Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 40,000
......Mahojiano yangu hayo na Mhe. Anne Kilango Malecela (CCM - Same Mashariki) yatarushwa siku ya Ijumaa kupitia KLH News International na pia tunatarajia yataweza kusomwa kwenye mojawapo ya magazeti ambayo yamekubali kutupa nafasi.
Mimi niko impressed na watu mara chache sana.. this is one of those times.
MKJJ....cheki PM yako
"Tulikokuwa tunaenda siko, tumeamua kugeuka"
Nadhani moja ya maswali uliomuuliza mama AKM ni hili; Tanzania ya JSM ingekuwaje na yeye kama "First Lady"?
Je maneno haya ni dhati au ya wale ambao hawakupata kipande cha keki?
kama ni ya ambao hawakupata kipande cha keki inafanya tofauti gani?
Kuna tofauti. Kama ni ya wale waliokosa kipande cha keki, akishapatiwa wanakaa kimya ,kwa mfano, Mzee wa mabomu alipopata mkopo kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa.
Tunachohitaji ni dhamira za dhati na uchungu wa kweli katika kutetea maslahi ya nchi hii.
hiyo dhamira ya dhati unaipima vipi? kuna wengine hawana hicho kipande cha keki lakini bado wamekaa kimya tu wakisubiria zamu yao kufika.
Mama Malecela anafanya kazi yake bila kujali kuwa JK anaweza kufanya uteuzi muda wowote. NI uzembe kusema kuwa kwa vile mzee wa mabomu alitulia basi wote watatulia wakipata keki.
Time will tell. Nadhani tulipe muda hili, tutakuja kujua upande upi wa ukuta alioko huyu mama.
Kwa kuongeza tu, nakubaliana na wewe, jitihada anazoonyesha ni mwanzo mzuri "regardless of" dhamira yake.
Naona unataka kuwa sheikh yahya hapa kwa kusoma nyota na future za watu.
Hiyo dhamira ya mama Malecela wewe umeijua na umeipima vipi?