Kiukweli Huwa "SICHEKESHWI" na Vichekesho Vya "MKALI WENU (TVE)"

Traveller X

JF-Expert Member
May 2, 2017
271
500
Pengine ni stress tu za maisha zinanifanya nishindwe ku enjoy vichekesho vya huyu jamaa kwa maana kila kichekesho chake nnachotazama hua sicheki ama kufurahi kabisa naona kama ni vitu vile vile tu vilivyokosa ubunifu,

Au pengine ni sanaa ya bongo hasa hasa kwenye fani hii ya comedy ndio kusema imekosa ubunifu kabisa siku hizi,kwa maana vitu ambavyo wanatuletea tufurahi naona kama ni vitu vya kawaida mno kiasi kwamba labda mtoto mdogo ambae akili bado haijapevuka ndo anaweza vunjika mbavu kwa kucheka,

Ama pengine ndo kusema akili zetu sisi watazamaji ndo zimevurugwa labda ni kutokana na mambo yanayoendelea kwenye nchi hii na ndio kusema hata tukitazama vichekesho siku hizi akili zetu zinakua zishachoshwa na siasa na changamoto nyingine za nchi hii??

Kiukweli nashindwa kupata majibu,Na hii sio kwa msanii huyu tu ni karibia wasanii wote wa sanaa ya uchekeshaji naona hawana ubunifu kabisa sikuhizi.

Sijui kwenu nyie wadau??
 

Traveller X

JF-Expert Member
May 2, 2017
271
500
alaf
Mchovu kweli kweli huyo jamaa eti kama Kuna kivideo alicheza anamlazimisha mtu ku do.. Nikamuona Hovyooo kabisa
inaskitisha ndo anapewa kiki kweli kweli,najiuliza tu hamna wakali zaidi yake wakuwaweka pale,kiukweli ni aibu sana
 

Nyotinzuri

Senior Member
Mar 17, 2017
133
250
Sema clip nyng za mkaliwenu zmejaa lugha ya matusi cjui nmeeleweka hapo, kwan sa ingne inaweza ikatokea clip ambayo kwa kweli km upi na watu wazma unaona aibu, ht ebitoke nae cmuelewi sn.
Wote n wauza sura na watafuta kiki kwa nguvu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom