KKKT labariki unywaji wa Pombe

Hizi zisije kuwa ni jitihada za kuongeza mapato ya kodi kupitia unywaji pombe!!
 
HAPA umeivunjavunja hoja tu ila msingi wake haujauvunja.Pombe ni kilevi tu,na ipo kundi la dawa za kulevya!.Naam ni dawa ya kulevya isiyopewa kipaumbele kutokomezwa sawa na tumbaku.Kuna mtu alikunywa pombe akalewa,katika ulevi wake akakaa uchi, kuna mtoto wake aliona uchi,mzee akaishia kulaani mtoto wa mtoto wake,athari ya laana inajulikana.Sasa kwa nini pombe ishadidiwe kuwa ni nzuri ni ulevi na madhara yake yapo katika jamii?
 
Haina maana hiyo. Pombe inakupelekea hata unisaidie mbele ya wanao unapokuwa an addict to it. Nipe faida moja ya pombe mbali na kukupa calories ambazo elimination yake ni shida tupo. Hata ambao hawanywi pombe hufanya pia maasi.
Faida za pombe ni pamoja na kuburudisha, kuchangamsha na kuliwaza japo kwa mda. Historia ya pombe ianendana na historia ya binadamu ilikuwepo ipo na itaendelea kuwepo
 
nadhani mleta mada kama una shida na malasusa vile na sio unywaji pombe.
Ki vipi mkuu? Sijaelewa maana hiyo ni taarifa ya kilichotokea mkutanoni. Mimi ni KKKT pia
 
Tul
Tuliombee Kanisa na Uongozi wake na tumwache Mkuu wa Kanisa Dr Shoo aliongoze Kanisa na Dr Malasusa apumzike sasa uongozi.
 
Lakini katika Qur'an kuna ahadi kwamba Waumini watakaofaulu kuingia Akhera watakuta mito inayotiririsha maziwa na Mvinyo mzuri sana.

Au utabisha na hili?
Mvinyo huu uliotajwa katika Qur'an ni mahsusi tena ni alcoholic free. Kuna beer kama beer unayoijua wewe nchini Saudi Arabia lakini haina kilevi. Tafadhali soma tena hiyo verse na ushehereshaji wake ndiyo utapata maana halisi.
 
Timotheo 5:23

Hiyo ni mistari baadhi tuu..Ila ipo mingi tuu

Rejea Harusi ya Kana na Yesu
Otorong'ong'o ,
Kwanza ujue sina mpango wa kubadili mtu anachoamua kuamini juu ya jambo lolote. Kwangu mimi jukumu langu ni kuusema ukweli na kila mtu aamue yeye mwenyewe. katika miaka yangu yote ya kusoma maandiko hakuna mahali nimekutana na andiko likiongelea vizuri kuhusu pombe na ulevi. Hakuna!
1. Baada ya kupona na gharika Nuhu alilewa akakaa uchi
2. Ajali nyingi sana na maamuzi ya kijinga yanatokana na Pombe.

Najua argument yako ni pombe sio mbaya bali ulevi. Ulevi unatokana na kunywa pombe. Unasema kunywa kiasi si dhambi. Bahati mbaya Biblia haijasema hivyo na hakuna kipimi cha kiasi. Je Mungu akiwa anahukumu siku hiyo atatumia kipimo gani kujua nilipita "kiasi"? Kiasi ni kipi na ni kwa andiko gani? Ulevi ni dhambi iwe wa Chupa moja au nusu glasi.

Nimeomba maandiko yanayoruhusu kwa sababu ninajua hayapo. "Nabii" Tito wa posta naye alikuwa hivyo hivyo lakini pamoja na kuwa "nabii" naye alikosa andiko akaja na hilo hilo.

Tim 5:23 hairuhusu Pombe kwa maana ya Safari Lager, John Walker, Vodka au Sijui nini Wine. Inaruhusu Tomotheo kunywa Mvinyo kama sehemu ya dawa. Na leo tuna dawa nyingi tu zenye pombe ndani yake. Lakini hatunywi kujitafutia furaha humo, la Hasha! Tunakunywa kama dawa kama ilivyokuwa kwa Tim.

