Kiwanda kipya cha sukari MOROGORO

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,000
2,000
Shamba la kiwanda kipya cha sukari Morogoro kimeruhusiwa kufanya yale yaliyokatazwa kwenye shamba la Mh. Mbowe. Kisa uharibifu wa mazingira.
Serikali ilikataza wakulima kutumia maji ya mito/maziwa kufanya umwagiliaji.

Kitu ambacho ndio kilichomponza mbowe shamba lake kuchakazwa. Sasa hiki kiwanda nacho kinampango na kipo mbioni kufyonza maji kutoka mito iliyopo karibu na shamba hilo jipya.

Hii maana yake nini?/ nashindwa kuelewa hii serikale ya CCM kwanini inaendekeza ubaguzi usio na faida zaidi ya kuleta mitafaruku na hatimaye kuumizana bila sababu.

MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,000
2,000
mashamba ya mh mbowe yamezuiwa na hatimaye yamevurgwa kisa maamuzi waliotoa mwanzo ya kumzuia asitumie maji ya mito kufanya umwagiliaji kwenye mashamba yake kwa kisingizio uharibifu wa mazingira yameshindwa. na hatimaye wameamua sasa kupitisha greda kung'oa kila likichopo shambani hapo. huu ndio serikale inaona ni uamuzi mzuri kwa akili ndogo.
halafu leo kuna kiwanda kimeanzishwa moro cha sukari na kina shmba la ukubwa wa hekta nyingi sana ambazo tayari wanaendelea na mchakato wa kunyonya/kuvuta maji ya mito kwa ajili ya umwagiliaji katika shamba hilo. hapa uharibifu wa mazingira haupo.. SHAME!!
 
Juma wa Juma

Senior Member
Jan 13, 2017
151
250
Naomba kuelimishwa hayo mashamba yapo karibu na mto kwa mitaa ambazo haziruhusiwi kisheria au wanakatazwa kwa sababu wanatumia maji ya mito????
 
MWALLA

JF-Expert Member
Dec 12, 2006
15,000
2,000
Naomba kuelimishwa hayo mashamba yapo karibu na mto kwa mitaa ambazo haziruhusiwi kisheria au wanakatazwa kwa sababu wanatumia maji ya mito????
labda uniambie ni mita ngapi kutoka mtoni ndio unaruhusiwa kutumia maji hayo
 
sir longo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
1,058
1,500
mbowe hajazuiliwa kufanya kilimo cha umwagiliaji, ila shamba lake lipo ndani ya hifadhi ya maji kisheria. sio unalalama tu humu.
 
MasterP.

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
6,643
2,000
..Ukiacha hilo shamba la morogoro kule arusha kuna mashamba mengi tu ya wazungu maelfu kwa maelfu ya hekari yanamwagiliwa kwa kufyonza maji ya mito na chemchemi lakini kwa sababu ni wazungu hawaguswi na badala yake serikali imekuwa ikiwakingia kifua!
Kuna mto nduruma miaka ya nyuma ulikuwa ukitiririsha maji majira yote ya mwaka ila wazungu walipoanzisha mashamba yao miaka ya 90 maji karibu yote yakawa yanaishia kwenye hayo mashamba na mto umekauka kabisa, walala hoi waliokuwa wakiutegemea mto kwa umwagiliaji sasa hakuna tena maji.
Tunakoelekea na hizi siasa zetu chafu Mungu atusaidie tu
 
sir longo

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
1,058
1,500
soma vizur post yangu, nmekwambia shamba lake lipo ndani ya hifadhi ya maji. na sio maji yapo ndan ya hifadh. inaonekana mgumu kuelewa na hujui unacholalamika.
 
mtanzania1989

JF-Expert Member
May 20, 2010
2,966
2,000
Kuna tofauti kati ya kulima kwenye chanzo cha maji na kulima kwa kutumia maji ya mto, Mbowe kama anaamini ameonewa aende mahakamani vingenevyo atulie tu sheria ichukue mkondo wake, yeye hayupo juu ya sheria.
 
inamankusweke

JF-Expert Member
Apr 24, 2014
6,211
2,000
..Ukiacha hilo shamba la morogoro kule arusha kuna mashamba mengi tu ya wazungu maelfu kwa maelfu ya hekari yanamwagiliwa kwa kufyonza maji ya mito na chemchemi lakini kwa sababu ni wazungu hawaguswi na badala yake serikali imekuwa ikiwakingia kifua!
Kuna mto nduruma miaka ya nyuma ulikuwa ukitiririsha maji majira yote ya mwaka ila wazungu walipoanzisha mashamba yao miaka ya 90 maji karibu yote yakawa yanaishia kwenye hayo mashamba na mto umekauka kabisa, walala hoi waliokuwa wakiutegemea mto kwa umwagiliaji sasa hakuna tena maji.
Tunakoelekea na hizi siasa zetu chafu Mungu atusaidie tu
inatakiwa shamba liwe nje ya 60m toka chanzo cha maji
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom