kuku haimpati mwewe.
Hawa sasa watasema na kuitisha vikao mpaka waulizane mbona fedha inayotumika kwa vikao ni nyingi na huku Muungwana amekwisha mwaga vumbi akiwaambia hizo kelele ni za mlango hazimsitui mwenye nyumba.

Mwiba,

Unaamini hayo unayoyasema?

Ni Watanzania wachache sana wakiwemo wana CCM wenyewe wanaoweza kusema mambo ni salama.

Amani na utulivu vinajengwa na uongozi bora na wala sio mtutu wa bunduki. Nchi yenye amani na utulivu, watu hawazuiwi kukutana na watu wengine.
 
Kitila,

Najua TZ bado tuko nyuma katika haya mapambano ya demokrasia, ingawaje sasa ni nafuu sana kuliko enzi za Mkapa wakati akina Mrema walikuwa wanapigwa mabomu ya machozi kila siku, na watu kuuawa kule Zanzibar.

Huyu Jk anaonekana afadhali kwa sababu alikuwa hajapewa kibano sawasawa na wapinzani na ukweli kwamba anaamini bado yupo popular. Nakwambia kwa jinsi mambo yanavyokwenda huyu bwana atakuwa tyrany kuliko Mkapa. Tazama hayo matokeo ya udiwani, umewahi kuona wapi wapinzani wanashinda viti vya udiwani kwa kiwango tunachoona. Tulizoea katika viti 100, wapinzani wanapata kimoja,sasa katika viti 3, wapinzani wanapata kiti. it is becoming serious for JK and good for the country and I am afraid this could be the beginning of JK' tyranny. However, I like your optimisim and hate my pessimism!
 
Pole sana bwama Mwiba maana naona mwishowe utajichoma . Hapa walikuja Wachambuzi nk lakini waliondoka bila ya kuaga . Natumaini hutakuwa mmoja wao kuweka rekodi hapa . Madai yako yamenifanya nikushushe kabisa maana arguement yako inashindwa na uwezo wa yule kijana wa Ukwere aliyempiga Waziri Mkuu swali.

Je unayajua haya yafuatayo?
Unajua kwamba kesi ya jinai kwa sheria zetu inaendeshwa na Serikali ? Unaujua ugumu wa kuwa na private investigater na prosecutor ? Je ulikuwa wapi wakati wa kesi ya Edmond Mjengwa na kesi ya wizi ? Je unajua yaliyo wakuta wale walio fungua kesi dhidi ya Chitalilo wa CCM yenu ?

Watu waliomba serikali kumfungulia Mbunge Mjengwa kesi ili wawe mashahidi Serikali ikawa Bubu kama sasa hivi.Lakini one day waliamua kufungua kesi na ikaingia Mahakani ndipo DPP mwenye mamlaka makubwa alisema kesi sasa itaendeshwa na serikali kwa mujibu wa sheria zetu na baada ya muda DPP aliifuta kesi na ikawa mwisho wa mchezo .Je walijua hili ?

Kesi hii watu hawataki iishie kwa njia hiyo ndiyo maana wanawataja watu ili waamue kwenda Mahakamani watu wakamwage mambo. Pia kumbuka bwana Mwiba kwamba katika historia ya Tanzania tumekuwa na Majaji jasiri wachache sana wa kuweza kuamua uhalali . Mahakamani ni chaka kubwa la kumaliza mambo na kuwasafisha CCM . Wapinzani mahakamani kesi itatupwa kama wanavyo fanya then mtajenga hoja nzito ya uzushi kama unavyo anza kuzusha .

Nimekusaidia kuelewa tu kwamba Nchi ya utawala bora shutuma na tuhuma nzito kama hizi watu hawaimbi amani na utulivu bali JK was supposed to react and act . So far he has done nothing .Au ndiyo kakutuma uje kuimba hapa ?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom