Wabunge wa Viti Maalum waliofukuzwa CHADEMA kuongoza Kamati za kudumu za Bunge ikiwemo PAC na LAAC

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,516
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai Januari 18 amefanya utuezi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge 17, huku pia wenyeviti wa kamati hizo wakitajwa, wakiwemo baadhi ya wabunge waliofukuzwa uanachama wa Chadema.

Miongoni mwa wabunge waliotajwa ni Naghenjwa Kaboyoka aliyetetea uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Grace Tendega aliyeshinda uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

Naghenjwa na Tendega ni miongoni mwa wabunge 19 wa Chadema waliofukuzwa uanachama Novemba 27, baada ya kwenda bungeni Dodoma kuapishwa bila idhini ya chama.

Hata hivyo, wabunge hao walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho, wakisubiri kusikilizwa.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kamati hizo zinapaswa kuongozwa na wabunge wa upinzani.

Mbali na Kaboyoka, kamati ya PAC imepata makamu mwenyekiti mpya ambaye ni Mbunge wa jimbo la Vwawa (CCM), Japhet Hasunga.

Kwa upande wa LAAC, mbali na Tendega, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo akichaguliwa Seleman Zedi Mbunge wa Bukene (CCM).

Mbunge mwingine aliyetetea nafasi yake ni wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso anayeendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi kingine.

Nafasi ya umakamu imeenda kwa Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria huku nafasi ya umakamu akifanikiwa kuitetea Najma Giga.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa amechaguliwa Mbunge wa Kuteuliwa Humphrey Polepole ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.
Nafasi ya umakamu mwenyekiti imekwenda kwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abdallah Chaurembo.

Mwingine aliyefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti ni Mbunge wa Mkinga (CCM) Danstan Kitandula ambaye amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Katika uchaguzi huo, Seifa Gulamali alichaguliwa kuwa Manonga (CCM) amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk Christine Ishengoma amechakuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji huku nafasi ya umakamu ikienda kwa Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM) Athuman Maige.

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) amechaguliwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Grace Tendega huku

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Fatma Toufiq amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi huku makamu akichaguliwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk Alice Kaijage.

Kamati ya Bunge ya bajeti wamemchagua Mbunge wa Babati Vijijini (CCM) Sillo Baran huku makamu mwenyekiti akichaguliwa Mbunge wa Kilindi (CCM) Omar Kigua.

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Emmanuel Mwakasaka amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa mara nyingine huku aliyekuwa Naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu ulemavu Stella Ikupa akichaguliwa kuwa makamu.

Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma amechaguliwa Atupele Mwakibete mbunge wa Busokelo (CCM) huku umakamu mwenyekiti ukienda kwa George Malima ambaye ni Mbunge wa Mpwapwa (CCM).

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii amechaguliwa Dk Alyoce Kwezi (Kaliua-CCM) huku makamu wake akichaguliwa Dk Pius Chaya (Manyoni Mashariki-CCM).

Mussa Azan Zungu (Ilala-CCM) aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika kipindi kilichopita amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.

Katika Uchaguzi huo, wajumbe walimchagua Vicent Mbogo (Nkasi Kusini-CCM) kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika jana.

Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira huku nafasi makamu mwenyekiti ikibakia wazi baada ya wajumbe kutofanya uchaguzi.

