Unaamini kuwa Lowasa ni Fisadi? una ushahidi? kama huna alishawaambia pelekeni mahakamani kama hamna "SHUT UP"Msema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi: Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.
Maneno hayo sasa yanakuwa ya uhalisia. Tangu Lowassa ajiunge CHADEMA, pamoja na kinachosemwa kuwa CHADEMA/UKAWA imeongeza idadi ya Wabunge na kuminywa kwa demokrasia, wanaCHADEMA kindakindaki wamekuwa kama 'wamejitenga' na chama chao. Wanakosa hoja za kukosoa masuala ya ufisadi kwakuwa waliyekuwa wakimsema sasa wanaye.
Tangu Lowassa kujiunga na CHADEMA, CCM imeibeba ajenda ya kupambana na ufisadi. Haikuwahi kutokea CCM kutamka hadharani kupambana na ufisadi kwenye kampeni zake au hata kwenye utawala wake kwa kujiamini kuliko kuanzia siku Lowassa alipojiunga na CHADEMA. Ufisadi, kama hoja ya kujidai kwa wananchi, umepokwa na CCM toka CHADEMA!
Kimsingi, hata kama ni kimya kimya, Lowassa anaitesa CHADEMA. Anawabana wasipate cha kusema kuhusu ufisadi. Imekuwa rahisi kwasasa kwa wanachama wa CCM kupindisha kila hoja ya ufisadi toka kwa CHADEMA kwa kusema kuwa hata Lowassa aliyesemwa miaka nenda miaka rudi naye yuko CHADEMA.
Unaamini kuwa Lowasa ni Fisadi? una ushahidi? kama huna alishawaambia pelekeni mahakamani kama hamna "SHUT UP"
Hukuulizwa weweHawa ndio wanapaswa kutoa ushahidi
Hiyo ni Typing error tu, next time jikite kwenye hoja tuKiuharisia au Kiuhalisia?
Usijali mkuu tupo pamoja.Mkuu, hata kama nimeongea pumba kwenye bandiko hili usiache kuniheshimu. Nakuomba sana!
Vyema MkuuUsijali mkuu tupo pamoja.
Sidhani kama huyu MTU ni asset kwa chamaHongera kwa kusema ukweli kijana wangu. Najua utatukanwa lakini,umeongea ukweli mtupu. Kwa sasa wamebaki na hoja moja tu...eti mtu akifa wanasema 'kafa sababu alimsema Lowassa'...ndio hivyo tena toka siasa za hoja hadi siasa za ramli. Kuelekea uchaguzi mkuu 2010 walitangazia umma kuwa chadema haitasimamisha Wagombea kumpinga Sitta,Mwakyembe,Olesendeka kwa jinsi walivyosimamia ufisadi serikalini lakini eti sasa wamekuwa maadui wao...wanasema eti ripoti ya Richmond ilikuwa ni uongo.
kumbe we shabiki nildhani mjumbe wa kamati kuu, peleka ushabiki wako simba na yanga ndo panakufaa
Sema wewe maana tukisema sisi inaonekana tuna bifu naye. Kwa hakika CHADEMA wamenasa pabaya!
Sasa choo kilipokuwa nje ya nyumba chama kilikuwa kikilaani ile harufu chafu ya choo. Leo hii chama kile kile kimekihamishia kile choo chumbani. Je bado wana jeuri ya kulaani ile harufu chafu. Ina maana chama chote KINANUKA harufu ya choo.
Dr. Slaa alisema "wamehamishia kinyesi chumbani", lakini choo kimebaki kule kule yaani (...) kinaendelea kuzalisha kinyesi zaidi.Maneno hayo.aliyesema Dr Slaa wakamuona hafai acha lichama liwadodee
Andika kiswahili ueleweke. Sisi akina nani na tuna mamlaka gani ya kukamata na kushtaki. Nani ana dola?Tuwaulize ninyi mliohubiri kwa miaka 8 Ufisadi wa Bwana fulani lakini mkampokea na kumteua kuwa Mgombea wenu! Niwaulize ni lini mtamfikisha Mahakamani????
Msahihisho mkubwaMsema ukweli ni mpenzi wa Mungu. Humu humu JF nimewahi kuandika hivi: Sikubaliani na hoja ya Lowassa Kujiengua CCM na Kujiunga CHADEMA/UKAWA. Andiko langu hilo, nikiwa kama mtanzania nisiye na chama chochote cha siasa, lililenga kukosoa kujiunga kwa Lowassa huko CHADEMA.