Traveller X
JF-Expert Member
- May 2, 2017
- 271
- 305
Pengine ni stress tu za maisha zinanifanya nishindwe ku enjoy vichekesho vya huyu jamaa kwa maana kila kichekesho chake nnachotazama hua sicheki ama kufurahi kabisa naona kama ni vitu vile vile tu vilivyokosa ubunifu,
Au pengine ni sanaa ya bongo hasa hasa kwenye fani hii ya comedy ndio kusema imekosa ubunifu kabisa siku hizi,kwa maana vitu ambavyo wanatuletea tufurahi naona kama ni vitu vya kawaida mno kiasi kwamba labda mtoto mdogo ambae akili bado haijapevuka ndo anaweza vunjika mbavu kwa kucheka,
Ama pengine ndo kusema akili zetu sisi watazamaji ndo zimevurugwa labda ni kutokana na mambo yanayoendelea kwenye nchi hii na ndio kusema hata tukitazama vichekesho siku hizi akili zetu zinakua zishachoshwa na siasa na changamoto nyingine za nchi hii??
Kiukweli nashindwa kupata majibu,Na hii sio kwa msanii huyu tu ni karibia wasanii wote wa sanaa ya uchekeshaji naona hawana ubunifu kabisa sikuhizi.
Sijui kwenu nyie wadau??