Kiungo gani katika mwili kina (control) uzee? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kiungo gani katika mwili kina (control) uzee?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Limbukeni, Jun 3, 2009.

 1. L

  Limbukeni Senior Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uzee nikitu kisichoepukika , kinatokana na mchanganyiko wa shughuli nyingi katika mwili zenye uwiano wa moja kwa moja na umri. Moyo wa mwanandamu ndio kiungo kikuu kinachotoa maelekezo kwa mwili juu ya muonekano wake kwa nje. Uso wa mwanadamu kwa muonekano unatoa majibu mengi sana juu ya maswaiba au furaha binadamu aliyonayo. Ukiangalia watu wengi wenye misongo ya mawazo sura zao zinajieleza na wasio na misongo ya mawazo sura zao zinajieleza. Kila mtu anaweza kukumbwa na misongo ya mawazo ila inategemea akili yake inatatuaje hiyo misongo kabla haijaharibu maumbile ya mwili. Kufurahisha moyo na kuupa moyo amani kujizuia kupanic ni afya bora sana ya mwili. Wadau nisaidieni kuchangia hili. Asanteni
   
 2. S

  Simoni Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Oct 10, 2008
  Messages: 67
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Soma pia vitabu vya dini iwe QUran au Biblia vinasaidia sana kuuchangamsha mwili. Soma huku ukitafakari unayoyasoma na kuyazingatia kwa matendo. Very good anti uzee dose.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Ulichesema ni kweli kabisa na hakina ubishi.Kwa kuongezea ni kwamba,ukiwa ni mtu mwenye kuwa na nia mbaya, mawazo mabaya, mtenda maovu, vyote hivi vyaweza kuchangia kuongeza makunyanzi kwenye uso wako.Hivyo basi watu tujiepushe na mawazo, maneno na matendo maovu kwa kadri tuwezavyo.
   
 4. OsamaBinLaden

  OsamaBinLaden JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 706
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  thread yako ni nzuri na nitajaribu kupambanua katika mtazamo wa quran inasema nini kuhusu hili.

  Na kwa upande mmoja unayosema ni kweli.
   
 5. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ooh, nilidhani mtagusia pituitary glands, kumbe mnazungumzia ki -imani kuliko ki -sayansi. Haya, tuendelee...
   
Loading...