=====
BUNGE LA TANZANIA

IDARA YA KAMATI ZA BUNGE

MATOKEO YA UCHAGUZI WA WENYEVITI NA MAKAMU WENYEVITINa.KAMATI
NAFASI
ALIYECHAGULIWA
1.​
VIWANDA,
Mwenyekiti​
Mhe. David Mwakiposa Kihenzile, Mb
BIASHARA NA
Makamu​
-
MAZINGIRA
Mwenyekiti​
2.​
KATIBA NA
Mwenyekti​
Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa,
SHERIAMb
Makamu​
Mhe. Najma Murtaza Giga, Mb
Mwenyekiti​
3.​
MAMBO YA NJE,
Mwenyekiti​
Mhe. Mussa Azan Zungu, Mb
ULINZI NA
Makamu​
Mh. Vincent Paul Mbogo, Mb
USALAMA
Mwenyekiti​
4.​
UTAWALA NA
Mwenyekiti​
Mh. Humphrey Hezron Polepole, Mb
SERIKALI ZA
Makamu​
Mhe. Abdallah Jafari Chaurembo, Mb
MITAA
Mwenyekiti​
5.​
HUDUMA NA
Mwenyekiti​
Mhe. Stanslaus Haroon Nyongo, Mb
MAENDELEO YA
Makamu​
Mhe. Aloyce John Kamamba, Mb
JAMII
Mwenyekiti​
6.​
UWEKEZAJI WA
Mwenyekiti​
Mhe. Atupele Fredy Mwakibete, Mb
MITAJI YA UMMA
Makamu​
Mhe. George Nataly Malima, Mb
Mwenyekiti​
7.​
NISHATI NA
Mwenyekiti​
Mhe. Dunstan Luka Kitandula
MADINI
Makamu​
Mhe Seifa Khamis Gulamali, Mb
Mwenyekiti​
8.​
MIUNDOMBINU
Mwenyekiti​
Mhe. Moshi Selemani Kakoso, Mb
Makamu​
Mhe. Anne Kilango Malecela, Mb
Mwenyekiti​
9.​
ARDHI, MALIASILI
Mwenyekiti​
Mhe. Dr. Aloyce Andrew Kwezi, Mb
NA UTALII
Makamu​
Mhe. Dr. Pius Stephen Chaya, Mb
Mwenyekiti​
10.​
KILIMO, MIFUGO
Mwenyekiti​
Mhe. Dr Christine Gabriel Ishengoma,
NA MAJIMb

Na.KAMATI
NAFASI
ALIYECHAGULIWA
Makamu​
Mhe. Athuman Almasi Maige, Mb
Mwenyekiti​
11.HESABU ZA
Mwenyekiti​
Mhe. Naghenjwa L. Kaboyoka, Mb
SERIKALI
Makamu​
Mhe. Japhet N. Hasunga, Mb
Mwenyekiti​
12.HESABU ZA
Mwenyekiti​
Mhe. Grace Victor Tendega, Mb
SERIKALI ZA
Makamu​
Mhe. Selemani Jumanne Zedi, Mb
MITAA
Mwenyekiti​
13.MASUALA YA
Mwenyekiti​
Mhe. Fatma Hassan Toufiq, Mb
UKIMWI
Makamu​
Mhe. Dkt. Alice Karungi Kaijage, Mb
Mwenyekiti​
14.BAJETI
Mwenyekiti​
Mhe. Sillo Daniel Baran, Mb
Makamu​
Mhe. Omar Mohamed Kigua, Mb
Mwenyekiti​
15.HAKI, KINGA NA
Mwenyekiti​
Mhe. Emmanuel Adamson Mwakasaka,
MADARAKA YAMb
BUNGE
Makamu​
Mhe. Stela Alex Ikupa, Mb
Mwenyekiti​
16.SHERIA NDOGO
Mwenyekiti​
-
Makamu​
-
Mwenyekiti​
1611044279862.png
1611044311049.png
 
Attachments

  • File size
    92.4 KB
    Views
    6

Hakimu Mfawidhi

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
1,959
2,000
Hawa wabunge wa chadema waliojipeleka bungeni wamefundisha vyam vya siasa kua wanawake sio watu wa kuwaamini sana, lazima uwe nao makini.

Ubaya wa wanawake ni kua wao hufanya kwa kificho halafu matokeo yake yanapokuja kujulikana yanakua na athari kubwa zaidi.

Ila mimi binafsi hua sikushangaa kabisa kuhusu hao wanawake kwa waichokifanya. I am sorry lakini ukiachana na mambo ya pesa, wanawake sio watu wa kuwaamini sana.
 
Ngorunde

Platinum Member
Nov 17, 2006
2,251
2,000
CCM ni wazee wa "fitna" katika siasa za nchi hii.
Hilo ni jiwe gizani.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
4,419
2,000
Nijuavyo hao wenyeviti wa hizo kamati hupatikana kwa kupigiwa kura lakini sioni idadi ya kura walizopata, wala majina ya waliyokuwa washindani wao, wanasema tu wametetea nafasi zao, lakini hawasemi kwa njia gani, kwani huo ni utaratibu mpya?

Inawezekana hao wabunge wa Chadema kupewa uenyekiti wa hizo kamati ndio moja ya ahadi walizopewa mpaka kukisaliti chama chao na kukimbilia bungeni.

Shame.
 
Heijah

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,926
2,000
Nchi yoyote ni lazima iendeshwe kwa mujibu wa sheria kukiuka sheria au kudharau sheria ambazo mmeziweka wenyewe inaletwa taswira mbaya sana katika nchi. Kama wanaona sheria hii haifai basi wana nafasi ya kupeleka mswada na kubadili sheria ili ikidhi mahitaji hata kama ni mabaya lakini kwenda na kinyume ya sheria kwa makusudi hii sio sawa kabisa ni hatari kwa nchi. ukivunja sheria wewe leo kwa makusudi basi kesho sio nzuri.

Wakati mwingine kama sishangai sana maana tabia hizi za kuvunja sheria ziko hata barabarani, sheria zimewekwa na wenyewe ila wao wanavunja hata barabarani.

Utakuta gari ya judge kukimbia foleni wanakata upande wa pili, gari za serikali wao ndio kabisa wanavunja tu hakuna 50 wala nini na hawaguswi traffic akiona ST au sijui J hana habari nao vunja sheria sasa igiza wewe.. tabia hainzii ukubwani toka utotoni.
 
Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
388
1,000
Kaka pembe
Chadema ndo chama cha siasa kinachopendwa na watu licha ya kupora Kura kibao na kuwaingiza rais na wabunge wa ccm kwa nguvu still watu wanakipenda balaa. Angalia sugu Jana mbeya ndo utajua chadema iko damuni.

Ajira hakuna, biashara haziendi, wakulima wanalia, sector binafsi imekufa, Uhuru wa kuongea hakuna. Ccm imebaki unategemea tume na police na jeshi kubaki madarakini tu Kama bashiru alivyosema otherwise ingeshatolewa. Hata jpm analijua Hilo kuwa hakuna anayempenda.o
 
kolola

JF-Expert Member
Apr 26, 2020
2,041
2,000
Miss Zomboko kumbe na wewe ni mwandishi kanjanja. Hawa walifukuzwa na chadema halafu unaandika kuwa "wabunge wa viti maalum Chadema"... ukanjanja kutoka vyuo vya kata
Tatizo lenu mnataka aandike kama mnavyotaka. Anaandika kama hali ilivyo maana ni wabunge wa viti maalam hadi hapo itakapotangazwa na spika
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,375
2,000
Wewe msomi wa vyuo vya English medium ulitaka awaite wa chama gani ikiwa akina Silinde, Waitara ambao ni wanachama halali wa ccm lakini wapo wengine ambao bado hudai ni zao la chadema.

Usilete mizuka kuonekana wewe ni die hard wa chama Fulani. Learn to be dynamic

Sio wabunge wa cdm fullstop.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,864
2,000
Viti maalum upendekezwa na Chama cha Siasa bila shaka..CCM wao walipendekeza Viti maalum..Je,CHADEMA walipendekeza Viti maalum?
 
boomgate

Member
Jan 15, 2021
65
125
Yani hapo pote ni kutengeneza mazingira ili tupate hela za mabeberu?, daaah wakati mwingine siasa za tanzania ni kama sinema
 
Lwamadovela

JF-Expert Member
Mar 5, 2019
281
250
Amaa kwa hakika hakuna mkate mgumu mbele ya chai.najua kwa ufahamu mdogo wa Chagadema hamjanielewa bado😂😂😂😂😂
 
Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
11,114
2,000
Spika wa Bunge, Job Ndugai Januari 18 amefanya utuezi wa wajumbe wa Kamati za Kudumu za Bunge 17, huku pia wenyeviti wa kamati hizo wakitajwa, wakiwemo baadhi ya wabunge waliofukuzwa uanachama wa Chadema.

Miongoni mwa wabunge waliotajwa ni Naghenjwa Kaboyoka aliyetetea uenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) na Grace Tendega aliyeshinda uenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge la ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC).

Naghenjwa na Tendega ni miongoni mwa wabunge 19 wa Chadema waliofukuzwa uanachama Novemba 27, baada ya kwenda bungeni Dodoma kuapishwa bila idhini ya chama.

Hata hivyo, wabunge hao walikata rufaa Baraza Kuu la chama hicho, wakisubiri kusikilizwa.
Kwa mujibu wa kanuni za Bunge kamati hizo zinapaswa kuongozwa na wabunge wa upinzani.

Mbali na Kaboyoka, kamati ya PAC imepata makamu mwenyekiti mpya ambaye ni Mbunge wa jimbo la Vwawa (CCM), Japhet Hasunga.

Kwa upande wa LAAC, mbali na Tendega, makamu mwenyekiti wa kamati hiyo akichaguliwa Seleman Zedi Mbunge wa Bukene (CCM).

Mbunge mwingine aliyetetea nafasi yake ni wa Mpanda Vijijini (CCM), Moshi Kakoso anayeendelea kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi kingine.

Nafasi ya umakamu imeenda kwa Mbunge wa Same Mashariki (CCM), Anne Kilango Malecela.

Mbunge wa Rufiji (CCM), Mohamed Mchengerwa amefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria huku nafasi ya umakamu akifanikiwa kuitetea Najma Giga.

Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa amechaguliwa Mbunge wa Kuteuliwa Humphrey Polepole ambaye pia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM.
Nafasi ya umakamu mwenyekiti imekwenda kwa Mbunge wa Temeke (CCM) Abdallah Chaurembo.

Mwingine aliyefanikiwa kutetea nafasi yake ya uenyekiti ni Mbunge wa Mkinga (CCM) Danstan Kitandula ambaye amechaguliwa kwa mara nyingine kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini.

Katika uchaguzi huo, Seifa Gulamali alichaguliwa kuwa Manonga (CCM) amechaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo.

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk Christine Ishengoma amechakuliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji huku nafasi ya umakamu ikienda kwa Mbunge wa Tabora Kaskazini (CCM) Athuman Maige.

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) amechaguliwa Mbunge wa Viti Maalum (Chadema) Grace Tendega huku

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Fatma Toufiq amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Ukimwi huku makamu akichaguliwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Dk Alice Kaijage.

Kamati ya Bunge ya bajeti wamemchagua Mbunge wa Babati Vijijini (CCM) Sillo Baran huku makamu mwenyekiti akichaguliwa Mbunge wa Kilindi (CCM) Omar Kigua.

Mbunge wa Tabora Mjini (CCM) Emmanuel Mwakasaka amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya haki, Kinga na Madaraka ya Bunge kwa mara nyingine huku aliyekuwa Naibu waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu ulemavu Stella Ikupa akichaguliwa kuwa makamu.

Kamati ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma amechaguliwa Atupele Mwakibete mbunge wa Busokelo (CCM) huku umakamu mwenyekiti ukienda kwa George Malima ambaye ni Mbunge wa Mpwapwa (CCM).

Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii amechaguliwa Dk Alyoce Kwezi (Kaliua-CCM) huku makamu wake akichaguliwa Dk Pius Chaya (Manyoni Mashariki-CCM).

Mussa Azan Zungu (Ilala-CCM) aliyekuwa Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika kipindi kilichopita amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama.

Katika Uchaguzi huo, wajumbe walimchagua Vicent Mbogo (Nkasi Kusini-CCM) kuwa makamu mwenyekiti wa kamati hiyo kwenye uchaguzi uliofanyika jana.

Mbunge wa Mufindi Kusini (CCM) amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda, Biashara na Mazingira huku nafasi makamu mwenyekiti ikibakia wazi baada ya wajumbe kutofanya uchaguzi.
Muundo mbovu huo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom