KLH Exclusive:Mhe Anne Kilango Malecela Alonga!

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
"Tulikokuwa tunaenda siko, tumeamua kugeuka" - hayo ni baadhi ya maneno ya Mhe. Anne Kilango Malecela akizungumza na KLH News siku chache zilizopita akielezea mabadiliko ya wabunge wa CCM linapokuja suala la kulinda maslahi ya Taifa.

Kati ya mambo ambayo anayazungumzia ni pamoja na hali ya kisiasa nchini, kifo cha Ballali, kwanini wabunge wa CCM walikuwa wanaitetea serikali yao hata ilipokuwa inaharibu, kwanini anaamini Kikwete ni kweli anataka mabadiliko na masuala mengine kemkem.

Mahojiano yangu hayo na Mhe. Anne Kilango Malecela (CCM - Same Mashariki) yatarushwa siku ya Ijumaa kupitia KLH News International na pia tunatarajia yataweza kusomwa kwenye mojawapo ya magazeti ambayo yamekubali kutupa nafasi.

Mimi niko impressed na watu mara chache sana.. this is one of those times.
 
......Mahojiano yangu hayo na Mhe. Anne Kilango Malecela (CCM - Same Mashariki) yatarushwa siku ya Ijumaa kupitia KLH News International na pia tunatarajia yataweza kusomwa kwenye mojawapo ya magazeti ambayo yamekubali kutupa nafasi.

Mimi niko impressed na watu mara chache sana.. this is one of those times.

Bravo kaka Mwanakijiji, tunasubiri kwa hamu kusikiliza mahojiano yako na Mhe. Anne Kilango Malecela (Mbunge wa CCM - Same Mashariki) ili tuchambue contents na kuelewa mawazo yake yanavyooana na hatima ya nchi yetu katika hizi zama za UFISADI na WIZI ULIOKITHIRI. Mungu Ibariki Tanzania.
 
HUyu mama mm namkubali sana ni mama wa shoka anapigana kiume sana tena anawatoa kamasi wanaume wengi sana ambao kila kitu wao ni ndio mzee huyu mama kwake yeye NO anajali masirahi ya TAIFA anapigania wanyonge...tupo nae.
Watu wengi iwa tunajiuliza watu kama hawa wapiganaji kwa nn JK hawaiti kwenye balaza la mawaziri???ni watendaji wazuri sana kama Sendeka ni watu wanao lia na MAFISADI lakini JK hawaiti au hawateui kabisa kuwa mawaziri ina maana akiwateua watakuwa mwiba kwake???
 
Akiwaita kwenye baraza na wao watafungwa midomo. sii unajua kuna kiapo kuwa sitatoa siri za baraza la mawaziri. Mimi naona abaki kama alivyo aweze kuwa mwiba kwa serekali. Namkubali sana mama Malechela kwa kweli.

Mawazo yangu. Wanawake wajifunze kutoka kwake, kama wanataka huo usawa wa 50/50 mwaka 2010 basi tuanhitaji wanawake kama hao sio kubebwaaa tuu hadi wengine wanaanza kuwa na hisia kuwa wanachukuliwa na wakubwa. Kwa nini na wao wasipigane kama huyu mama? kwa nini wabebwe? halafu sioni hata cha maana wanachofanya huko bungeni
 
Mkuu Wangu MMJ,

Tupo ukurasa mmoja hapo, bravo maana sasa JF tunakaribia kuliongoza taifa kwa information, tukiendelea kama tulipo sasa basi very soon JF hatutakuwa na mpinzani kwenye national level,

Kwa sababu now we are almost there, yaani national heshima mbele mkuu! maana mpaka huyu mama kukubali kuja huku, sio mchezo mkuu Salute mkuu!
 