Hiyo ya Yesu hata sio ushahidi. Neno la Kigiriki lililotumika ni ambiguous kwa maana linaweza kumaanisha Divai au Mvinyo. Hatujui ni aina gani ya Divai Yesu alitengeneza kutoka katika mstari huu.

Kwa kuongezea tu Mungu anawazaje juu ya Pombe hebu tazama mistari hii:
Walawi 10:8-9 - "Kisha Bwana akanena na Haruni, na kumwambia, Usinywe divai wala kileo cho chote, wewe, wala wanao pamoja nawe, hapo mwingiapo ndani ya hema ya kukutania, ili kwamba msife; amri hii itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyenu;

Hesabu 6:3 - [Mnadhiri] atajitenga na divai na vileo; hatakunywa siki ya divai, wala siki ya kileo, wala asinywe maji yo yote ya zabibu, wala asile zabibu, mbichi wala zilizokauka.

Waamuzi 13:4 - [Mama yake Samsoni] Basi sasa, jihadhari, nakuomba, usinywe divai wala kileo, wala usile kitu kilicho najisi;

Isaya 5:11 - Ole wao waamkao asubuhi na mapema, wapate kufuata kileo; wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo imewaka kama moto ndani yao!

Isaya 5:22 - Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu, watu waume wenye nguvu kuchanganya vileo;

Mingine iko kwenye Biblia yako utaipitia!

Ukweli ni kwamba kitu pekee ambacho kinawafanya watu wapende Pombe ni sawa kabisa na kile kinawafanya wengine wavute sigara au madawa ya kulevya. Nacho ni kutafuta furaha na kutosheka. Mungu anaichukia Pombe kwa sababu anataka furaha na uteshelevu wetu uwe kwake. Ndio maana andiko kama alilonukuu FaizaFoxy la Waefeso 5:18 linasema tulewe Roho Mtakatifu. Kwa maana nyingine furaha yetu inapaswa kuwa ndani ya Roho Mtakatifu na ili ujazwe na Roho Mtakatifu lazima Utubu dhambi zako ikiwemo ulevi na Kuulilia msaada na msamaha alioununua Kristo katika Msalaba wa Kalvari!

Unaweza kuutete unywaji wa pombe aka ulevi kwa nguvu zote, na ni haki yako kufanya hivyo wala sitakuzuia. Ila nikualike kwa Yesu Kristo ambaye kwake kuna pumziko na raha ya moyo ambayo walevi, wavuta unga na wengineo wanaitafuta kwa gharama hata ya maisha yao.

Ukijazwa na Roho Mtakatifu hutahitaji pombe tena.

Kumbuka kila mlevi chakari alianza kidogo kidogo. Hakuna mlevi alianza na chupa kumi!

Shalom!
 
Hakuna sehemu kwenye biblia palipokatazwa pombe bali kunywa kupita kiasi( kulewa). Kama pombe ni dhambi basi kula na kuoa ni dhambi!
 
Kileo nini, tuanzie hapo kanzaaa.....
 
labda ulizidisha kiwango ila kwa vijikombe vidogo vile ambavyo hata watoto wanatumia then wewe ukalewa na kupepesuka kabisa...Inashangaza.
Alipiga kiki mbili jaza shavu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Huyo Malasusa anasema nini kuhusu Wamisionari na pombe? Angejua jinsi pombe inavyowapa wazungu kuumwa kichwa angekuja na kauli nyingine. Na huyo Mshaharakesho anasifiwa huko BKB kumbe in hambazo. Pombe uteketeza familia za watu halafu anaongea kama vile anaongelea togwa la ndizi (Olamba)? Shame on him![emoji1540]
 
Inaharibu familia za walevi sio wanywaji
 
Ngoja nikae sawa nikurudie.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…