Kiwango cha maambukizi ya Malaria chashuka kwa asilimia 50

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,053
28,245
Nampongeza JK kwa kuanzisha mchakato na nampongeza Magufuli kwa kuendeleza juhudi za kupambana na Malaria nchini.

Nawapongeza wadau wa afya kutoka nje na ndani ya nchi kwa kuusimamia na kuutekeleza mchakato.

Nawapongeza watumishi wa afya na kada nyingine kwa utendaji uliotukuka kuhakikisha malengo ya kuondoa malaria yakikaribia kufikiwa.

Nawashukuru wananchi kwauelewa juu ya madhara ya malaria na njia za kupambana nayo.

Hatimaye malaria nchini yapingu kwa kiasi cha asilimia zaidi ya 50%.
 
Pongezi kwa uongozi mzima wa serikali ya awamu ya tano kwa kulinda nguvu kazi
 
Naomba kuhamia sisiemu kuunga mkono juhudi za jiwe kupambana na malaria. Kwanza yule Dkt Mwele alikuwa anapandikiza vimelea vya malaria nchini
 
Naomba kuhamia sisiemu kuunga mkono juhudi za jiwe kupambana na malaria. Kwanza yule Dkt Mwele alikuwa anapandikiza vimelea vya malaria nchini
Dr Mwele alikuwa anapambana na neglected tropical deseases ..Malaria sio eneo lake.
 
Ni kweli malaria imepungua lakini kuna hili janga jipya linaitwa infection jamani embu mtuelimishe mbona dalili ni zile zile za malaria lakini ukipima hakuna kitu

Hili janga ni kwa wakubwa Na wadogo juzi jirani yangu mwanae ameumwa mpaka nimemuonea huruma kumbe ni infection mtoto kakaa Hosp siku nne

Wataalamu mtuelimishe hii infection ni kitu gani
 
Malaria ni Ugonjwa mbaya na hatari sana. Unaua sana kuliko ugonjwa wowote nchini ni wa kuogopwa na kufanyiwa kazi katika nguvu zote.

Kwa hii habari kama ni kweli; Pongezi sana kwa waliohusika na kama ni KIKI basi nalaani na kukemea sababu ya madhara yake ninayajua vizuri.

Watoto wengi chini ya umri wa miaka 5 na hasa waliokuwepo vijijini ambako huduma za Afya ziko chini au mbali na makazi hivyo wanakufa na kusahaulika haraka sana. Tafadhali tuendelee kufanya jitahidi zetu zote.

Mimi Mhanga wa hili.
 
Hiyo takwmi kama imetoka kwa mama chuwa fyekelea mbali wanamfurahisha jiwe wanajua ndo anachopenda kusifia tuuu
 
Kwa kweli ni jambo jema. Hasa huko Dom kuna maeneo hayana kabisaa malaria nina 3yrs hapa mimi mimi na familia yangu hatujawahi kuumwa malaria.
 
Back
Top Bottom