Kuna Haja ya Kuwekeza Katika Kiwanda cha Kutengeneza Mabasi na Daladala

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
7,931
10,482
Barua ya Wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa CCM Taifa

Kwako, Mheshimiwa Rais Dr. Samia Suluhu Hassan,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Amiri Jeshi Mkuu,
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa,

Mpendwa Kiongozi wetu,

Nakupa salamu za heshima na taadhima nikiwa na imani kubwa na uongozi wako imara. Kwa niaba ya Watanzania wote, napenda kuchukua fursa hii kuonyesha heshima yangu kwako na kuthamini juhudi zako zisizo na kifani katika kuleta maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na kisiasa nchini. Nikifikiria mbele, ninashukuru kwa utekelezaji wa mipango ya kimkakati ambayo inaleta ustawi wa watu wetu.

Mheshimiwa Rais,

Katika barua hii ya wazi napenda kutoa wazo la kuwekeza katika kiwanda cha kuzalisha mabasi makubwa na daladala hapa nchini. Itakuwa vizuri kama kiwanda hicho kitazalisha mabasi ya aina tatu, ya kutumia gesi, umeme, na mafuta. Sekta ya usafiri nchini imekua kwa kasi kubwa sana, na tunao uwezo wa kuingiza mapato mengi kupitia uwekezaji huu. Kwa kuanzisha kiwanda cha mabasi, tutakuwa na fursa ya kufikia soko kubwa na kuongeza mapato mengi sana kwenye serikali yetu.

Mheshimiwa Rais, naomba pia kama ikiwezekana, wawekezaji wanaoshiriki katika mradi wa mwendokasi, ambao ni mradi mkubwa wa usafiri wa mabasi kuliko yote nchini, tuwavute waweze kuwekeza pia katika uzalishaji wa mabasi makubwa na daladala. Huu ni uwekezaji utakaosaidia kukuza uchumi wetu na kuboresha huduma za usafiri kwa wananchi.

Naona mapato ya bure tena mengi sana kupitia uwekezaji huu. Hii ni fursa nzuri kwa taifa letu, na ninaamini itaongeza uchumi wa taifa na kuchangia katika ustawi wa jamii nzima.

Nashukuru kwa umakini wako katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya nchi yetu. Hii ni hatua muhimu zaidi katika kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia kiwango cha juu cha maendeleo katika sekta zote muhimu.

Wako katika Ujenzi wa Taifa,
+255687746471
Asante sana

Ndugu wasomaji wa hii barua ya wazi ya ombi kwa Rais Dr. Samia Suluhu, hii ni rejea ya viwanda alivyo zindua 2024:

SAMIA-9.jpg

GNIokupXIAA3klB.jpg


SAMIA-6.jpg


Hiki ni kiwanda cha ndege:
KIHENZILE-2.jpeg

KIHENZILE-3.jpeg


KIHENZILE-1.jpeg
 
Tanzania ya viwanda ilishakufa sasa hivi tunadili na mambo mengine🐼
 
Quality Group, Pugu/Nyerere road....
1998 nilipita pale kiwandani nilipokua field
 
Ugumu upo kwenye kuwapata hao wenye mitaji kuja kuwekeza kwenye hilo wazo lako.
Inaweza kufanikiwa, iwapo timu itatumwa kwenda huko nje kwenye viwanda vya magari/mabasi, wajaribu kuwashawishi ili waweze kufungua tawi huku kwa makubaliano maalumu.​
 
Ugumu upo kwenye kuwapata hao wenye mitaji kuja kuwekeza kwenye hilo wazo lako.
Inaweza kufanikiwa, iwapo timu itatumwa kwenda huko nje kwenye viwanda vya magari/mabasi, wajaribu kuwashawishi ili waweze kufungua tawi huku kwa makubaliano maalumu.​
Ni kweli mkuu kuna kiwanda cha magari nakumbuka kilizinduliwa na Rais mwaka jana unakikumbuka. Na kuna kile cha ndege pale Morogoro.
 
Assembly workshop sio kiwanda labda km hujui maana ya kiwanda
Ahsante kwa mchango wako, lakini mkuu hata Assembly workshop nayo ni aina ya kiwanda kwa sababu inahusika na mchakato wa kukusanya na kuunganisha sehemu mbalimbali za magari hadi kupata bidhaa kamili.

Hata kama haizalishi vipuri vyote kutoka mwanzo, bado ina mchango mkubwa katika kukuza viwanda na uchumi wa nchi.
 
Tanzania tuna uhitaji mkubwa wa magari ya aina hii, size zinalingana na magari yafuatayo
1. Mabasi/Daladala size zote nne (hiace, coaster, Tata, mabasi ya mkoani)
2. Magari ya mizigo size zote 5 (kirikuu, townace, canter tani 1- 3.5, mafuso 10T)
3. Gari za kubeba mchanga size ya canter na fuso
4. Gari za lenye friji ya kubeba vitu vinavyoharibika mapema kama mbogamboga, matunda, nyama, kuku walio chinjwa,samaki, maziwa. Gari za ukubwa wa tani 1-3.5 hadi tani 10
 
Back
Top Bottom