Kizungumkuti cha ndoa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kizungumkuti cha ndoa!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Eiyer, Nov 23, 2011.

 1. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Nimejiuliza wakati napitia uzi wa Cantalisia kuhusu jamaa alietoka nduki baada ya kugundua mpenzi wake ana mawe zaidi yake.Sasa swali linakuja,kwanza wanawake wanakubali kuwa mwanaume ni kichwa cha familia?(Kuwa kichwa kuna maana ya kutolea maamuzi ya mwisho jambo lolote linalohusu familia)kama wanakubali mwanaume ni kichwa kwa tafsiri hiyo,Je mwanamke anapoolewa akakutwa na mali aliyoichuma mwenyewe hii nayo itaingia katika usimamizi na maamuzi ya mwisho ya mume?(hapa nazungumzia maamuzi chanya sio ya kufuja mali)Yaani mke hatakua tena na kauli ya mwisho na namna ya kuendesha mali hiyo kwa sababu mwanamke huyo tayari anamilikiwa na mume ama mali ya mwanamke haitamhusu mume?Jambo hili huenda ndio sababu ya ugumu wa kuoa mwanamke mwenye mali!
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,223
  Trophy Points: 280
  wanaume bwana,

  kwanini uwe na uamuzi wa mwisho?

  kwa nini msiwe na uamuzi wa pamoja? kujadiliana kwa pamoja nini cha kufanya?
  kwa nini msipange priority zenu pamoja?
  kwa nini msishirikiane kwa pamoja?

  mtabishana humuuu weeeeeeee, mtajiita vichwa aka taasisi huru weeee...
  lakini mwisho wa siku nyumba yenye mafanikio ni ile inayosikilizana na kushirikiana kwa pamoja, ambayo kila mwanandoa anaweza kujieleza kwa uhuru
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...umeyaandika yote yalokuwamo kichwani mwangu,
  ubarikiwe sana!
   
 4. la Jeneral

  la Jeneral JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ntarejea
   
 5. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  BADILI TABIA,hakuna maamuzi ya pamoja,hakuna mahali popote pasipokua na mtu mwenye kauli ya mwisho,kwenye ndoa nako hakuna tofauti,kama unakataa mwanaume asiwe na kauli ya mwisho basi uwe wewe,lakini hujategua hicho kizungungumkuti hapo!Hebu sema utamruhusu awe na kauli ya mwisho kwenye mali yako?
   
 6. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hii nimeipenda sana, mara nyingi mwanaume huwa ni kichwa cha familia. Siamini kwenye dini illa huwa nachukulia bible na quran kuwa ni life principle books au life experience books. Kwanza kwa mwanamke anayependa usawa kwa vitendo huwa wanaachika sana hakai na mwanamme mmoja hata siku moja. uzuri ni kwamba wengi wao huwa ni maneno tu ukimkuta kwake yuko chini kabisaaaaa, nina mifano mingi tu mimi ni mtu mzima. Anayelalama kutaka usawa ujue kwake mpole sana tu. Anataka mifano ya kumpa mumewe
   
 7. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Nimeipenda hii!Ni vyema wakati mwingine tukawa na uongozi unaoeleweka!
   
 8. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  mwanaume ndisho mwisho wa safari ila mwanamke anaweza kumshauri kabla ya kufanya maamuzi yoyote yale..
   
 9. daughter

  daughter JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Jun 22, 2009
  Messages: 1,274
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  BADILI TABIA ameeleza yote,asante
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe,but vipi huhusu mali za mwanamke alizochuma kabla ya kuolewa na mume,zitakuwa chini ya nani?
   
 11. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Lakini hajasema kuhusu mali alizochuma mwanamke kabla ya kuolewa zinakua chini ya nani?
   
 12. S

  Sharp Observer Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Mali hizo ukiwa peke yako unao uwezo wa kuzi-manage bila madhara. Ila ukiwa na mme wako hutaweza kwa ufanisi uleule kwa kuwa hata madaraka madogo uliyopewa ndani ya bustani ya edeni uliyatumia vibaya. Mwenyezi Mungu akakupokonya madaraka akampa mwanaume i.e ulishindwa kujiongoza kwa ufanisi
   
 13. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  So hata mali alizozitafuta mwenyewe hatakua na sauti au maamuzi nazo?
   
 14. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Katika hili mm naamin km nitakuwa na kipato kikubwa kuliko mme wangu,
  Kipato changu hakina nafasi ya kubalidi wadhifa wa mume kwenye ndoa,
  Hata nina pesa kiasi gani nilishindwa kuwa peke yangu,ndio maana nikamkubali kuolewa naye na kila kilichokuwa changu inakuwa vyetu wote km tulivyoamua kuwa mwili mmoja,
  Pamoja na kushirikishana ktk maamuzi na kila jambo bado yy atabaki kuwa mwenye maamuzi ya mwisho km baba wa familia.
   
 15. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  I like this Canta!Natamani ingekuwa hivi kwa wanawake wote!
   
 16. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  Mali mali.....!! Mali kitu gani bna kaeni nazo...............ziwe waume zenu ziwapempe na ziwazalishe watoto! ARRRRRRRRRRGHHH!
   
 17. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Ngoja wanawake wakusikie!Mie simo!
   
 18. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Asante Eiyer,
  Hope hii inakuwa kwa mtu binafsi anavyofeel ule upendo bila kujali mambo ya vipato na mali ambavyo hata vikiisha vitafautika!
   
 19. M

  Masuke JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,606
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  Kama na mimi nina mali ambazo zinatosheleza familia, nitamwacha mali zake aamue yeye mwenyewe ili mradi anazitumia vizuri lakini kama matumizi hayatakuwa mazuri lazima niingilie bila kujali alizipata kabla ya ndoa au baada ya ndoa.
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Canta,i hope so!
   
Loading...