Mkuu,
Inapokuja kwenye biashara ya magari, kwa sasa imekuwa kama zilivyo Computer/Tablet/Phones ambapo Processors watengenezaji ni wachache sana. Hivyo hivyo inapokuja kwenye RAM, Hard Discs, Graphic cards, Sound Cards etc.
Kwenye Engines, kwa sasa nafikiri wengi wananunua kwa Benz na wakati huohuo, na wao anawafyatulia BOSC kama sikosei ila BOSC ndiyo amebaki kuwa mtengenezaji mkubwa wa parts za magari duniani hii ikiwa na maana inapokuja kwenye kucheza na STEELS au ALLOYS kwa ujumla, BOSC wako mbali sana duniani.
Biashara ya magari ni biashara iliyo na matatizo sana kwa leo hii. Viwanda vingi vimeuzwa kwa bei ya take away. Huwezi amini kiwanda kama cha VOLVO ilifika wakati hakuna aliyetaka kukinunua. Mchina mwisho kaamua kuingilia na kukiokoa. Magari ya Hammer ya USA nayo mtambo mzima uliuzwa kwa Mchina baada ya watu wote kugoma kuununua.
Kwa Wanigeria, kama unavyoona hapo picha Mabasi yakiwa barabarani (Asante
Dotworld na
Ritz kwa picha ), haijalishi ni Mabasi ya nani au parts zimetoka wapi. Hapa cha muhimu ni kuwa WATU WA NIGERIA WAMEPATA AJIRA. Kwa sasa inaweza pia kuwa njia nzuri kuwa MUUNDAJI na siyo parts makers. Ukishindwa kununua huku, unanunua kule na wakipandisha sana bei, unazima mtambo wa kuunga magari.
Katika dunia ya leo, hakuna anayejitosheleza kwa kila kitu. Nilishakuwa kwenye bari NISSAN Navara na jamaa akaniambia kuwa hilo gari, ENGINE yake ni ya RENOLT na iko hivyo kwa sababu jamaa wana mkataba wa kushirikiana. Magari kama SKODA na SEAT, engine zake ni Volkswagen ingawa yanatengenezwa Czech na Spain.
Mwanzo kabla sijasoma post yote nilishangaa kidogo, nilijiuliza mbona magari haya yanafanana na magari ya kichina! na kweli ni(CKDs) za Kichina - siwasemi vibaya wa Nigeria nawapongeza. Tuwe wakweli hapa Wafrica mpaka tufikie hatua ya kumimina Engine blocks na ku-manufacture subassemblies zote za Engine mpaka ifikie kufanya kazi sioni kama hilo linaweza kufikiwa in our lifetime, tutaishia kuhunga hunga magari ya wenzetu na kuyapachika a local name lakini sio ku-manufacture magari per se. Nani atakubali kukuhuzia/kukujengea a modern forge an foundry Shops,pattern shops, heat treatment shops, modern labs za material/hardness testing, modern electroplating shops, sophisticated machine tools,R&D nk hivyo ndivyo vitu vya muhimu katika uhundaji wa magari, lakini cha umuhimu zaidi ni skilled labour i.e wenye elimu na uwezo wa kutumia vifaa hivyo effectively.