Nataka niwe Shameless! Yaani niwe oil chafu

Rio Shabazz

JF-Expert Member
Jan 18, 2024
1,334
2,169
Kuna staff mwenzetu nilikua nafanya nae kazi yaani yeye ni shameless. Si kwa ubaya lakini najaribu kuonesha tabia yake. Kuna watu ambao ni shameless huwezi msema kwa lolote akadharirika au akaaibika. Hawa wamejitengenezea immunity haogopi, hajali watu wanasema nini, hajali wanafikiri nini ili mradi anachokitafuta anakijua na kukiamini yeye humtoi kwenye reli. Hizi personality zipo kwene sanaa kama vile kina Mwijaku, Baba levo, Juma lokole, Shilole, Mange kimambo na gigy money na wengine wengi ambao sijawataja hapa.

Pia wamo kwenye siasa pia tunawajua wao huwa hawachafuki wala hawachafukiki na kulingana na tabia alojitengenezea basi tabia zimekua zikiwabeba hata linapotokea jambo hamna mtu anajisumbua kuamini au kuliongelea kwa muda mrefu kwasababu inakua si habari maana raha ya vita adui aumie na ujue kua limemchoma.

TURUDI KWENE MAADA…

Mwanzo kabisa nilikuwa naona kama mtu wa hivyo labda hazimo au yuko 9 kasoro ni vile si unajua muungwana lazima uwe na aibu ila si kwa huyu staff! Bahati nzuri au mbaya nikaja baadae kua supervisor wake. Nilimchukia sana kutokana na tabia yake na uwezo wake mdogo kufanya mambo technical. Kifupi si mtu smart sana lakini ni shameless elewa neno SHAMLESS.

JINSI NILIVOANZA KUVUTIWA NA HII TABIA

Kazi yangu hiyo niliyokua nafanya ilitemea watu na ushawishi wa watu na kuweza kujuana na watu tofauti tofauti kwa wakati mfupi na kuanzisha nao mahusiano ya kazi kisha waweze kutaka huduma ambazo tunazitoa. Kifupi ilikua inahitaji akili lakini pia ilihitaji hulka au kariba ya kuweza kuwaface watu, kuongea nao na kuwashawishi kifupi si kazi rahisi kwa mtu mwenye aibu au asiyeweza kuzoeana na mtu fasta na mchangamfu.

Hivo kati ya watu 10 niliokua nikiwasimamia ikaja kuonekana huyu shameless (Jina kapuni) ndiye mwenye perfomance nzuri kuliko wote pamoja na mazingira magumu na sababu lukuki wenzie walizokuwa wanatoa ila yeye matokeo yalikuwa mazuri. Hivyo mambo yakageuka nikajikuta namtegemea kwenye kuninyooshea mambo na kunisafishia CV yangu ya kazi. Kwa ambao washafanya kazi za makampuni utaelewa kwamba kazi zinategemeana Wajuu anamtegemea wa chini hivo kama wachini wanakuangusha naww hamna lolote utalokua unaonekana unafanya.

LAKINI KWANINI KUA SHAMELESS NI MUHIMU?

Katika kujifunza funza nikaja kukutana na hiki kitu. Cheki hapa chini

0E21F5F6-6243-4E13-8B63-E030D7150E18.jpeg


Kuna kitu inaitwa Vibration Energy hii tunaishi nayo kila kitu kinatoka ndani. Katika energy chanya ndio kuna amani, kukubaliana na hali, upendo nk, na energy hasi ndo kuna aibu, kujihukumu, woga, majonzi na hasira. Kama unajua kashule kidogo waweza fatisha uo mchoro.

Hivo bas kua na aibu, hasira, hamu, kujivuna kujisikia si hali ambayo binadamu ameumbiwa ni hali ambayo huleta uharibifu na kuzuia mafanikio ya mtu nikiongelea mafanikio simaanishi pesa au vitu vya kushikkiaka.

Baada ya hapo ndipo nilipoona kua asiye na aibu si mwehu ila yuko level nyingine ya maisha tena level ya juu. Hapa hatumaanishi kujitoa akili kufanya maovu, no.

Ni kufikiria mambo mangap umeyakosa au umefeli kutokana na kuhofia watu wanachowaza au watakuonaje au kuwaonea aibu. Vitu vingap umevikosa kutokana na hasira kujiona na kujisikia? Jibu unalo mwenyewe.

***********************************
6C5BFA4F-6470-4AC5-A07F-08A0D51EFCF7.jpeg

Leo hii nimeacha kazi pale kama miaka mitatu lakini sina namba za wote tumepotezana nao lakinI guess what ni namba yake huyu mtu shameless. Baadae nilivutiwa sana na hii hulka yake ningekua nayo hii ningekua mbali sana.

Nataka nijue nawezaje kuwa shameless?
 
Kuna staff mwenzetu nafanya nae kazi yaan huyu ni shameless

Jaman daah yaan uwiiii huyu n mbwa nyie.Yaan type za kina Gig money au Shilole.
No si kwa ubaya lakini najaribu kuonesha tabia yake.

Mwanzo nilikua naona kama hazimo vile si unajua muungwana lazima uwe na aibu si kwa huyu staff !

Bahati nzuri au mbaya nikaja baadae kua supervisor wake.Nilimchukia sana kutokana na tabia yake na uwezo wake mdogo kufanya mambo technical.

Kifupi si mtu smart sana lakini ni shameless elewa neno SHAMLESS.

***********************************

LEo hii Nimeacha kazi pale kama miaka mitatu lakini Sina namba za wote tumepotezana nao lakin guess what Ni namba yake huyu mtu SHAMELESS.

Baadae nilivutiwa sana na hii hulka yake ningekua nayo hii ningekua mbali sana.

Nataka nijue NAWEZAJE KUA SHAMELESS
Wewe ni ke au me?
 
Back
Top Bottom