..Ukiacha hilo shamba la morogoro kule arusha kuna mashamba mengi tu ya wazungu maelfu kwa maelfu ya hekari yanamwagiliwa kwa kufyonza maji ya mito na chemchemi lakini kwa sababu ni wazungu hawaguswi na badala yake serikali imekuwa ikiwakingia kifua!
Kuna mto nduruma miaka ya nyuma ulikuwa ukitiririsha maji majira yote ya mwaka ila wazungu walipoanzisha mashamba yao miaka ya 90 maji karibu yote yakawa yanaishia kwenye hayo mashamba na mto umekauka kabisa, walala hoi waliokuwa wakiutegemea mto kwa umwagiliaji sasa hakuna tena maji.
Tunakoelekea na hizi siasa zetu chafu Mungu atusaidie tu