KLH News,JF,Dr. Slaa,Zitto Kabwe,Hamad Rashid,Tundu Lissu...na sasa Anne Kilango,Kimaro,Ole Sendeka,Mwakyembe&the Richmond Team...chachu ya mabadiliko kueleka Tanzania mpya?...well that's what I believe...
 
Bravo all Wana JamiiForums with constructive criticism, positive thinking and active roles in spearheading the changes, mchakamchaka, nina imani tutafika &Inshallah Mwenyezi Mungu atakuwa upande wetu & Tutashinda ni suala la muda tu. Naam udharimu ulishamili kwa muda na ukatamalaki lakini ni muda wa ukweli, haki na nguvu ya umma kushinda, ilikuwa ni kujidanganya tu kuwa a bunch of suckers will prevail for long, ni kuwa tu hatukuwa organised na waka-capitalise on that for so long, sasa uwezo wa kufichua taarifa na ku-share information tutautumia & tunautumia kwa makini sana zaidi ya wao wanavyofikiria na matokea yatakuwa yakushangaza sana kwao kadri muda unavyokwenda. Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika, Ushindi uko njiani.
 
Nadhani moja ya maswali uliomuuliza mama AKM ni hili; Tanzania ya JSM ingekuwaje na yeye kama "First Lady"?
 
Huyu mama ni mmoja kati ya wabunge wachache wa CCM ninaowakubali. Hongera Mwanakijiji kwa kufanya nae interview. Huyu mama anawafanya baadhi ya madokta na maprofesa yaliyojazana kule bungeni kupitia CCM kama kindergarten vile kielimu, kwa kuchanganua hoja na kusimamia maslahi ya nchi.
 
kama ni ya ambao hawakupata kipande cha keki inafanya tofauti gani?

Kuna tofauti. Kama ni ya wale waliokosa kipande cha keki, akishapatiwa wanakaa kimya ,kwa mfano, Mzee wa mabomu alipopata mkopo kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa.
Tunachohitaji ni dhamira za dhati na uchungu wa kweli katika kutetea maslahi ya nchi hii.
 
Kuna tofauti. Kama ni ya wale waliokosa kipande cha keki, akishapatiwa wanakaa kimya ,kwa mfano, Mzee wa mabomu alipopata mkopo kuanzisha kiwanda cha kusindika nyama Rukwa.
Tunachohitaji ni dhamira za dhati na uchungu wa kweli katika kutetea maslahi ya nchi hii.

hiyo dhamira ya dhati unaipima vipi? kuna wengine hawana hicho kipande cha keki lakini bado wamekaa kimya tu wakisubiria zamu yao kufika.

Mama Malecela anafanya kazi yake bila kujali kuwa JK anaweza kufanya uteuzi muda wowote. NI uzembe kusema kuwa kwa vile mzee wa mabomu alitulia basi wote watatulia wakipata keki.
 
hiyo dhamira ya dhati unaipima vipi? kuna wengine hawana hicho kipande cha keki lakini bado wamekaa kimya tu wakisubiria zamu yao kufika.

Mama Malecela anafanya kazi yake bila kujali kuwa JK anaweza kufanya uteuzi muda wowote. NI uzembe kusema kuwa kwa vile mzee wa mabomu alitulia basi wote watatulia wakipata keki.

Time will tell. Nadhani tulipe muda hili, tutakuja kujua upande upi wa ukuta alioko huyu mama.
Kwa kuongeza tu, nakubaliana na wewe, jitihada anazoonyesha ni mwanzo mzuri "regardless of" dhamira yake.
 
Time will tell. Nadhani tulipe muda hili, tutakuja kujua upande upi wa ukuta alioko huyu mama.
Kwa kuongeza tu, nakubaliana na wewe, jitihada anazoonyesha ni mwanzo mzuri "regardless of" dhamira yake.

Naona unataka kuwa sheikh yahya hapa kwa kusoma nyota na future za watu.
Hiyo dhamira ya mama Malecela wewe umeijua na umeipima vipi?
 
Back
Top Bottom