Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,870
- 34,357
Katika mji wa Guangzhou nchini China, kuna kiwanda kikubwa zaidi cha mbu duniani, ambacho kinazalisha mbu wa kiume zaidi ya laki 5 hadi milioni 1 kila wiki.
Mbu wote wanaozalishwa katika kiwanda hicho wanabeba kimeleo cha Wolbachia. Mbu wa kiume wa aina hiyo wakijamiiana na mbu wa kike, mbu wa kike hawataweza kuzaa tena.
Mwaka 2001, Xi Zhiyong alianza kutafiti kimeleo cha Wolbachia, na ni mtu wa kwanza kuweka kimeleo hicho katika mbu wenye virusi vya dengue na malaria.
Xi Zhiyong na timu yake hawataki kuangamiza mbu wote, na wanatakia kubadilisha mbu wanaoweza kuambukiza virusi kuwa mbu wa kawaida.
Kiwanda cha Mbu pia kinaungwa mkono na tajiri mkubwa dunia Bill Gates, ambaye alichangia dola milioni 15 za kimarekani.
Chanzo: CRI Kiswahili