KKKT lahaha kumsafisha Askofu Malasusa

KKKT lahaha kumsafisha Askofu Malasusa

MTK;
Mkuu, nimeumia sana kukusoma maneno yako haya ya kebehi; "eti mtumishi wa Mungu" na "tumechoka na mitumishi mifirauni....". Kwanza niseme, Askofu Malasusa si Askofu wangu wala hatakaa awe. Lakini, ni mtumishi wa Mungu aliye hai. Mungu ndiye aliyemwita sio watu. Uchungaji si kazi ya kuomba ajira bali ni wito. Kama Mungu aliye hai, mwenye kuogofisha hakumpiga alipokuwa anafanya maovu hayo, mimi ni nani hata nimdharau au niudharau utumishi wake? Acha Mungu amshughulikie. Sio kwamba Mungu hamuwezi au anamuogopa, HAPANA. Mungu wetu ni mvumilivu sana. Anataka toba si maangamizo.
Kwa ufupi; Kama kweli amefanya hivyo, Askofu, atubu haraka. Jina la Bwana halitatukanwa kwa ajili yake. Mungu wa Wakristo hahitaji msaada wowote. Atajitetea mwenyewe wala usimtetee

Mkuu nimeina like niliyokupa kama haijatoshaa, umenena vema sana kwa huyo aliyemtukana mtumishi wa Mungu, watukane wengine woteee hata ukiwaita MABWEGE ila siyo mtumishi wa Mungu adhabu yake ni mbaya sana
 
Hii ya Dk Malasusa inaweza kuwa moja ya habari muhimu sana wakati huu. kuibeza ni kutojitendea haki sisi wenyewe. Mkumbuke akina Malasusa na wenzake, I mean viongozi wa kiroho, ndio wanatarajiwa wawe msaada katika kuliondoa taifa katika mkwamo wa kimaadili lilipokwama. Na ni hawa ambao wanatarajiwa walisaidie taifa katika vita vya ufisadi ambalo rais mnayemshangilia hapa anaviongoza. Hii sio tuhuma ya kwanza kwa Dk Malasusa, kushambulia Mwanahalisi na Mseto haina maana yoyote zaidi ya kuwa undumilakuwili. Najua wengi wetu, hasa Wakristo, tunaangalia maandiko yanayosema "tusihukumu", "tusiwaguse wapakwa mafuta wa BWANA" nakadhalika. Lakini maandiko hayo hayo yanatutaka "tuwe wadadisi"; kwanini tusichague kuwa wadadisi? Pesa na madaraka sio tatizo kwa wanasiasa peke yao bali na kwa watumishi wa Mungu pia, tofauti ni kwamba watumishi wa Mungu wanajaribu sana kuwa wasiri zaidi lakini kwa kuwa Mungu hapendi huwaumbua tu. KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani kutoa tamko la kukanusa ni kuzidi kujichafua zaidi, maana kanisa halifanyi uzinzi bali mtu ndiye anayezini! Malasusa apambane mwenyewe kujinasua, asiliingize kanisa.
 
Back
Top Bottom