Kiwanda cha dawa alichozindua Rais Magufuli kipo tangu mwaka 2014, sio kipya

Kiwanda cha kwanza cha dawa za binadamu Mwanza

Maelezo ya hatua kwa hatua ya utengenezaji dawa.
Habari via GSengo Blog -- MKUU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka wamiliki wa viwanda katika mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya viwanda kabla yakufikiria watu kutoka mbali.

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi na kuzindua katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akiweka Jiwe la Msingi na kuzindua katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical cha jijini hapa kilichopo katika eneo la Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze kukifungua kiwanda hicho mapema na shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja. " Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika halafu wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k" huku akimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo pamoja na msafara wake uliojumuisha Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Baraka Konisaga pamoja na madiwani na viongozi wengine ulipata nafasi ya kutembelea idara mbalimbali za uzalishaji kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji wa mazingira, ulinzi wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,

Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.

Prince Pharmaceutical ndicho kiwanda cha kwanza na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.

Moja ya mashine zilizosimikwa kiwandani hapa kwaajili ya uzalishaji dawa.

Ufafanuzi kwa kina.

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alivutiwa na uwekezaji huu wa kwanza kufanyika jijini Mwanza.

Mitambo.

Uzalishaji kwa majaribio tayari umekwishaanza na hii ni moja kati ya sample zitakazo oneshwa kwa wakaguzi wa Viwanda, Chakula na Madawa watakao dhuru kiwandani hapa hivi karibuni kwa ajili ya ukaguzi ili uzalishaji upate kuchukuwa nafasi.

Korido ndani ya kiwanda hicho cha madawa.
siyo hicho tu,Kuna kingine kipo butimba na chenyewe ni cha zamani
 
mkuu, ebu kusanya wajinga wenzako, waone kuwa Magufuli alienda kule kwa ujinga tu wala hakuwa na purpose maalumu, aliamua tu!! angeenda basi kufungua barabara ya Nyerere au airport terminal II

Ungeuliza mkuu!!!! acheni kujivika chuki na ujinga!!

Kiwanda kinaweza kufunguliwa hata mara 100 ilimradi kila mtu anapoenda anaenda na kuna kitu kipya? extension/upgrade?
hadi unatia huruma!!!! kuna siku mtakiri kwa kusema"tumeshindwa kumtetea bwana huyu" haishi vituko
just beat it mate
 
Tutofautishe kuweka jiwe la msingi na kufungua kiwanda.

Hata daraja la Furahisha Kikwete aliweka jiwe la msingi na Magufuli amenifungua.

Tatizo liko wapi. Tunapenda tu kuanzisha negative mada dhidi ya Magufuli kwa sababu mahususi
Umesoma vizuri lakini?
Habari via GSengo Blog -- MKUU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka wamiliki waviwanda katika mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozungukamaeneo ya viwanda kabla yakufikiriawatu kutoka mbali.

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi na kuzindua katika kiwanda cha kuzalishadawa za binadamu
 
Kiwanda cha kwanza cha dawa za binadamu Mwanza

Maelezo ya hatua kwa hatua ya utengenezaji dawa.
Habari via GSengo Blog -- MKUU wa mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo, amewataka wamiliki wa viwanda katika mkoa wa Mwanza kuhakikisha wanatoa kipaumbele cha ajira kwa wananchi wanaozunguka maeneo ya viwanda kabla yakufikiria watu kutoka mbali.

Kauli hiyo ameitoa Jiji Mwanza wakati wa uwekaji wa Jiwe la Msingi na kuzindua katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo akiweka Jiwe la Msingi na kuzindua katika kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical cha jijini hapa kilichopo katika eneo la Buhongwa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.

Katika hatua nyingine Ndikilo amewaomba mamlaka ya Chakula na dawa nchini kuona uwezekano wa kukifanyia ukaguzi ili waweze kukifungua kiwanda hicho mapema na shughuli za uzalishaji ziweze kuanza mara moja. " Ndugu zangu haiwezekani kila kitu kimekamilika halafu wenzetu wa TFDA wanasema watakuja kufanya ukaguzi tarehe ishirini na nane, alisema Ndikilo na kuongeza, lazima wafahamu kuanza kwa kiwanda ni ajira, uzalishaji, ukuzaji wa uchumi n.k" huku akimtaka Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na dawa kanda ya Ziwa kuwasiliana na makao makuu kuona uwezekano wa kufanya ukaguzi wa haraka na kukiruhusu kiwanda hicho kufanya kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Injinia Evarist Ndikilo pamoja na msafara wake uliojumuisha Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula, Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Baraka Konisaga pamoja na madiwani na viongozi wengine ulipata nafasi ya kutembelea idara mbalimbali za uzalishaji kiwanda cha kuzalisha dawa za binadamu cha Prince Pharmaceutical.

Aidha Mkuu huyo wa mkoa, alionya juu ya utunzaji wa mazingira, ulinzi wa kiwanda kwa wananchi wanaozunguka na kuhakikisha wakti wote wanatoa ushirikiano kwa Mwekezaji.

Kwa upande wake mmiliki wa kiwanda hicho, ameupongeza na kuushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza na wilaya kwa ushirikiano mkubwa waliompa tangu alipokuwa na dhamira ya kuanzisha kiwanda hicho hapa mkoani,

Katika kuhakikisha anaunga mkono juhudi za Serikali kuwaletea maendeleo wananchi, Mmiliki wa Kiwanda hicho bw. ametoa Jumla ya Mifuko ya Sementi 100 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya Maabara kwa Shule za Sekondari za Lwanyuma na Buhongwa, zilizopo wilayani Nyamagana sehemu ambayo kiwanda hicho kipo.

Prince Pharmaceutical ndicho kiwanda cha kwanza na cha kipekee katika kanda ya Ziwa, ambacho mara baada yakuanza kazi, kitakuwa Tegemeo kwa wananchi wa kanda ya ziwa na Mikoa ya Jirani na kanda hiyo ikiwa ni pamoja na Nchi Jirani.

Moja ya mashine zilizosimikwa kiwandani hapa kwaajili ya uzalishaji dawa.

Ufafanuzi kwa kina.

Mstahiki Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus Mabula alivutiwa na uwekezaji huu wa kwanza kufanyika jijini Mwanza.

Mitambo.

Uzalishaji kwa majaribio tayari umekwishaanza na hii ni moja kati ya sample zitakazo oneshwa kwa wakaguzi wa Viwanda, Chakula na Madawa watakao dhuru kiwandani hapa hivi karibuni kwa ajili ya ukaguzi ili uzalishaji upate kuchukuwa nafasi.

Korido ndani ya kiwanda hicho cha madawa.
aibu kam kile cha vi
 
kILIWEKEWE JIWE LA MSINGI NA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA ENG NDIKILO ILA SASA RAIS MAGUFULI AMEKIFUNGUA RASMI ILA KINAFANYA KAZI
Kwa hiyo mkuu wa mkoa alifungua nini ? mi nimeshatumia kabisa dawa ya kidonda kutoka hapo kiwandani mwaka jana sasa nashangaa kusikia leo mtu anakuja kupiga nacho selfie eti anafungua... hana kazi za kufanya yule
 
kuna vitu vingi vinatumika na havijafunguliwa... mfano daraja la Kilombero linatumika muda sasa na halijafunguliwa
 
Back
Top Bottom