Kiwanda cha Super Loaf chamuomba radhi mteja aliyekuta uwazi kwenye mkate. Chaahidi kumlipa fidia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
118,316
219,591
Kiwanda cha kutengeneza mikate nchini Kenya cha Super Loaf kimemuomba radhi mteja wake Kelly Inyani aliyelalamika kukuta uwazi katikati ya mkate alionunua, jambo alilolitafsiri kama kupunjwa mkate ikilinganishwa na thamani ya fedha alizolipa.

1.jpg

Kiwanda hicho kimeahidi kumlipa fidia , japo haijafahamika ni fidia ya namna gani atakayolipwa.

Chanzo: Swahili Times
 
hahahha nimecheka sana.. Yaani huku mkate tumezoea ukinunua lazima ukute uwazi. usipoukuta unaurudisha dukani kusema mbona huu mkate hauna shimo la kupumulia? Ahsante mtoa mada kwa kutufumbua macho. Huku ukinunua mkate ukute uwazi ,urudishe unajibiwa kidhungu kwamba< Unajua maana ya respiresheni wewe au ulikimbia umande? unaondoka zako
 
Nakumbuka Kenya huwa wahusika wa ujazo wanapima mpaka mikate kuona ina ujazo sawa unaotakiwa au mlaji anapunjwa,huko TZ,nasikia wale wanaotembeza kwenye magari huwa wanapunguza slices kwenye kila mfuko ,ukifika dukani kwa mangi naye anajipunguzia.
 
Kiwanda cha kutengeneza mikate nchini Kenya cha Super loaf kimemuomba radhi mteja wake Kelly Inyani aliyelalamika kukuta uwazi katikati ya mkate alionunua , jambo alilolitafsiri kama kupunjwa mkate ikilinganishwa na thamani ya fedha alizolipa


View attachment 1797966


Kiwanda hicho kimeahidi kumlipa fidia , japo haijafahamika ni fidia ya namna gani atakayolipwa .

Chanzo : Swahili Times
Responsibility at work!
Ni matokeo ya katiba nzuri, bunge lipo huru , mahakama zipo huru
Kiwanda cha superloaf kinajua kabisa , jamaa kwenda kulalamika kwao kwanza ni uungwana angeweza kwenda mahakamani na kukidai kiwanda fidia anayotaka na kiwanda kingelipa pesa .
 
Back
Top Bottom