Kiwanda cha kutengeneza soda bandia chakamatwa..
============
============
Wakuu,
Kuna tukio limetokea nchi za wenzetu huko Patistan ambalo linahusisha mtu mmoja ambaye ametambuliwa kwa jina la Ali Niswana, akitengeneza soda feki kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Nimeshikwa na butwaa baada ya kupata hizi taarifa, sielewei kuwa tatizo ninini lakini kuna hatari kubwa sana kwa watumiaji wa vyakula na vinywaji kwamaana kila kitu kinachakachuliwa sasa.
Kwa hapa kwetu Tanzania, yawezekana kuna watu wanaotumia mwanya huu kutuumiza na sisi kwa njia hii, watumiaji tujitahidi kuwa waangalifu tunapotumia bidhaa kama hizi ili kama tunazitilia shaka iwe rahisi kushirikisha watu wengine na kupata ukweli wa bidhaa hizi.
Picha mbalimbali za tukio hilo hizi hapa,
![]()
![]()