Kiwanda cha Magari - NIGERIA.

Kiwanda cha Magari - NIGERIA.

Mwanzo kabla sijasoma post yote nilishangaa kidogo, nilijiuliza mbona magari haya yanafanana na magari ya kichina! na kweli ni(CKDs) za Kichina - siwasemi vibaya wa Nigeria nawapongeza. Tuwe wakweli hapa Wafrica mpaka tufikie hatua ya kumimina Engine blocks na ku-manufacture subassemblies zote za Engine mpaka ifikie kufanya kazi sioni kama hilo linaweza kufikiwa in our lifetime, tutaishia kuhunga hunga magari ya wenzetu na kuyapachika a local name lakini sio ku-manufacture magari per se. Nani atakubali kukuhuzia/kukujengea a modern forge an foundry Shops,pattern shops, heat treatment shops, modern labs za material/hardness testing, modern electroplating shops, sophisticated machine tools,R&D nk hivyo ndivyo vitu vya muhimu katika uhundaji wa magari, lakini cha umuhimu zaidi ni skilled labour i.e wenye elimu na uwezo wa kutumia vifaa hivyo effectively.

Mkuu Bukyanagandi ni muhimu ukatambua kuwa kwa sasa manufacturing industry hai-operate kwa jinsi unavyofikiria wewe. Ni watengenezaji wachache wa magari ama hata mitambo mingine wanaofanya kila kitu, sasa hivi manufacturers wengi wanashirikiana ili kurahisisha kazi na kupata product imara na nzuri zaidi.

Kwa mfano Waingereza wana kiwanda kinachotengeneza engines zinaitwa Perkins, hao jamaa wanauza engines zao kwa manufacturers mbalimbali kama viwanda vya zana za kijeshi(kuna baadhi ya vifaru vinatumia engines za Perkins), wanauza engines zao kwa watengenezaji wa tractors kama Massey Ferguson na Farmtrac, vile vile wanauxza engines zao kwa manufacturers wa generators kama Olympian, FGWilson, Marapco, AJPower, SDMO, Jubaili bros n.k

Kama vile ambavyo watengenezaji wa engine za ISUZU wanavyowauzia manufacturers wengine kama wa Forklift, manufacturers wa magari n.k
Kwahiyo ninachotaka kukufahamisha hapa ni kwamba sio lazima manufacturers atengeneze components zote za machine yake ndio aonekane anaweza, unaweza kuchagua baadhi ya vitu vya kutengeneza na vingine ukawapa manufacturers wengine lakini bottom line ni kwamba utatoka na product yako mwenyewe.

Hata Tanzania kama tungekuwa makini kukiendeleza kiwanda cha nyumbu bila shaka sasahivi tungekuwa tunatengeneza magari yetu wenyewe ya kitanzania na kwa kufanya hivyo tungeongeza wigo wa ajira lakini pia tungesaidia sana ukuaji wa teknolojia na ubunifu.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom