SoC03 Kizungumkuti cha maadili nchini Tanzania

Stories of Change - 2023 Competition

Yvo

New Member
May 8, 2023
2
7
KIZUNGUMKUTI CHA MAADILI NCHINI TANZANIA.

Miaka ya hivi karibuni duniani kote na hata Tanzania, kumeshuhudiwa kuwapo Kwa suala la Kizungumkuti cha maadili na limeonekana kuwa suala mtambuka na lenye kuleta mjadala mkubwa ili tija ipatikane Kwa kuinusuru jamii yetu. Hivi sasa jamii imepoteza uasili wake wa maadili kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia Kwa kuiga tamaduni za wageni zenye ukakkasi na kuacha zao ili tu waonekane kuwa wanaenda na usasa ya kwamba dunia nini inataka, mfano mfumo wa maisha, mila ,desturi.Kizungumkuti cha maadili kinaibua Vizungumkuti vingine vingi Mfano Ushoga, Usagaji, ukuhadi, ulawiti , ubakaji na mauaji kwa wenza wa ndoa ambpo Kwa Tanzania vimeshika kasi na kuonekana ni watumwa wa Utamaduni wa kigeni kwani wahenga walisema "mkataa asili ni mtumwa".

Sababu zinazo sababisha Kizungumkuti cha maadili ni pamoja na:

Kutothamini uumbaji wa Mungu na Nasaha toka Kwa Viongozi wa dini .Endapo watanzania tusipotambua thamami ya uumbaji wa Mungu na kutokua na hofu kwake kama viongozi wa dini Maaskofu, Mapadri,Wachungaji, Mashekhe wanavyotuasa katika mahubiri yao na mawaidha katika nyumba za ibada basi Kizungumkuti hichi cha maadili kitaendelea kuwapo na kitatufuna hivyo Kila mtu anapaswa atambie Kwa Mungu anathami kubwa hivyo ajisikie fahari hivyo alivyo ndio mana kamuumba Kwa jinsi ya kike au ya kiume ,hivo mtu asipotambua thamani ya uumbaji wa Mungu nia ya kubadili maumbile au kushirirki mapenzi ya jinsia moja ataona ni kitu cha kawaida.

Wazazi au walezi kuacha wajibu wao kama kituo cha kwanza kabisa cha malezi katika familiai. Familia nyingi za kitanzania linachukulia suala la malezi kuwa ni la kawaida sana pale wazazi au walezi wanapoacha kutimiza wajibu wao wa kuwalea watoto katika maadili mema na kukaa nao pamoja mda mwingi ili kujadili maswaiba mbalimbali yanayowakumba sehemu mbalimbali mfano mashuleni ,vyuoni, majumbani au mitaani .Hii yote inatokana na wao kuwa bize na uchakarikaji wa utafutaji wa fedha ilimradi mwisho wa siku mkono uende kinywani na hii imekua Kwa Kiasi kikubwa kutokana na kupanda kwa gharama za hali ya maisha wangejua kumbe wanaangamiza kizazi kijacho.

Uaminifu uliokithiri Kwa ndugu, jamaa na marafiki wa karibu. Jamii inatakiwa kujua kuwa "kikulacho kinguoni mwako" kwani kumwamini mtu wa karibu Kwa dunia ya sasa si hoja kwani hujui ana nia gani. Kipindi hichi kumeshuhudiwa na matukio mengi ya mmonyoko wa maadili ambapo ndugu, jamaa na marafiki wa karibu ndio wafanyaji au wafundishaji wa matukio hayo mfano ubakaji, ulawiti kwa Watoto hufanywa na wajomba ,baba mazazi, binamu na kaka na familia huona aibu kuripoti katika vyombo vya dola ili viwachululie hatua na badala yake kulalamika kwamba hamna utawala bora wakati wenyewe hawakuwajibika katika nafasi yao.

Mahusiano ya kimapenzi yasiyo rasmi Kwa Vijana wa kike na kiume. Mfumo wa "sogea tukae" nchini Tanzania umekua chanzo cha kutokuwepo Kwa uaminifu miongoni mwao pia kuibua Usaliti na wivu wa kimapenzi na hii yote hupelekea ugomvi na muda mwingie hadi kufikia suala la mauaji miongoni mwao.Hii yote ni kutokana na ukosefu maadili Kwa sababu watu wanachumbiana katika mitandao ya kijamii mfano WhatsApp, Instagram au Facebook bila ya kuonana wala kujuana tabia.

Maendeleo ya Sayansi na teknolojia.Wahenga wanasema "akili za kuambiwa changanya na zako" Urahisi wa teknolojia mfano Simu janja, kompyuta, ambapo jamii hutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook,WhatsApp, Instagram, Telegram ambapo Wazungu hutumia kuenezea utamaduni wao usiofaa kupitia picha ,video, ujumbe mfupi zinazohamasisha Ushoga ,ulawiti, ubakaji, ngono zembe ambapo Tanzania watumiaji wakubwa ni Vijana ,watu wazima na watoto Kwa Kiasi kidogo wanaomiliki hivyo vifaa vya kielektroniki walivyopewa toka Kwa wazazi au walezi wao.Hivyo wengi huiga na kusababisha upotevu wa maadili.

Kutokuwepo Kwa sera, Sheria na mipango madhubuti za usimamizi juu ya suala la malezi Kwa jamii. Nchini Tanzania sera za maadili ya jamii na viongozi zitumikazo sasa zimepitwa na wakati hivyo haziendani na kasi ya dunia katika utekelezaji ,Pia Sheria zilizopo hazifanyi jamii kujutia kutokana na adhabu itakayopewa endapo itaenda kinyume na maadili.Pia viongozi wakati mwingine hawatilii mkazo suala la malezi na maadili katika majukwaa yao ya kisisasa .

Uwepo wa asasi chache za usimamizi wa maadili katika serikali na jami na ushirikishwaji mdogo wa Mashirika yasiyo ya kiserikali. Uwepo wa asasi na taasisi chache za serikali zinazosimamia maadili ya jamii pamoja na ya viongozi wa umma.Mfano Tume ya Utumishi wa umma na utawala bora,Tume ya maadili ya viongozi wa umma na Tume ya haki za binadamu ambapo katika ngazi za chini kabisa vijijini na mitaani haziwafikii wananchi ,Pia serikali kutowashirikisha Mashirika yasiyo ya kiserikali katika kazi zao na hata kuwashika mkono katika rasilimali watu na fedha.

Hivyo basi, Ili Tanzania iweze kuepukana na dubwana hili la Kizungumkuti la maadili inatakiwa kuwekeza nguvu katika malezi na maadili kuanzia katika ngazi ya familia hadi ngazi ya taifa, kufuata nasaha za viongozi wa dini na Katika vitabu vitukufu kama Biblia na Qurani Kwa kuthamini uumbaji wa Mungu na hofu juu yake, Kusambaza wataalu wa saikolojia mitaani ili kukutana na Vijana ambo ndio wimbi kubwa linaloathirika, kurekebisha na Kusimamia sera na Sheria ili ziendane na wakati na kukaribisha wadau, makampuni, Mashirika na wanaharakti na watu binafsi ili kusaidia katika kurudisha maadili na malezi ili kuleta Uwajibikaji wa wananchi Kwa serikali na kuleta utawala bora Kwa Viongozi katika kuwatumikia wananchi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom